'Baadhi ya wabunge CCM wanafiki'

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
'Baadhi ya wabunge CCM wanafiki'
Na Mwandishi Wetu

MFANYABIASHARA maarufu wa Zanzibar, Bw. Mohammed Raza, amesema unafiki wa baadhi ya wabunge wa CCM katika kuzungumzia mambo yenye maslahi kwa umma, unatoa nafasi kwa wapinzani wanaozungumza ukweli kung'ara katika medani ya kisiasa.

Bw. Raza ambaye pia ni kada wa CCM, amesema kashfa ya ufisadi iliyoikumba Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ni mfano mzuri ambao baadhi ya wabunge wa CCM, walitaka kuifunika, lakini wa upinzani, wakaianika.

Alisema hayo jana Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na Majira, kuhusu kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya fedha, ulioikumba BoT.

"Wabunge wa CCM wafike mahali pa kuzungumza ukweli kwa mambo yanayohusu maslahi ya umma, waache unafiki unaosababisha wapinzani kung'ara kisiasa kutokana na kuzungumza ukweli na mfano ni huu wa kashfa ya ufisadi ndani ya BoT," alisema Bw. Raza.

Alisema wabunge wa CCM wana wajibu wa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, kwa kumweleza mambo ya ukweli yanayohusu wananchi na Taifa lao kwa jumla.

"Wanapaswa (wabunge) kujua, kwamba uongo wao kwa wananchi, unakigharimu chama chetu kwa kukimbiwa na wanachama wanaotaka kusikia ukweli," alisisitiza.

Katika mazungumzo yake, Bw. Raza alimpongeza Rais Kikwete kwa kuchukua hatua za ujasiri katika kushughulikia ufisadi ulioikumba BoT.


"Rais Kikwete amefanya kitendo cha ujasiri mkubwa mno katika kushughulikia kashfa hii ya ufisadi ndani ya BoT, kwa hakika ameirejeshea Tanzania heshima yake," alinena Bw. Raza.

Alisema kwa hatua hiyo, Rais Kikwete ameonesha jinsi Serikali yake inavyosikia vilio vya raia wake hasa katika mambo ya msingi.

Mfanyabiashara huyo alisema hata hivyo, kashfa hiyo, isielekezwe kwa Dkt. Daud Balali peke yake, kwa sababu inahusisha watu wengi.

Pia aliishauri Serikali kushughulikia matatizo ya kiuchumi, ili kuwawezesha wananchi kuishi maisha yanayoridhisha.

"Hali ya maisha ya wananchi walio wengi ni mbaya kwa kweli na hilo linatokea wakati wachache wanaishi maisha ya kifahari sana," alisema.

Kuhusu ghasia zilizoikumba Kenya, Bw. Raza alisema wakati umefika kwa Rais Mwai Kibaki, kujiuzulu ili kuirejesha nchi hiyo katika amani na utulivu.

"Kibaki anajua kuwa mshindi katika uchaguzi wa Kenya ni Raila Odinga na chama chake cha ODM, iweje yeye sasa anataka kung'ang'ania kiti kile wakati hakushinda," alisema.

Alisema litakuwa jambo la burasa kama Rais Kibaki kwa kuzingatia umri wake, ataamua kumpisha Bw. Odinga kuongoza Kenya, hatua ambayo alisema itamaliza mvutano na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.
 
Mtu wa Pwani,

Huyu Raza anatafuta ugomvi na Kingunge Ngombale na vigogo wengine ndani ya ccm?

CCM na ufisadi ni watoto mapacha, ukianza kupondea ufisadi ukiwa ndani ya ccm basi siku zako zinaanza kuhesabiwa.
 
'Baadhi ya wabunge CCM wanafiki'
Kuhusu ghasia zilizoikumba Kenya, Bw. Raza alisema wakati umefika kwa Rais Mwai Kibaki, kujiuzulu ili kuirejesha nchi hiyo katika amani na utulivu.

"Kibaki anajua kuwa mshindi katika uchaguzi wa Kenya ni Raila Odinga na chama chake cha ODM, iweje yeye sasa anataka kung'ang'ania kiti kile wakati hakushinda," alisema.

Alisema litakuwa jambo la burasa kama Rais Kibaki kwa kuzingatia umri wake, ataamua kumpisha Bw. Odinga kuongoza Kenya, hatua ambayo alisema itamaliza mvutano na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Raza nimekusikia sana, Sidhani kama Kibaki anajua kuwa Raila ndie Mshindi...
 
sio baadhi, bali ni wote. nitajie wa sisiem asiyekuwa mnafiki. na ni wezi wakubwa ambao wanaona ufisadi ukiendelea ila wanaubariki kwa kuupigia kula. mimi hata mbunge wangu sina hamu naye na atakuwa na kibarua kigumu kuniridhisha ni jitihada gani alifanya baada ya ufisadi kuonekana unaendelea.
 
Wote tu ni wanafiki wakubwa kabisa si tu hawastahili kuwa wabunge bali hata mabalozi wa nyumba kumi kumi. Walichoweka mbele ni maslahi yao na ya CCM hata kama kufanya hivyo ni kuiangamiza Tanzania.
 
Hata Raza ndio walewale tuu,Hizo ni kauli za kutafuta pa 'kutokea'kisiasa.
 
kwa kweli Raza siku hizi alikuwa kimya mda mrefu, huenda anajiandaa kwa uchaguzi wa 2010.

si mnajua kuwa aligombea kule mkwajuni kwa swahiba wake komandooo na wakamnyima walau kura moja.

sasa amewajengea kule sehemu ya hospitali yao na hivi mkuu anaonyesha jinsi alivyo mzalendo.

ila sijui kama ushuru analipa vyema kwa mambo yake yanayopita bandarini na sijui ile kampuni yake ya zat jee haifanyi manuva kuiibia smz?
 
Maneno yake ni mazito sana,

However, ni vigumu kuamini nia yake kwa sababu huyu pia alishirikiana na Salmin, kuiba uchaguzi wa mwaka 1995 kama alivyofanya Kibaki, lakini hakuona vibaya ila ameona sasa kwa sababu yuko nje ya mlo wa power au?
 
Maneno yake ni mazito sana,

However, ni vigumu kuamini nia yake kwa sababu huyu pia alishirikiana na Salmin, kuiba uchaguzi wa mwaka 1995 kama alivyofanya Kibaki, lakini hakuona vibaya ila ameona sasa kwa sababu yuko nje ya mlo wa power au?


Hii inaprove usemi wa wahenga, "Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu" au "Nyani haoni shaurile". Naona memory ya Raza si nzuri kwani ni majuzi tu alishiriki kumsaidia kipenzi chake kumwibia Maalim kura!
 
Raza nimekusikia sana, Sidhani kama Kibaki anajua kuwa Raila ndie Mshindi...

Kibaki anajua fika kwamba Raila Odinga ni mshindi, dalili za kujua hilo ni matokeo ya viti vya wabunge. Katika hali ya kawaida na katika hali kama ilivyotokea Kenya isingekuwa rahisi mpiga kura akamchagua mbunge toka ODM na akamchagua Kibaki kuwa rais.
 
Hii inaprove usemi wa wahenga, "Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu" au "Nyani haoni shaurile". Naona memory ya Raza si nzuri kwani ni majuzi tu alishiriki kumsaidia kipenzi chake kumwibia Maalim kura!
Memory yake ni nzuri tuu kama walivyo watawala wetu wengi hapa Tanzania. Ila wanalodhani wao ni kuwa sisi ndio ambao hatuna uwezo wa kutunza kumbukumbu ya yanayojiri ndani ya nchi yetu baada ya kutupa vitenge na T shirt.
 
FMES,Heshima kwako mkuu!
Naona umenisaidia sana kwani kinachotokea kenya ndicho kilichotokea Zanzibar,Lakini Raza hakuweza hata kutoa kauli ya kupinga.
 
Raza naye ni mnafiki tu na ni miongoni mwa mafisadi walionufaika na ufisadi wa CCM. Sioni mantiki ya kumpongeza rais anapotimiza wajibu wake. Kuna sabau ya kumwambia baba yako asante kwa kunipeleka shule? nafikiri hakuna kwani huo ni wajibu wake kama mzazi. Ni wajibu wa JK kama rais kulinda uchumi na kutokomeza rushwa katika taifa analolioongoza. Kwa hiyo Raza sioni mantiki ya pongezi zako. Nongempongeza rais kama angemsimamisha kazi Mramba na Meghji na kuwafuta kazi wakurugenzi na waasibu wote wanaoshughuklikia EPA account
 
hiyo ndio siasa ya kwetu, jina likififia unaweza ukatafuta nitoke vipi?

huenda pia ndugu yetu Raza baada ya kukaa nje na kuwa mbali na mlango wa Ikulu tofauti na wakati wa Swahiba yake amejifunza kutubu na sasa yuko tayari kuwa mkweli na mzalendo.

na nnaasikia kuna nyepesi siku hizi amekuwa CUF ila ni wachini chini kulinda maslahi yake ila weshamshtukia wenziwe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom