Baadhi ya Wabunge wa Upinzani wadaiwa kujipanga kuhamia CCM

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Messages
5,158
Points
2,000

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2013
5,158 2,000
Kumekuwepo na taarifa za uhakika kutoka CCM na baadhi ya watu kuhusu mpango wa baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani kutaka au kutakiwa kuhamia CCM kabla ya mwezi wa nane mwaka huu kwa sharti la kupewa nafasi ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM October 2015 au ubunge wa viti maalum vya wanawake au rais.

Hawa ni wabunge ambao wanajua kuwa hawatapewa tena nafasi ya kugombea ubunge kupitia vyama vinajumuisha UKAWA.
Baadhi ya Wabunge hao ni:
1/John Shibuda(Maswa Mashariki-CHADEMA)
2/Said Arfi(Mpanda kati-CHADEMA)
3/Hamad Rashid(Wawi-CUF)
4/Augustino Mrema(Vunjo-TLP)
5/Leticia Nyerere(Viti maalum-CHADEMA)
6/***Baadhi ya wabunge wa viti maalum kutoka CUF, CHADEMA, TLP na UDP.

Mpango huu unasemekana umekuja makusudi baada ya wabunge hao kutaka kuhakikishiwa nafasi za ubunge kwa kuwa tayari wamekuwa wakionekana wakiisadia CCM kisiasa na kuonekana ni wasaliti na mamluki wa Upinzani.

Baadhi ya wabunge hao walikuwa tayari kuhamia ACT na ADC lakini wana hofu kubwa sana kisiasa kwa kuwa vyama hivyo havionyeshi nguvu kubwa ya kuweza kupambana na UKAWA tofauti na ilivyotarajiwa.

Inasemekana Augustino Mrema yeye anataka CCM isiweke kabisa
Mgombea jimbo la Vunjo ili aweze kupambana na Mbatia wa NCCR, John Shibuda anataka CCM imuhakikishie nafasi ya pekee ya kugombea Maswa naye atahamia.

Hali ni tete kwa Saidi Arfi na Hamad Rashid ambapo wamehakikishiwa ubunge na Waziri Mkuu Pinda lakini haijulikani kwa namna ipi, na inabashiriwa labda wa ubunge viti kumi vya urais kama CCM itashinda tena nafasi ya urais.
Mpaka sasa inafahamika kuwa Hamad Rashid atahamia ADC ili kugombea urais wa Zanzibar na pia Said Arfi kuhamia ACT ili kugombea ubunge wa mpanda kati japokuwa yuko njia panda sana kutokana na nguvu hafifu sana ACT katika jimbo lake.

Mpango huu ni sehemu ya mwendelezo uleule wa Zitto kuja kugombea Kigoma mjini ili kuliachia jimbo la Kigoma Kaskazini kwenda CCM lakini unaelekea kukwama kwani Peter Serukamba tayari amejipanga kugombea tena Kigoma mjini na wakati huo huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Kaborou naye anajipanga kutaka kugombea Kigoma Mjini.

Baadhi ya wadadisi wanasema Zitto ametumika kama Kitangulizi cha kuandaa mazingira, kupima upepo na kuvutia wengine kufuata mkondo lakini mpaka sasa bado haijakidhi matarajio yao na hivyo wengine wameanza kusitasita kwa woga.
Pia inaelezwa kuwa mipango hii ingekuwa rahisi na yenye mafanikio kama tu, mgombea urais wa CCM angekuwa tayari amepatikana kuliko ilivyo sasa ambapo hakuna umoja wa kweli kwa viongozi waandamizi wa CCM kwa kuwa kila mmoja yuko mbio mbio na urais.
 

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2014
Messages
3,311
Points
2,000

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2014
3,311 2,000
Sisi kama chadema hatuwezi kuwazuia wafuasi wetu kujadili issues, so wale wote wanaoleta hoja zao humu hatuwezi wazuia ni maoni yao, sasa, hao wabunge hawana madhara yoyote hata wakihama, hata tukipoteza majimbo yao hakuna shida,
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2008
Messages
5,136
Points
2,000

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2008
5,136 2,000
Kwani muda wote wa ubunge wa Shibuda si alikiwa kama yuko Ccm?? Hakuna tatizo hata sasa akijitoa. Mpanda ni Chadema sio Arfi hivyo Ccm isijidanganye kwamba Arfi atashinda at any cost
 

cos p

Member
Joined
Apr 4, 2015
Messages
63
Points
0

cos p

Member
Joined Apr 4, 2015
63 0
Mmeanza propaganda nyie wachaga,saccos yenu imebuma ndo maana wabunge wenye akili wanawakimbia,mda si mrefu atabakia Mbowe na Mkwe wake Mtei
Mambo mengine yanafurahisha kweli, kweli kwa akili zako unaona hao ndo wabunge wenye akili? au hujala jamaa yangu, utabaki wewe na mkeo kushabikia upumbavu..
 

Forum statistics

Threads 1,391,862
Members 528,498
Posts 34,092,324
Top