Baadhi ya wanafunzi kutumia "Surnames" za makabila zisizo na staha ya Kiswahili haitaleta ukakasi wakija kuwa viongozi wa umma??

MuganyiziMushiMwaipopo

JF-Expert Member
Oct 14, 2018
281
500
Ahahaaa Umenikumbusha O-level alikuja Mwanafunzi tokea Rwanda Sir name yake ilikuwa ni K siku hiyohiyo ameripot tayari alikuwa ashajulikana shule nzima...
 

Mgayajr

Member
Aug 22, 2016
17
45
Naomba namimi niweke mchango wangu juu ya majina,

Ki uhalisia sisi ni waafrica wenye tamaduni zetu, tunapaswa kufahamu ya kwamba mwanadamu anayo icon yake ambayo inapaswa kuwa tofauti na mtu mwingine yeyote,

Icon hiyo huwa ni jina ambapo jina kamili la mtu ni lazima yawe matatu

Jina lako wewe, jina la baba yako, na jina la ukoo

Jina lako yawezekana ikawa ni lile ambalo ulipewa na wazazi wako ukiwa mdogo au pengine ulilibadilisha wewe mwenyewe kisheria kwa kuapa mahakamani

Jina la kati ni lazima liwe la baba yako mzazi labda kuwe na uhuni mama yako alifanya lakini lazima jina la baba yako mzazi ndo liwe katikati

Jina la mwisho ambalo ni la tatu ni lazima liwe la ukoo ili kukutofautisha na mtu mwingine

Mfano Jerico Simon Mgaya hili ni jina pekee ambalo siyo rahisi kumkuta mwingine ana jina kama hilo

Lakini ukiandika, Jerico Simon wapo wengi tu

Au hata Jerico Mgaya wapo wengi pia

Kwa hiyo kinachotofautisha hapo ni kati na ukoo

Nije kwenye umuhimu wa ukoo

Ukoo ni muhimu sana kwa sababu katika maisha yetu ya Leo tunazunguka sana kutafuta

Leo na kesho umekutana na msichana anajitambulisha kwa majina mawili mf Angel Simon umempenda umeshamzoea kabisa binti na unawaza kwenda kujitambulisha kwao

Kumbe ni Angel Simon Mgaya ni Dada yako wewe umechelewa kumhoji vizuri hadi ushalala naye

Kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Yocktan Jackson Hosea

Ana majina matatu kweli lakini jina la ukoo hakuna nimejaribu kumhoji hilo jina la ukoo hajui chochote

Sasa na yeye ni MTU mzima na anawatoto wake he unafikiri anao uwezo wa kuwafundisha wanae?

Kwa hiyo kumbe hata huyo Angel Simon na Jerico Simon wanaweza kuoana kwa sababu hilo jina la ukoo wote hawalitumii na hawalijui kabisa

Naomba tuwafundishe watoto wetu kuyatumia majina yetu yote matatu

Na hii ni kanuni yetu kisheria ila waliotuharibu ni waarabu wametufundisha visivyo

Ruksa kukosoa lakini siyo matusi

Asanteni
Elewa Surnames mara nyingi ni jina la ukoo mtu husika. Mf. Mboro ni ukoo
Huku Manzese Kuna jamaa anaitwa "Kundugeni"
pia maeneo ya Buza nyama choma Kuna dalali anaitwa "Khamis Nguo gani" na mwingine Mtoro wa kufikia wa ma mdogo anaitwa "Dotto Mumewangu"
 

Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,596
1,250
Kwanza matako na mkundu kwa Kiswahili ni maneno sahihi kabisa tena kwa maana yanashikamana vema.

Pili kuna majina mengi ambayo (kwa bahati nzuri) hayaeleweki kabisa kwa Kiswahili hata hivyo wako wengine wenye majina ya aina hii wamekuwa mashuhuri kabisa.

Namkumbuka Bwana Sykes (je unaelewe maana ya jina lake? Huogopi labda maana ya ajabu?).
Menginevyo Tanzania tunasimamiwa na Bwana Pombe. (tatizo?)

Kama mwenye jina ana tatizo na jina lake ana njia ya kulibadilisha. Kama wewe una matatizo na majina ya wengine, aibu yako.
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,040
2,000
Kumpa mtoto jina kama hayo unakuwa practically umemlaani. Hawezi kusimama siku moja mbele ya watu na kuomba kura kwa nafasi ya uongozi fulani. Hata wenye kuteua hawawezi kumfikiria hata kama ana uwezo. Kuna Balozi wa Zambia aliwahi kupendekezwa na nchi yake kuiwakilisha hapa Tanzania lakini Tanzania ikamkataa kwa sababu jina lake lilikuwa halitamkiki (tusi) katika Kiswahili. Angalau huyo hakuwa Mtanzania. Kuwa na Mtanzania ambaye jina lake ni tusi katika Kiswahili ni unthinkable.
Hakuna mtoto anapewa surname.... Utapewa first name mengine NI by default
 
Top Bottom