Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2020 - Zitto Kabwe

Mkuu ww endelea kulala, uzalendo uchwara haukutoi kwenye karne hii ya 21. Hivyo vitabu vya kiafrika soma ww, yeye anasoma kitabu kwa kuangalia maudhui bila kujali ni cha mwafrika au mzungu. Ingia hapo Library ya UDSM ukaone vitabu vya wazungu ni vingapi na vya waafrika ni vingapi, na vinaongelea nini. Ukifanikiwa kujua uje ulete mrejesho.
Hivyovitabu ni vyamabeberu, zaidi nimbinu zakutukandamiza waaafrica, na kwatarifa yako ukienda kwao huko hamna anayevisoma hivyovitabu mwaka mziimaaa, ndiomaana wanaovunja rekodi ya kuvisoma ni akina zito tuuu. Sisi tunataka vitabu vinavyoelezea uafrica wetu ilitupate maendeleo yasiyotegemeziii
 
Hata Mugabe alisoma vitabu vingi tu lakini alishindwa kuwanasua raia wake katika dimbwi la umasikini na badala yake aliongeza matatizo katika nchi. Mwafrica mweusi atakuwa mtumwa mpk siku ya mwisho ya dunia, Ni natural order hatuwezi kuiepuka.
 
Kwani Mugabe kusoma kwake vitabu ndiko kulisababisha ashindwe kuwanasua raia wake kutoka dimbwi la umasikini?
 
Mwaka 2020 nimejaaliwa kusoma vitabu 16 (2019:34, 2018:49), ni Orodha ndogo sana kulinganisha na miaka ya nyuma. Hii ni kwa sababu shughuli nazo zimekuwa nyingi, ikizingatiwa kuwa ulikuwa Mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Muda mrefu tumeutumia barabarani, Vijijini na Mitaani kuzungumza na wananchi. Pia kusoma Taarifa fupi fupi za tafiti za Uchaguzi na pia kuweza kuzalisha Ilani ya Uchaguzi ya Chama ambayo Mwaka huu kwa msaada mkubwa wa Kamati za Ilani tulikuwa na Ilani bora sana kote Jamhuri ya Muungano na Zanzibar.

Vile vile nimesoma ripoti nyingi za Serikali, mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF na majarida yenye maarifa mengi, Mfano Foreign Affairs ambalo hutoka mara 6 kwa Mwaka. Hata hivyo nashukuru sana nimejikongoja mpaka kufikia vitabu 16.

Mwaka 2020 kilichapishwa Kitabu ambacho kina Sura ambayo nimeandika. Kitabu hicho ni THE NEW SYSTEMS READER: Alternatives to a Failed Economy, Edited by James Gustave Speth na Kathleen Courrier. Sura niliyoandika inazungumzia Ujamaa baada ya Miaka 50 ya Azimio la Arusha (The Arusha Declaration: The Case for Democratic Socialism 50 years on).

Mwaka 2021 nitafanya jitihada kubwa kuandika kitabu kinachosimulia haswa Maisha yangu katika Siasa za Tanzania Katika miaka 15 iliyopita. Ni matamanio yangu kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 Kitabu kitakuwa dukani. Mungu atupe uhai, In Sha Allah.

Vitabu vya 2020

Riwaya

Mwaka 2020 nimesoma riwaya 6 tofauti tofauti, za watunzi wa Tanzania na Nje ya Tanzania. 50% ya riwaya hizo zimeandikwa na Watanzania sio tu wanaochipukia Lakini wanaoimarika sana katika uandishi. Naona fahari sana kuwa talanta ya uandishi wa riwaya za kusisimua bado ipo nchini, licha ya mazingira magumu ya Kazi za uandishi. Riwaya nilizosoma Mwaka huu ni Pamoja na;

1. An Orchestra of Minorities: Chigozie Obioma

2. Borderlines: Michela Wrong

3. Beneath Lion’s Gaze: Maaza Mengiste

4. Rafu: Fadhy Mtanga

5. Fumbo: Maundu Mwingizi

6. Tuzo: Fadhy Mtanga, Lilian Mbaga, Maundu Mwingizi, Laura Pettie na Hussein Tuwa

Wasifu (Biographies and Autobiographies)

Mwaka 2019 tulibahatika kupata vitabu vya baadhi ya Viongozi wetu nchini. Rais wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin Mkapa aliandika Wasifu wake. Kabla ya hapo Marehemu Mzee Njelu Kasaka, aliyekuwa Mbunge na Katibu wa Kundi la G55 lililotaka Serikali ya Tanganyika alitoa kitabu chake pia.

Mwaka 2020 Wanazuoni waandamizi Prof. Issa GulamHussein Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dkt. Ng’wanza Kamata walikamilisha Juzuu 3 za Maisha ya Mwalimu Julius K Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania. Juzuu ya 4 ipo njiani. Kazi kubwa na ya kuthaminiwa sana ambayo Wanazuoni wetu wamefanya. Kitabu hiki chenye Juzuu 3 (kimsingi ni vitabu 3 vinavyoweza kusimama vyenyewe) kilitoka wakati muafaka sana kwa kizazi chetu. Sio tu ni kitabu cha kusoma na kumaliza bali ni Kitabu rejea kwa Miaka mingi ijayo.

Mwaka huu pia Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Steven Bwana alichapisha kitabu cha Maisha yake. Kitabu hiki kinasimulia Maisha ya Jaji Bwana kuanzia Kijijini kwao mpaka ustaafu na maono yake kuhusu Tawi la utoaji haki (judiciary) katika Ujenzi wa Taifa. Mwaka 2020 umemalizika kwa kazi iliyosubiriwa kwa hamu kubwa ya Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama. Kitabu kizuri Sana kuhusu Mweusi huyu wa kwanza kuwa Rais wa Taifa kubwa duniani.

Wasifu niliosoma Mwaka huu ni Pamoja na;

7. Julius Nyerere, A Biography: Saida Y Othman, Ng’wanza Kamata na Issa G Shivji

8. Maisha Yangu, Utumishi Wangu: Steven J Bwana

9. A promised Land: Barack Obama

Nilisoma pia Mchanganyiko wa vitabu mbalimbali kama kawaida. Ni katika kuongeza maarifa na kuendelea kujifunza kutoka sehemu mbalimbali za Dunia. Pia katika kujifunza makosa ya wengine ili kutorudia makossa hayo. Vitabu mchanganyiko mwaka huu ni pamoja na;

Vitabu Mchanganyiko

10. Asia aspirations, Why and How Africa Should Emulate Asia -- and What It Should Avoid: Greg Mills, O Obasanjo Et al

11. The Naked Diplomat, understanding Power and Politics in the Digital Age: Tom Fletcher

12. Taxing Africa, Coercion, Reforms and Development: Mick Moore, et al

13. Homo Deus, A brief history of tomorrow: Yuval Noah Harari

14. The Promise of Canada, People and Ideas that have shaped our country: Charlotte Gray

15. How to lose a Country, The Seven Steps from Democracy to Dictatorship: Ece Temelkuran

16. The Room Where it Happened, A White House Memoir: John Bolton

Mwaka 2020 ulikuwa mwaka wenye changamoto nyingi sana zitokanazo na janga la COVID 19 (Korona) mpaka Uchaguzi mbovu kabisa kupata kutokea katika historia ya Tanzania. Hakika hapakuwa na Uchaguzi kwa maana ya Uchaguzi bali operesheni Maalumu ya kusaga saga demokrasia ya Vyama vingi Nchini. Kwangu Binafsi namshukuru Mungu kwa kunisuru na ajali niliyopata Oktoba 7, 2020. Ilikuwa miujiza. Mungu mkubwa Sana.

Nawatakia kheri katika kumaliza mwaka 2020 na kila la kheri katika mwaka 2021. Nawashawishi kupata muda wa kujisomea japo kitabu kimoja kila mwezi. Kusoma ni kurutubisha ubongo. Tunaoweza kuandika pia tuandike.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Dar es Salaam
Disemba 26, 2020

View attachment 1659446View attachment 1659447View attachment 1659448View attachment 1659449View attachment 1659450View attachment 1659451View attachment 1659453View attachment 1659454View attachment 1659455View attachment 1659456
Pamoja na kusoma vitabu vyote hivyo lakini ubunge CHALIII !!!!! Havikusidia hata kidogo zaidi ya kutishia kuloga watu.Vitabu soma lakini uwekeze kama Bw.Sugu au hela zote ziliishia kwenye vibonde maji ?
 
The only reason mtu ataweza afford muda wa kusoma vitabu ni kama hafanyi kazi za hand to mouth. Bahati mnaya wengi wetu ndiyo tunazifanya
 
Kwani Mugabe kusoma kwake vitabu ndiko kulisababisha ashindwe kuwanasua raia wake kutoka dimbwi la umasikini?
Hapana point yangu kwa mtu mweusi hata asome vp bado hana uwezo wa kutatua changamoto zilizomzunguka, sisi watu weusi kuna vitu tupo vizuri na ni bora tujikite huko mfano katika tasnia ya burudani, kwanini bwana Zitto asifungue bendi akatuburudisha na kama siasa hata ukiwa mwanamuziki unao uwezo wa kuwa mwanasiasa.
 
Naona hicho cha "Naked Diplomat" umeamua kumchimba Bernard Membe. Haina noma jombaa
 
Hapana point yangu kwa mtu mweusi hata asome vp bado hana uwezo wa kutatua changamoto zilizomzunguka, sisi watu weusi kuna vitu tupo vizuri na ni bora tujikite huko mfano katika tasnia ya burudani, kwanini bwana Zitto asifungue bendi akatuburudisha na kama siasa hata ukiwa mwanamuziki unao uwezo wa kuwa mwanasiasa.
Mtu mweusi ni nani na utajua vipi huyu ni mweusi na huyu si mweusi?

Na je, hao unaosema watu weusi wote tabia zao ziko sawa?
 
Kusoma bila kuelimika au kupata maarifa chanya ni kubaki na ujinga pamoja na hulka yako pasipo kubadilika. Lakini pia si kila tunachosoma kinatufaa katika mazingira yetu na utamaduni wetu. Kila mtu na kila jamii ina mitazamo tofauti na maisha tofauti.
Hongera sana Mr Zitto unanipa hamasa sana kwa namna unavyoweza jipambanua kwa kuitumia vyema talanta yako ya siasa hususani katika kujiongezea maarifa.

Umeanza vyema sana na nilitegemea utamaliza vyema zaidi kwa namna ulivoukoleza uzi wako. Kitendo chakusema uchaguzi ulikuwa wa hovyo ndipo umeharibu zaidi maana nikheri usingelisemea hilo kabisa na lisiwepo katika uzi wako kwani, wengi tumeshuhudia yaliyotokea juu yenu na kusema ukweli! Hamkujipanga vyema kushika dola na matokeo mliyoyapata yalikuwa ndio mategemeo ya mlichokipanga na kukosa mshikamano ndani yenu.

Uzi ni mzuri sana lakini ulivyoumalizia, wengine tunaweza kusema unapiga porojo tu tukuone msomi kwakuweka vitabu konki ilihali hata vitabu viwili haujasoma na pengine umeishia kushika vichwa vya habari!!.
 
Mwaka 2020 nimejaaliwa kusoma vitabu 16 (2019:34, 2018:49), ni Orodha ndogo sana kulinganisha na miaka ya nyuma. Hii ni kwa sababu shughuli nazo zimekuwa nyingi, ikizingatiwa kuwa ulikuwa Mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Muda mrefu tumeutumia barabarani, Vijijini na Mitaani kuzungumza na wananchi. Pia kusoma Taarifa fupi fupi za tafiti za Uchaguzi na pia kuweza kuzalisha Ilani ya Uchaguzi ya Chama ambayo Mwaka huu kwa msaada mkubwa wa Kamati za Ilani tulikuwa na Ilani bora sana kote Jamhuri ya Muungano na Zanzibar.

Vile vile nimesoma ripoti nyingi za Serikali, mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF na majarida yenye maarifa mengi, Mfano Foreign Affairs ambalo hutoka mara 6 kwa Mwaka. Hata hivyo nashukuru sana nimejikongoja mpaka kufikia vitabu 16.

Mwaka 2020 kilichapishwa Kitabu ambacho kina Sura ambayo nimeandika. Kitabu hicho ni THE NEW SYSTEMS READER: Alternatives to a Failed Economy, Edited by James Gustave Speth na Kathleen Courrier. Sura niliyoandika inazungumzia Ujamaa baada ya Miaka 50 ya Azimio la Arusha (The Arusha Declaration: The Case for Democratic Socialism 50 years on).

Mwaka 2021 nitafanya jitihada kubwa kuandika kitabu kinachosimulia haswa Maisha yangu katika Siasa za Tanzania Katika miaka 15 iliyopita. Ni matamanio yangu kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 Kitabu kitakuwa dukani. Mungu atupe uhai, In Sha Allah.

Vitabu vya 2020

Riwaya

Mwaka 2020 nimesoma riwaya 6 tofauti tofauti, za watunzi wa Tanzania na Nje ya Tanzania. 50% ya riwaya hizo zimeandikwa na Watanzania sio tu wanaochipukia Lakini wanaoimarika sana katika uandishi. Naona fahari sana kuwa talanta ya uandishi wa riwaya za kusisimua bado ipo nchini, licha ya mazingira magumu ya Kazi za uandishi. Riwaya nilizosoma Mwaka huu ni Pamoja na;

1. An Orchestra of Minorities: Chigozie Obioma

2. Borderlines: Michela Wrong

3. Beneath Lion’s Gaze: Maaza Mengiste

4. Rafu: Fadhy Mtanga

5. Fumbo: Maundu Mwingizi

6. Tuzo: Fadhy Mtanga, Lilian Mbaga, Maundu Mwingizi, Laura Pettie na Hussein Tuwa

Wasifu (Biographies and Autobiographies)

Mwaka 2019 tulibahatika kupata vitabu vya baadhi ya Viongozi wetu nchini. Rais wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin Mkapa aliandika Wasifu wake. Kabla ya hapo Marehemu Mzee Njelu Kasaka, aliyekuwa Mbunge na Katibu wa Kundi la G55 lililotaka Serikali ya Tanganyika alitoa kitabu chake pia.

Mwaka 2020 Wanazuoni waandamizi Prof. Issa GulamHussein Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dkt. Ng’wanza Kamata walikamilisha Juzuu 3 za Maisha ya Mwalimu Julius K Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania. Juzuu ya 4 ipo njiani. Kazi kubwa na ya kuthaminiwa sana ambayo Wanazuoni wetu wamefanya. Kitabu hiki chenye Juzuu 3 (kimsingi ni vitabu 3 vinavyoweza kusimama vyenyewe) kilitoka wakati muafaka sana kwa kizazi chetu. Sio tu ni kitabu cha kusoma na kumaliza bali ni Kitabu rejea kwa Miaka mingi ijayo.

Mwaka huu pia Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Steven Bwana alichapisha kitabu cha Maisha yake. Kitabu hiki kinasimulia Maisha ya Jaji Bwana kuanzia Kijijini kwao mpaka ustaafu na maono yake kuhusu Tawi la utoaji haki (judiciary) katika Ujenzi wa Taifa. Mwaka 2020 umemalizika kwa kazi iliyosubiriwa kwa hamu kubwa ya Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama. Kitabu kizuri Sana kuhusu Mweusi huyu wa kwanza kuwa Rais wa Taifa kubwa duniani.

Wasifu niliosoma Mwaka huu ni Pamoja na;

7. Julius Nyerere, A Biography: Saida Y Othman, Ng’wanza Kamata na Issa G Shivji

8. Maisha Yangu, Utumishi Wangu: Steven J Bwana

9. A promised Land: Barack Obama

Nilisoma pia Mchanganyiko wa vitabu mbalimbali kama kawaida. Ni katika kuongeza maarifa na kuendelea kujifunza kutoka sehemu mbalimbali za Dunia. Pia katika kujifunza makosa ya wengine ili kutorudia makossa hayo. Vitabu mchanganyiko mwaka huu ni pamoja na;

Vitabu Mchanganyiko

10. Asia aspirations, Why and How Africa Should Emulate Asia -- and What It Should Avoid: Greg Mills, O Obasanjo Et al

11. The Naked Diplomat, understanding Power and Politics in the Digital Age: Tom Fletcher

12. Taxing Africa, Coercion, Reforms and Development: Mick Moore, et al

13. Homo Deus, A brief history of tomorrow: Yuval Noah Harari

14. The Promise of Canada, People and Ideas that have shaped our country: Charlotte Gray

15. How to lose a Country, The Seven Steps from Democracy to Dictatorship: Ece Temelkuran

16. The Room Where it Happened, A White House Memoir: John Bolton

Mwaka 2020 ulikuwa mwaka wenye changamoto nyingi sana zitokanazo na janga la COVID 19 (Korona) mpaka Uchaguzi mbovu kabisa kupata kutokea katika historia ya Tanzania. Hakika hapakuwa na Uchaguzi kwa maana ya Uchaguzi bali operesheni Maalumu ya kusaga saga demokrasia ya Vyama vingi Nchini. Kwangu Binafsi namshukuru Mungu kwa kunisuru na ajali niliyopata Oktoba 7, 2020. Ilikuwa miujiza. Mungu mkubwa Sana.

Nawatakia kheri katika kumaliza mwaka 2020 na kila la kheri katika mwaka 2021. Nawashawishi kupata muda wa kujisomea japo kitabu kimoja kila mwezi. Kusoma ni kurutubisha ubongo. Tunaoweza kuandika pia tuandike.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Dar es Salaam
Disemba 26, 2020

View attachment 1659446View attachment 1659447View attachment 1659448View attachment 1659449View attachment 1659450View attachment 1659451View attachment 1659453View attachment 1659454View attachment 1659455View attachment 1659456
Hongera sana bro, umejitahidi kadiri ulivyoweza kujisomea. Ila kuna kitabu kimoja ambacho ni muhimu sana kuliko vyote nacho ni Qur'an umewahi kuisoma na kuielewa?
 
Huna lolote kwa sasa,umepoteza ushawishi mbele ya jamii kwa kukubali kutumiwa na ccm.
 
Wewe ni mnafiki mkubwa sana na mpigania tumbo lako
 
Mbona hivi vitabu vyote vimetungwa na mabeberu?? Halafu utaniambia vitakuwa na mtazamo mzuriii kwa Africa ?. Kwanii hamsomi vya watunzi wa kiafrica??
Mmepandikizwa ujinga, na mkaridhia kubeba ujinga! katika orodha ya vitabu alivyotuwekea Zitto kuwa amevisoma wewe umeona vya mabeberu tu? Pumbav.
 
Back
Top Bottom