Baadhi ya viongozi wa serikali ni 'vichaa', wakiondolewa ndipo Watanzania watapata ahueni

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,480
35,375
Habari za asubuhi!

Leo kuna mtu alipost jambo humu akanikumbusha jambo, nikaingia library kupekua nikakutana na picha za matukio kadhaa ya nyuma yaliyofanywa na viongozi wetu.

Hebu icheki hii picha chini kisha utagundua kuwa tuna baadhi ya viongozi vichaa katika Taifa hili.

Hawa watu wenye makazi duni kiasi hiki ni kipi kilistahili kutangulia kati ya kuboreshewa makazi yao au kuwekewa umeme?

Najua wapo watu watatetea kuwa serikali jukumu lake si kujenga makazi ya wananchi. Je, serikali haina jukumu la kuhakikisha ustawi wa wananchi?

Endapo wangeboresha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi wananchi hawa wasingeweza kuwa na makazi bora?

Serikali inajisikia fahari kusema wameweka umeme vijijini kwa asililimia nyingi?

Hawa ndio watakatwa 1000 kila mwezi kulipia majengo yao.

Serious?

FB_IMG_1622734978097.jpg


FB_IMG_1623187789249.jpg
 
Tunataka makusanyo ya sh 1000 kila mwezi toka kwenye luku ndiyo maana mita zinawekwa hata chini ya miti
 
Tunataka makusanyo ya sh 1000 ila mwezi toka kwenye luku ndiyo maana mita zinawekwa hata chini ya miti
Kwani hayo makusanyo si ni ya jengo? Hapo kuna jengo linalitambulika kisheria? Watakuwa wahuni tu
 
Mleta mada umetumia neno kali vichaa lakini ni la staha ingepaswa uwaite was**** ili hata kama tunaenda jela tuende kihalali
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom