Baadhi ya Walokole na Wasabato tumekuwa na tabia za ajabu sana

GREAT NAME

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
932
1,249
Habari za leo,

Hizi dini kwa sasa zimekuwahazivutii kabisa tofauti na zamani hasa hawa wanaojiita walokole.

Wamekuwa na vijitabia vya ajabu ajabu katika maisha yao ya kila siku sio wote ila wengi wao ni wanafiki, wachonganishi, wachoyo na wanapenda kujionesha kwa watu kuwa wao ni wema lakini rohoni ni tofauti.

Na sisi wasabato wa siku hizi tumekuwa wa hovyo kupita maelezo ubishi, kujifanya kila kitu tunajua sisi wakati sisi wenyewe hatufuati sheria za MUNGU.

Tubadilike kwa sababu tunajidanganya wenyewe, tunasoma biblia kwa kukurupuka sana na vimjadala vya uchochezi.

MUNGU anataka tuokoe sio tuangamize. Atutangulie na atupe akili ya uelewa kila mmoja wetu.
 
Mimi nina jirani yangu Msabato tokea ahamie hapa tuna miaka kumi na ushee lakini sijawahi kumuona yeye wala famila yake na vitabia vya ajabu ajabu..msema kweli ni mpenzi wa mungu..Walokole wao huwa wanapenda kuhubiri kwa jazba huku jasho likiwatoka hata kama yuko peke yake.

Mimi nikimuona mtu anawaasa watu wasifanye madhambi au akiwa anawaita kwenda Msikitini kufanya Ibada hujisikia raha sana rohoni mwangu.
 
Mimi huwa nikimuona mfuasi wa dhehebu lolote anataka hata muonekano wake wa nje ufanane na imani yake basi huwa najua kuna udhaifu mkubwa ndani yake(uasherati, wizi, unafiki,nk) anauficha kwa kivuli cha uumini wake
 
izo jamii zinajihisi(gi) ni malaika na sie tulio baki ni wafuasi wa shetani ila ukweli zina kasoro nyingi sana

kwa kufanya matendo maovu kwa kujificha ziko njema, kumsikiliza baba mchungaji kuliko mme/mke ama baba/mama jinga sana.
Kweli kabisa ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ya hawa watu wanaojiita manabii tatizo kubwa sana hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
izo jamii zinajihisi(gi) ni malaika na sie tulio baki ni wafuasi wa shetani ila ukweli zina kasoro nyingi sana

kwa kufanya matendo maovu kwa kujificha ziko njema, kumsikiliza baba mchungaji kuliko mme/mke ama baba/mama jinga sana.
Dhambi zooote alizozikataza Yesu_walokole ndio wanazikumbatia na kuziishi mkuu eg,majivuno,unafki,fitina,uchoyo,chuki,majungu...ni watu wa hovyo kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mlokole mmoja aliniambia kuwa kwa dini niliyokuwepo siwezi kwenda peponi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo sasa Muisilamu mujahidina atakubebea panga na kukuambia wewe ni Kafir,Mroma atakuita heathen au pagan,Mhindu atakuambia "veve golo taenda kuliwa nyama na Lord kali",Myahudi atakuita wewe ni jentail,..bora mdomo uende kinywani wewe ishi vizuri tu na watu kwa mujibu wa amri kumi za Mungu.
 
Kuna ile imani nyingine ambayo ukishajiunga nayo tu ww ni peponi automática hua wanajiona wao ndio the chosen one huku wakuwa na maroho mabaya kupindukia.


Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Msichana wangu wa kazi za ndani aliingia dhehebu flani la kilokole la nabii flani.Ajabu akawa baada ya muda anakwenda maombi ya usiku.
Siku moja nikamuuliza mwanangu hivi ni kweli maombi ni usiku tu?
Siku moja nikaenđa kwa siri sehemu wanapoabudia usiku sikukuta mtu ila sikumshushua kesho yake.
Siku moja nikamuuliza huwa mnaombea wapi akaniambia kanisani nikamuambia mbona nilikwenda kanisani kwenu sikuona mtu akaniambia siku zingine huwa tunakwenda kwenye majumba ya watu.Nikamuambia mbona nilimuuliza mchungaji wenu maana tumesoma naye darasa moja akasema hakuna kitu kama hicho?.akainama chini kwa aibu.
Nikaamua kumuondoa kwangu nikamrudisha kwao nisije pata lawama kwa wazazi wake.
Baada ya miezi mitatu nikapata habari ni mjamzito na kweli wazazi wake walinijia juu mtoto wao kaharibikia kwangu sikumchunga.
Nikamjibu mama yake maana naye mlokole ningemkataza kwenda kanisani pia mngenilaumu nendeni kamuulizeni mchungaji wake.
Siku moja nikakutana na binti nikamuambia naona ulichokuwa unakitafuta umekipata sasa nenda kwenye mataifa uhubiri habari hii njema.
Ninavyoandika habari hii ameolewa na muumini mwenzake wa kanisa hilo.
WAARABU HUJUANA KWA VILEMBA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi imani zilizopo Ambazo ni Abrahamic hazina noma ila kuna imani zimeanzishwa hizo ndio ziko njiani zinakuja hizo ukiweza kwenda kuishi msituni peke yako basi jiandae.
 
Shida ya mtu mmoja mmoja unataka kuifanya ni ya jamii nzima.Taratibu za hizo dini ziko wazi sasa mtu anapoenda kinyume chake haimaanishi ndo watu wote wa hizo dini wako hivyo sasa unapowashutumu wote kupitia mawazo yako na hisia zako binafsi huo ni ujinga.
 
Back
Top Bottom