Ukichambua vizuri, asilimia kubwa ya wana JF ni Chadema au wanaipenda CDM hata kama si wanachama. Nawaomba sana wana CDM na woote wanaoipenda CDM humu JF muwe makini sana kuchangia hizi hoja, manake kuna njia nyingi sana adui anazitumia kukulainisha. Chuki za wana CDM (baadhi yao) kwa Mh. Zitto Kabwe zinawafanya CCM wapate habari nyingi sana za kukichambua CDM na kupata data kamili za kukiangamiza 2015.
Kabla hamjashtuka, mtakuwa mmekwisha na umoja wa CDM utakuwa ni ndoto kuchukua nchi 2015. Ukifuatilia vizuri, CCM kwa sasa wanapigana sana kurudisha heshima ya chama iliyopotea miaka takribani saba iliyopita (kipindi cha Rais Kikwete) kutokana na makundi. Gharama ya kurudisha umoja huo ni kubwa sana na sometimes usipokuwa makini by the time unarudisha umoja huo, it will be too late, kinachobaki ni kusema TUNGEJUA!
Msiingie kwenye mtego wa kukipeleka chama cha CDM kwenye makundi, kwani itawagharimu sana kurudisha umoja huu. WATCH OUT!
Lakini hapa issue ni ufisadi,Zitto atoe tamo kama hahusiki, zitto alianza kubadilika alipopewa kuwa mwenyekiti kamati ya madini