Elections 2010 Baadhi ya wana-CCM Arusha wajiandaa kufanyakazi na utawala mpya wa Dr. Slaa!!!!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Jana jioni nilipata nafasi ya pekee ya kukutana na viongozi na wakereketwa wa chama tawala na kwa mbali walionyesha kukataa tamaa.

Waliniuma sikio kuhusu taarifa za siri za idara ya usalama wa taifa kuwa zinawakatisha tamaa kwa sababu vijana ambao ni asilimia sitini na tano ya wapiga kura wote wanamkubali Dr. Slaa kwa asilimia sabini na mikoa kumi na tano ambayo ndiyo yenye kura turufu ya Uraisi asilimia sitini ipo beneti na Dr. Slaa.

Hata hivyo jamaa zangu hawa wa karibu wanajivunia ya kuwa ushindi wa Dr. Slaa ni asilimia hamsini tu yaani bado ni kiduchu na atapaswa afanye kazi nao CCM kwani hatakuwa na kile walichokiita "overall mandate"

Yaani eti Dr. Slaa hatavuka asilimia hamsini na kuonyesha kukubalika nchi nzima. Wanasema watamdhibiti Bungeni kwani huko taarifa hizi zawapa matumani angalau ya kuongoza kwa idadi ya wabunge na hivyo kutoa Waziri Mkuu na kuunda sehemu kubwa ya baraza la mawaziri........Chadema wanapaswa kuwasaidia wagombea wao wa ubunge kama nia ni kuunda serikali nje ya CCM................

Mikoa ambayo inawapasua CCM bongo ni hii hapa Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar-Es-Salaam, Iringa, Morogoro, Iringa, Mbeya, Rukwa, Pwani, Singida na Dodoma kwa mbali.

Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma jamaa zangu hawa wa karibu walidai mambo ni swafi haswa yaani CCM ni 40%, CUF 30 na Chadema 20%.

Mikoa mingine jamaa zangu wanadai wapo salama. Hivyo umtegemee JK kuzuru hiyo mikoa 15 mara kwa mara kupunguza makali ya Dr. Slaa.

Yaani nilishtuka mno.

Ila kilichonisikitisha walinilaumu kuwa mimi na wana-CCM wengine wenzangu waliotubatiza jina bandia la wasomi eti tumekisaliti chama chetu.

Lakini jamani, ukweli si upo wazi? Sisi CCM kazi yetu ilikuwa ni kuleta uhuru kazi ya kuujenga uchumi historia yabainisha upinzani wataifanya shughuli hiyo vyema.........

Dr. Slaa kwenye hotuba yake ya kuapishwa Uraisi ninamwomba sana awe muungwana na atupungeze CCM kwa kuleta uhuru hata kama kazi ya uhuru wa kiuchumu tumeboronga.

Ni hayo, tu wanajamvi wenzangu..........
 
Yaani ndugu yangu yaani leo sikupata usingizi. Hawa watu siyo wadogo hata kidogo. Ukiona wanalia basi tu.
 
Ni kweli, lakini CHADEMA lazima tufanye kazi kubwa sana kulinda hizo kura. CCM are very smart in chakachuation...
 
CCM kinachowauma ni kuachia ngazi ya ulaji serikalini wala siyo kusikitikia kuwa watapoteza nafasi ya kuleta maendeleo ya nchi hii
 
Wanataka kutupeleka kusiko...Wakubali kwamba hakuna marefu yasiyo na ncha..
Hivyo zama zao ziko ukingoni...
 
Kwa Selemani.

Tatizo siyo kuwa watanzania hawapo tayari kuwaweka Chadema madarakani bali ni uchakachuaji wa kura tu ndyo karata turufu ya CCM
 
Wana JF,

Mikoa ambayo inawapasua CCM bongo ni hii hapa Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar-Es-Salaam, Iringa, Morogoro, Iringa, Mbeya, Rukwa, Pwani, Singida na Dodoma kwa mbali.
Je Mwanza - Rock City

Kweli hiyo mikoa kwa wana CCM ni pasua kichwa full halina ubishi ilo swala kwani ndani ya wana CCM tuseme ukweli tumegawanyika sana tokana na tofauti zetu kwa mambo fulani fulani mengine sisi wana CCM hatuyapendi au kuyafumbia macho kwa kuogopa au kwa kutokujua katiba yetu ya chama na kuhoji au kuhofia vitu fulani.

mfano navyo sikia huko Arusha kuna mpasuko kwanza kwa UVCCM wilaya wenyewe na kutengwa katika harakati za kampeni za Batilda na wengine kuhamia ati kambi ya aliye kuwa mbunge wao wa zamani Felix Mrema na kuhisi kuwa wana tupa nguvu nyingi kwa mgombea wa CHADEMA G.Lema.

Pia nasikitika sasa katika uchaguzi huu kwani huko Arusha kumewaka moto TAKUKURU leo ni siku ya 5 wanakanusha tuu tuhuma ya kutomkamata Batilda kunani wao kila kukicha kwenye vyombo ya magazeti na kuongelea issue ya Batilda au wao ndio walio haribu deal ya kumbamba Batilda kuota rushwa kwenye hivyo vikao vyao vya ndani wansema??

 
Tuamke tuache ushabiki. Yote yanawezekana kwa kupiga kura. Hakuna wenye umiliki wa Tanzania zaidi ya watanzania wenyewe. Vote for Dr. Slaa!
 
Wana JF,

Je Mwanza - Rock City


Hata mimi nashangaa! Hivi kweli UWT wanaweza kupuuza mkoa wa Mwanza ambao ni miongoni mwa mikoa inatakayochangia katika uamuzi wa nani awe rais? Nashauri kwamba, mikakati mikubwa ya Dr Slaa ielekezwe katima maeneo ambayo amekubalika zaidi na ambayo yana watu wengi watakaopiga kura. Kanda ya Ziwa yote, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Magharibi na kusini magharibi. Sehemu za kusini amwachie Kikwete na Prof huko wanakubalika zaidi.
 
Kama hii habari ina ukweli, sidhani kwamba Serikali ya CCM inaweza kukubali matokeo hayo kirahisi. Bila shaka hivi sasa Serikali ya CCM kwa kushirikiana na vyombo vyake kama UWT wanatafuta kila njia ya kuhakikisha CCM inashinda at any cost. Just wait and see!
 
Kama hii habari ina ukweli, sidhani kwamba Serikali ya CCM inaweza kukubali matokeo hayo kirahisi. Bila shaka hivi sasa Serikali ya CCM kwa kushirikiana na vyombo vyake kama UWT wanatafuta kila njia ya kuhakikisha CCM inashinda at any cost. Just wait and see!


Dr.Slaa kwa sasa anatakiwa kufanyia kazi mambo mawili;
  1. Ateue kamati itakayoanza kazi ya kuchambua wataalamu waliopo nchini na nje ya nchi watakaounda serikali yenye tija kwa wananchi.Tanzania ni kubwa sana lazima apate human resource ya kutosha maana kumbukeni miaka mitano ni kiduchu anaweza asitimize anayosema
  2. ahakikishe kura za wapiga kura zinathaminiwa hasa kwa maeneo mbayo chadema haina wagombea ubunge na udiwani,.Tafadhalini muwatendee haki wapiga kura kwa kulinda kura zao.Tumieni gharama yoyote
  3. Aunde kamati ya wataalamu wa kubuni mikakati ya kulinda kura CCM wanayo mikakati zaidi ya sita ya kuhakikisha ushindi lazima chadema wawe na anti-CCM strategies
 
Chief--we hope utakuwepo hapa ukumbini siku matokeo yakitangazwa.

Teh teh teh. Nashauri baada ya uchaguzi na baada ya matokeo kamili kutangazwa, kila member aitwe jina na ajibu nipo ama sipo. Nina hakika tunaweza kupata watu wawili ama watatu waliojinyonga kwa hasira. Teh teh teh. :becky:
 
Hiyo stronghold ya Opposition ni sawa kabisa. Ndio maana piga ua lazima kikwete atarudi tena Iringa, Mbeya, Arusha na Moshi. Ila kuna mikoa unaweza ukabaki kinywa wazi kuishngaa eti Ruvuma nako kuna mtu alipita bila kupingwa kama si matatizo ninini! naupenda ule moto wa pale Iringa mjini maana hata baada ya JK kwenda yule mama Mbege sijui wala asijidanganye eti kukubalika! Kuna pastor pale anatisha nilimsikia siku moja kwenye Redio akihojiwa ni balaa! sasa hao ndo tunaowataka sio wanaosinzia mjengoni.
Pamoja sana!
 
... Dr. Slaa kwenye hotuba yake ya kuapishwa Uraisi ninamwomba sana awe muungwana na atupungeze CCM kwa kuleta uhuru hata kama kazi ya uhuru wa kiuchumu tumeboronga.

Ni hayo, tu wanajamvi wenzangu..........

Wana ccm wote wangekuwa wazalendo kama wewe ... nji hii ingepaa kwa hakika!
 
Dr.Slaa kwa sasa anatakiwa kufanyia kazi mambo mawili;
  1. Ateue kamati itakayoanza kazi ya kuchambua wataalamu waliopo nchini na nje ya nchi watakaounda serikali yenye tija kwa wananchi.Tanzania ni kubwa sana lazima apate human resource ya kutosha maana kumbukeni miaka mitano ni kiduchu anaweza asitimize anayosema
  2. ahakikishe kura za wapiga kura zinathaminiwa hasa kwa maeneo mbayo chadema haina wagombea ubunge na udiwani,.Tafadhalini muwatendee haki wapiga kura kwa kulinda kura zao.Tumieni gharama yoyote
  3. Aunde kamati ya wataalamu wa kubuni mikakati ya kulinda kura CCM wanayo mikakati zaidi ya sita ya kuhakikisha ushindi lazima chadema wawe na anti-CCM strategies

Dr Slaa anakubalika sana mijini, lakini kila jitihadi inabidi ifanyike ili aweze kuwafikia watu wa vijijini pia kwani sera za Chadema zinakubalika kote. If not Dr Slaa, then other Chadema leaders must visit teh villages too.
 
Back
Top Bottom