Baadhi ya wanyama wahamishiwa hifadhi ya Burigi

we nae ni kilaza kama walivyo vilaza wengine hivi hilo jambo la wanyama kuhamishwa ndo unaliskia leo?
mbona lipo siku nyingi sana?
Au kwasabu ni chato ndo imekua shida?
Kwa sababu ni chato, hizi nyumbu zinadhani chato ipo congo labda.
 
Unapoleta habari usilete habari kiushabiki.
Swala la kuhamisha wanyama sio jambo geni wala jipya katika maswala ya ikolojia na uhifadhi.

Na kuweka kumbukumbu sawa, mbuga za taiga zilizotangazwa na TANAPA ni mbili zikitokana na kuunganishwa kwa baadhi ya jumuiya (WMA). Hivyo mbuga zikizoanzishwa ni BURIGI-CHATO NATIONAL PARK na IBANDA-KYERWA NATIONAL PARK. Hivyo kuna baadhi ya wanyama watahamishwa pia kupelekwa Ibanda-Kyerwa itakapobidi, sasa tujiulize kutakua na ubaya au.? au kwa kuwa wamepelekw chato

Rai yangu tusiwe watu wa kuongozwa na hisia bila kuyajua mambo kwa undani wake. Swala la kuanzisha national park husimamiwa na TANAPA na si IKULU.
Pananuka ubinafsi. Pambeni mnavyoweza, hapa pana umimi. Mbona Kigoma kuna Malagarasi,.pori kubwa sana, badala ya kuliendeleza, wakawekwa wanyama, limebakia malisho ya ng'ombe za wenzetu toka Shy n.k, wala hakuna anayesema jinsi mazingira yanavyoharibiwa?

Leo tunaona, Kiwanja cha ndege, taa za barabarani mahali ambapo magari ni ya kuhesabu, benki kubwa isiyo na wateja, sasa mbuga ya wanyama, nk, nk. Ubinafsi utaleta baadaye, ukabila na ukanda.
 
Hili la wanyama kuhamishwa kwenda huko huenda lina mkono wa ubanafsi wa kimadaraka lakini ni jambo la kawaida na litakalokuwa na tija huko mbeleni. Tendo la kuhamisha wanyama limekuwa likifanyika, japo sio kwa msukumo huu wa sasa lakini sio jambo gani.

Nakumbuka twiga walisafirishwa kwenda nje enzi za JK kwa usimamizi wa kina Nyalandu, tukapiga kelele na hakuna lolote tulifanya, kama hawa wanahamishiwa hapa hapa nyumbani japo kuna ubinafsi ndani yake lakini kuna afadhali. Kwa madhaifu ya katiba yetu ni nadra kuzuia ubinafsi wa watawala wetu, lakini kama jambo halina madhara kwenye haki za binadamu inabidi tukubaliane nalo tu hata kwa shingo upande.

Ni dhahiri hapo karibu kuna uwanja wa ndege umejengwa na ni kodi zetu na hatuwezi kuzuia. Ni bora hao wanyama wapelekwe maana ni jambo la kawaida hata huo uwanja utumike kuleta watalii kuona hao wanyama. Kinyume na hapo hata hao wanyama wasipopelekwa uwanja ni tayari na hela umekula.
 
Hivi Chadema vichwa vyenu vimevurugwa? Hii Tanzania yetu wote. Je wale waliokuwa wanapakiza Twiga na kupeleka nje ya nchi mbona hamkuleta Uzi hapa? Hizi ni Mali hasiri zetu woote kama taifa na kuhamisha wanyama toka mbuga moja kupeleka nyingine ni kawaida
 
Mkuu unachosema kinaweza kuwa sahihi, lakini kwa nini iwe Chato, nasio hifadhi nyingine yeyote nchini?.
Una uhakika na unachokisema?
Kuna hifadhi nyingi zinawekewa wanyama ili kuendeleza ikolojia na kuhakikisha kunakua na 'balance of nature'.
Mfano kama kwenye hifadhi hakuna predators in hatari kwa hiyo inabidi predators wapelekwe ili kucontrol idadi ya 'herbivores'.
Hili linafanyika hifadhi nyingi hapa nchini...Sio kila kitu ukitizame kisiasa
 
August 6 ,2018
Chato Beach Resort alama ya uzuri
Ukiwaza Geita, picha ya haraka inakuwajia kichwani ni machimbo makubwa makubwa ya dhahabu. Kamwe huwezi kuwaza kuwa kuna beach ambayo unaweza kupumzika. Daily News Digital gazeti rasmi la serikali la Kiingereza Tanzania linakuletea uzuri wa mkoa wa Geita kupitia Jukwaa la Fursa za Biashara

Source : Daily News Digital
 
Mliokuwa mnapinga ujenzi wa airport Chato mnaona hiyo mambo?
Chato inaenda kugeuka Serengeti B
Aaah wapi mkuu hata Pinda alijengewa uwanja wa ndege huko Sumbawanga watalii waende huko mbugani katavi umeiona kilichotokea ni uwanja kugeuka kuwa Batolite ya Mobutu.
 
Tuchangie kwa hoja... Tujadili faida na hasara za huu mradi... Tujaribu kukua kidogo kimawazo..
 
Kwa haya niliyoyaona kupitia hii video iliyopo mtandaoni,nakiri huyu mtu ni mbinafsi na anapendelea sana kwao kuliko hata hao wachaga.

Ubinafsi mwingine ni ule wa kutaka yeye tu ndio aonekane na kusikika na si mtu mwingine yoyote.,

Hakika ukitaka kujua tabia halisi ya mtu, ngoja mtu huyo apate pesa au madaraka.
Hiyo video imepotoshwa.
Wanyama walikuwa wanapelekwa burigi hifadhi hii ipo kagera huko wilaya ya muleba.na
 
Pamoja na kwamba jiwe ni mbinafsi, ila kwa hili sioni kama ni kosa. Kwangu huu naona ni utaratibu wa kawaida kuhamisha wanyama kwenda mbuga nyingine. Kwa hili kupitia ubinafsi wake naona kapatia.
Animal migration is natural happened,uwo uhamishaji wa magari unaonekana hujui unachokiandika ndugu
 
Aug 11, 2018
Chato ilivyojipanga kufaidi fursa za nchi za Maziwa Makuu na EAC
Mkurugenzi Mtendaji wa Mhandisi Joel Hari wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato anaeleza mipanga iliyoandaliwa ili kuweza kunufaika na jiografia yake ambayo iko kifursa zaidi .Msikilize anavyoelezea wakati serikali ya mkoa wa Geita ikijiandaa na Jukwaa la Fursa za Bishara zililoandaliwa kwa kushirikiana na Tanzania Standard Newspapers Limited, wachapishaji wa magazeti ya Daily News, HabariLeo, SpotiLeo na kuendesha mitandao ya kijamii (Facebook, twitter na instagram).
 
Back
Top Bottom