Baadhi ya wanyama wahamishiwa hifadhi ya Burigi

Watanzania sometimes tunapenda kulalamika bila kufanya uchunguzi na kujudge picha na video za kwenye mitandao,nilikuwa kwenye hiyo mbuga miezi miwili iliyopita na kweli kuna baadhi ya wanyama ambao ni wengi kwenye hiyo mbuga na baadhi kupunguzwa na kuhamishwa kwenye mbuga nyingine mpya,mbuga mpya imefunguliwa,wanyama wanaongezwa ili waende kuzaliana kwenye mbunga hiyo mpya .


Hayo ni maendeleo,kuna misitu mingi sana hii Tanzania na Mapori ambayo bado hazijaitwa mbuga na kuna wanyama wachache mno,,kuongeza wanyama au kuanzisha mbuga mpya ni akili nzuri sana.
Tuangalie hata baadhi ya mbuga za Africa kusini.
Serengeti ina nyumbu zaidi ya million moja na nusu,unaona wivu nyumbu kumi jinsia tofauti kukamatwa na kupelekwa kwenye mbuga mpya?swala wako wangapi mikumi?Twiga wapo wangapi?
chato iko juuu juuu juuu zaidi
 
Huyu bwana ni mbinafsi na mchoyo kuliko maelezo, kila kitu kwao, teuzi zake nyingi ni watu wa kwao mpaka kichefuchefu
Ni mbinafsi kweli! Wanyama wabaki kanda ya kasikazini tu, kwanini anawapeleka huko Burigi mkoa wa Kagera? Kwanza yeye ni wa mkoa wa Geita! Huoni kwamba huyu ni mbinafsi saana? Pia ni mbinafsi kiasi kwamba amesahau kwamba hifadhi ya Burigi ndiyo pekee duniani ilikuwa na twiga weupe (wa asili). Walimalizwa na majangili. Huyu bwana ni mbinafsi pia amesahau kwamba hifadhi ya Bihalamulo na Buligi zilikuwa na wanyama wengi kuliko Tarangire, Mikumi na Manyara. Mpaka kichefuchefu eti.
 
Pamoja na kwamba jiwe ni mbinafsi, ila kwa hili sioni kama ni kosa. Kwangu huu naona ni utaratibu wa kawaida kuhamisha wanyama kwenda mbuga nyingine. Kwa hili kupitia ubinafsi wake naona kapatia.
1125950
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kuna kitu cha kufikirisha hapa na kila mtu anaweza kuja na mawazo yake, baada ya kuingia mkuu madarakani unaona project kubwa na za kitaifa zinafanyika maeneo yale unakaa unajiuliza awamu za nyuma hawakuona umuhimu wa kupeleka hivyo vitu kipindi hicho au strategy za kiuchumi zikoje kuhusu Chato ? hizo harakati za kuipandish hadhi hiyo hifadhi ina interval ya muda gn like ten or five years? kwanini bandari ya chato inajengwa kipindi hiki na faida zake kiuchumi zikoje? maana yawezekana magu kalazimisha hivi vitu viende kule kwa research yake mwenyew like Tawi la crdb
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko akikagua Miundombinu ya Bandari ya Nyamirembe iliyopo Chato, Geita.
Bandari hiyo inatarajiwa kuwa kitovu cha usafirishaji wa mazao na bidhaa kwa eneo la magharibi mwa Ziwa Victoria na kuwa kiungo hadi nchi jirani.
Capture 11


Capture 12


Capture 13

Bandari ya Nyamirembe kazi imefikia asilimia kubwa toka mkurugenzi wa TPA alipotembelea.
Miradi aliyoitembelea ni pamoja na Bandari ya Nyamirembe iliyoko kijiji na Kata ya Nyamirembe Wilayani Chato

 
Unapoleta habari usilete habari kiushabiki.
Swala la kuhamisha wanyama sio jambo geni wala jipya katika maswala ya ikolojia na uhifadhi.

Na kuweka kumbukumbu sawa, mbuga za taiga zilizotangazwa na TANAPA ni mbili zikitokana na kuunganishwa kwa baadhi ya jumuiya (WMA). Hivyo mbuga zikizoanzishwa ni BURIGI-CHATO NATIONAL PARK na IBANDA-KYERWA NATIONAL PARK. Hivyo kuna baadhi ya wanyama watahamishwa pia kupelekwa Ibanda-Kyerwa itakapobidi, sasa tujiulize kutakua na ubaya au.? au kwa kuwa wamepelekw chato

Rai yangu tusiwe watu wa kuongozwa na hisia bila kuyajua mambo kwa undani wake. Swala la kuanzisha national park husimamiwa na TANAPA na si IKULU.
Usije tegemea habari yyt toka ufipa kuhusu serikali ikaja bila propaganda.
 
Nani anafanya kazi hiyo? Kuwaswaga simba, chui, nyati...nk kuingia huko Burigi?

Ila wizi na wale watekaji watapungua huko sasa.
Nyati, simba, chui wapo wa kutosha labda twiga, tembo na Faru majangiri waliwamaliza.
 
Pananuka ubinafsi. Pambeni mnavyoweza, hapa pana umimi. Mbona Kigoma kuna Malagarasi,.pori kubwa sana, badala ya kuliendeleza, wakawekwa wanyama, limebakia malisho ya ng'ombe za wenzetu toka Shy n.k, wala hakuna anayesema jinsi mazingira yanavyoharibiwa?

Leo tunaona, Kiwanja cha ndege, taa za barabarani mahali ambapo magari ni ya kuhesabu, benki kubwa isiyo na wateja, sasa mbuga ya wanyama, nk, nk. Ubinafsi utaleta baadaye, ukabila na ukanda.
Ila hizo mbuga zipo kagera zote na wala sio chato
 
Hakunaga mbuga isiyo ya asili. Hiyo itakuwa ZOO LA CHATO ...Mungu hakuwa mjinga kuwaweka maeneo waliyopo
 
Back
Top Bottom