Baadhi ya wabunge wapo kwa ajili ya kukamilisha akidi bungeni

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,427
32,193
Kwa mfano kuna mbunge kama Livingston Lusinde, Mama Salma Kikwete na Naibu Spika ndugu Tulia Akson hao ni baadhi tu hadi muda huu sijaona michango yao yenye tija kwa Taifa zaidi ya kuitumia pesa ya mlipa kodi vibaya kwa posho na mishahara wanayolipwa hawana tofauti na watumishi hewa.

Lusinde hata anachosimamia hakieleweki yeye kazi yake kashfa tu ktk jimbo lake la Mtera raia wake wapo hoi mno.

Huu uzi uwe special kwa wabunge wafanya madudu tunawaona sana tu na sarakasi zao.

Nikikumbuka Lissu na kambi nzima ya upinzani walivyopinga Sheria ya mafuta na gesi kupitishwa bila kupatiwa muda wa kusoma wakina Lissu walilazimika hadi kutoka nje lakini CCM walipitisha sasa hivi wanajidai kuhuzunika juu ya hiyo mikataba ya hovyo.

Nitaendelea kuwaleta tu
 
Wabunge wa ccm isipokuwa Bashe na Nape wengine hasara tuu kazi yao kugonga meza
Ila nape toka apigwe chini uwazir kabadilika mkuu mwanzo alikuwa sio chanzo cha kufunga bunge live huyu
 
Fafanua kwa ushahidi
Lusinde ana elimu ya darasa la saba tu na ana cheti cha Uongozi kutoka Chuo cha CCM cha Ihemi.

Kati ya mwaka 2010 – 2014 vyama vya Upinzani havijafanya kazi kubwa ya kisiasa katika jimbo la Mtera na hata Mbunge wake Livingstone Lusinde hajasifika kwa kufanya jambo lolote kubwa katika jimbo hilo. Wananchi wa Mtera na maeneo ya Dodoma ni kati ya wananchi wenye vipato vya chini sana hapa Tanzania na hakujawa na mikakati bayana ya kukuza vipato vyao kupitia sekta za kilimo na ufugaji.
 
Mwaweza kusema mnalotaka lakini 2020 sio mbali. Tunategemea kuyarudisha majimbo yoote na kukomboa mengi tu ya upinzani. Mfano, Arusha mjini, Mbeya mjini, Kigoma yote mnategemea nini?? Wabunge hao waanze kujitafutia kazi nyingine kama kuigiza filamu
 
Mwaweza kusema mnalotaka lakini 2020 sio mbali. Tunategemea kuyarudisha majimbo yoote na kukomboa mengi tu ya upinzani. Mfano, Arusha mjini, Mbeya mjini, Kigoma yote mnategemea nini?? Wabunge hao waanze kujitafutia kazi nyingine kama kuigiza filamu
Akili za kuku hizi toka 1961 hadi 1995 majimbo yote yalikuwa chini ya chama kimoja umewahi kusikia kulikuwa hakuna shida ya maji safi,umeme na barabara?

Ipi faida ambayo mtanzania ataipata kama majimbo yote yakiwa chini ya chama kimoja?

Ni mjinga tu anaeweza kuwaza kumiliki sio kutatua kero.
 
Kuna Joseph Musukuma huyu amna kitu kabisa,Siku moja anasema hajasoma ila anawazidi hakiri waliosoma, ajui kwamba kuna watu wapo kwaajili ya kuakikisha anaishi salama,wataalamu wamejichimbia mahabara kutafuta tiba za magonjwa mbalimbali.
 
Back
Top Bottom