Baadhi ya wanafunzi kutumia "Surnames" za makabila zisizo na staha ya Kiswahili haitaleta ukakasi wakija kuwa viongozi wa umma??

ahahahahahaha dah! yani unazaliwa ukoo unaitwa mk.u.ndu???
japo sishangai nishawahi soma na mtu aitwa kumalija
 
Mkuu usichanganye Utandawazi, Kiswahili na Lugha za Asili hayo majina mengi yana maana zake kwa asili na ywezekana Kiswahili pia , wewe unasoma kwa Kiswahili pekee ndio maana inakuletea taabu ( tena ni kwa kuwa wewe una majina ya Wakoloni) Mbona majina ya Wakoloni huoni ubaya wake Mfano John Stones( Stones= Mawe), Daniel Drinkwater( Maji ya Kunywa), Danny Rose, Raheem Sterling, Kelvin Trippier, Calum Chambers, Snodgrass, Westgate, Eastgate, Gareth Southgate, woodburn, Rice, Hazard( hatari), Redman, Grealish, nk mbona huoni ubaya wake?

Hapa Burundi kwa majirani zetu majina yao ukisoma kwa Kiruri, Kijita au Kikwaya ni Matusi/ Viungo vya Siri ukienda kwa Bondeni/ Afrika Kusini majina yao ni taabu kuyatamka. Ebu fikiria nje ya Sanduku na utoke huku Utumwani ulikojifungia!
 
Duh!, hayo majina nakumbuka tulishawahi rudisha balozi wa Mozambique kwao sababu ya jina alikuwa anaitwa ka.k.um.a
 
Sasa mkuu, kati ya kiswahili na lugha ya asili ya kabila ni ipi lugha inayounganisha taifa na inaongelewa sana na watanzania??


Lugha za asili zina nguvu sana, hata Kiswahili kimetokana na lugha za Kibantu/Kiasili hatà wewe unajiita ".....Nkosazana" unajua maana yake kwa Kiswahili? kwanini uponde majina yetu?
 
Mboro, bora haya ni majina ya wachaga kibosho, machame nk mboro haina shida sana maana kiungo chenyewe ni shadidi na jasiri, ila matako, mkundu aisee noma sana, majina yanabadilishwa na hakuna mtu akikua anaweza kubali kutumia jina hilo ndo maana hao kina mkundu huwezi wasikia ila mboro au mbora hazina shida kabisa na wapo wengi tu.
 
Wazeeeee nao hawajielewi kwakweli,haya majina ya ukoo wangeyaficha na kutumia jina la kawaida mwisho.

eg:Juma Ally Mohammed...ingependeza.

Sasa mtoto nae akaitwe mnduku si balaaaaa.
 
Kumpa mtoto jina kama hayo unakuwa practically umemlaani. Hawezi kusimama siku moja mbele ya watu na kuomba kura kwa nafasi ya uongozi fulani. Hata wenye kuteua hawawezi kumfikiria hata kama ana uwezo. Kuna Balozi wa Zambia aliwahi kupendekezwa na nchi yake kuiwakilisha hapa Tanzania lakini Tanzania ikamkataa kwa sababu jina lake lilikuwa halitamkiki (tusi) katika Kiswahili. Angalau huyo hakuwa Mtanzania. Kuwa na Mtanzania ambaye jina lake ni tusi katika Kiswahili ni unthinkable.
Elewa Surnames mara nyingi ni jina la ukoo mtu husika. Mf. Mboro ni ukoo
 
Back
Top Bottom