tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Nimesikiliza majadiliano ya wana Diaspora walioko Marekani hasa jimbo la Washington DC wakiwa na Mhe Tundu Lissu akieleza namna alivyoshambuliwa na hali kisiasa na kidemokrasia nchini huku akiruhusu maswali kutoka kwa baadhi ya watanzania.
Katika hali ambayo ilionekana kabisa kukwera nayo ni baadhi ya wanadiaspora kutofautiana na msimamo wa Lissu kuhusu kupigwa kwake risasi kwa kuhitumu serikali npasipo kuwa na ushahidi wowote ukizingatia yeye Lissu ni Mwanasheria nguli tu.
Maswali hayo yamekuwa yakimkera sana na kuanza kujibizana na muuliza maswali hata kabla ya kumaliza kuuliza swali.Lissu amekuwa akieleza kuhusu tukio kama vile ana ushahidi wote wa tukio na kutaka kuwaaminisha wanadiaspora kuwa serikali ya Tanzania ni mbaya sana na ya kinyama sana na huku tunaishi kama vile tuko jehanamu yaani ni vitishi vitupu katika maelezo yake kiasi cha kushauri basi na wanadiaspora wengine kuwa kama hali ni hiyo basi usirudi huko omba ukimbizi huku Marekani.
Lakini katika maelezo yake yeye Lissu anasema atarudi tu pale madaktari wake watakapo mwambia kuwa sasa uko mzima kurudi nyumbani na huku akisema dunia yote itajua kuwa Lissu sasa anarudi nyumbani na kutaka serikali imlinde 24/7
Nadhani kutofautiana na wanadiaspora kwa msimamo wake huo ndiyo utamfanya aonekane mijadala yake baadhi ya watz kutoshiriki kwa maana ya kutafuta solution kama kweli kuna matatizo.
Nadhani atakuwa anapambana na maswali magumu kila mkutano wake anaofanya na kama kweli anajua kila kitu kilichotokea kwanini anaogopa kusema na hata kuwataja hao ambao anasema akiwataja basi watauwawa siku inayofuata.
Lissu kuna kitu nadhani anakitafuta katika kujenga hizo hofu kwa watz na propaganda anazozieneza. Sijasikia hata Serikali moja duniani ikisupport chochote kuhusu Lissu pamoja na maneno yake yote hayo ya kusema kuwa ni serikali ndiyo imefanya jaribio hilo.