Baadhi ya wapiga debe pale Chato Stand si waaminifu

Gogadiholo

Member
Jul 16, 2021
6
1
Mama mmoja wa umri wa kati ya miaka 65 na 70 alipita pale stand ya mabasi CHATO na kukaribishwa na wapiga DEBE huku wakimhoji anasafiri kwenda wapi. Katika kujieleza mama huyo aliulizia ofisi za NIDA ziko wapi ili akapate huduma ya vitambulisho.

Wale wapiga debe walimuuliza yule mama ni kwa nini amepitia humo stand kwa kuwa stand siyo mahali pa kupitapita ovyo. Mwisho walitoza Tsh 3000 na kumwonyesha njia aende zake.

Wito wangu ni kwenu wapiga Debe wa hapo Chato, mrudishieni huyo bibi hela zake la sivyo yatakayowapata msilaumu mtu. Kama mligawana posho, zichangeni mzirudishe na mtende haki msiharibu kazi yenu.
 
wapiga debe Wa Chato akiwemo diwani Wa kata ya Chato na kuna afisa usalama x hawawezi kumtoza sh 3000 ya kuonesha ofisi za nida.


ingekuwa amekatiwa tiketi kwa bei ya juu sawa, lakini kwa hili haiwezekani.


waombe radhi wapiga debe Wa stendi ya Chato iliyo km 1 mashariki ya alipolala jpm.
 
Back
Top Bottom