Baadhi ya waandishi wa habari wanatia aibu

Wakulonga

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
729
1,000
Katika hali ya kushangaza mwandishi wa habari wa gazeti la msema kweli ameshindwa kutofautisha matumizi sahihi ya neno AJUZA mpaka kafikia kumwita mwanaume mzee Ajuza. Hii inaonyesha ni jinsi gani tasnia ya habari inavyopoteza weledi wake siku hadi siku.

Msema Kweli.jpg
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,414
2,000
Nilidhani journalist ethics zimerukwa kama ni mambo ya typing ngoja wenzako waje wakuunge mkono.
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,915
2,000
Gazeti lenyewe hata hatulijuwi,je litakuwa na waandishi wa maana na wenye ujuzi?
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
6,834
2,000
Kwani maana ya ajuza ni nini? Mimi nilikua nafikiri ni mtu kama Bashite na genge lake. Ama mtu anayejiengua CHADEMA na kuhamia CCM. Kumbe ina maana nyingine? Hebu tujuze boss wangu
 

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
4,970
2,000
Kama mnataka Kiswahili bora basi na taaluma husika ifundishwe kwa Kiswahili, maana huwezi muandaa mtu katika lugha ya kigeni aje afanye kazi katika lugha ya asili, tatizo kubwa pia waandishi wetu hawataki kujifunza kuhusiana na lugha, tatizo kubwa zaidi hata waswahili wenyewe hawathamini Kiswahili chao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom