Baadhi ya tweets muhimu sana za Mhe Bernard Membe wakati wa mchakato wa Katiba kuhusu uraia pacha

Kwa kweli Membe anawafaa sana Chadema kuwa mgombea wao wa urais 2020 na atashinda saa mbili ya asubuhi. Nawashauri wanachadema wenzangu tumsajiri Membe sasa hivi tusichelewe!! Hahahaha!
Membe for 2020.
 
Pesa ya korosho siyo pesa ya Serikali ni pesa ya Benki ya maendeleo ya Kilimo ndege zimenunuliwa na pesa ya serikali kupitia kwa Rais mwenyewe.Na alitoa tamko kuwa atanunua ndege.niambie sheria ya kumzuia Rais wa Tanzania kutumia pesa ya serikali kwenye maslahi ya Taifa.
Aisee, we jamaa umesoma mpaka la ngapi? Unaonekana hujui maana ya utawala wa sheria. Bunge liliidhinisha lini manunuzi ya ndege, kwenye bajeti ipi, au unafikiri kikao cha bajeti huwa ni kikao cha kahawa na kuchat, halafu sheria ya manunuzi ilifuatwa? Ulisikia tenda imetangazwa?. Kwenye uendeshaji wa serikali kuna checks and balances! Hazina sio mfuko wa rais, achukue hela muda anaotaka.
Halafu kuwa realistic basi! TADB ilianzishwa na serikali kwa mtaji wa kama 60 bil. kama sijasahau, na imeanzishwa miaka michache sana iliyopita. Kwa hali ya kawaida tu,hiyo benki inapata wapi 600 bil za kununulia korosho zote,kwa faida gani na ukwasi upi?
Hii nchi wajinga wanaongezeka kila siku.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
maelezo kuhusu 1.5 tr yalishatolewa na Naibu Waziri wa fedha Bungeni na kuhusu mikutano hakuna aliyezuiliwa kufanya mikutano baada ya uchaguzi.kinachoelezwa kuwa uchaguzi umekwisha kila Mbunge akafanye mikutano Jimboni kwake mpaka uchaguzi mwingine.Sasa wewe Sugu jimbo lako ni Mbeya mjini unakwenda kufanya mkutano Kigoma mjini kwa ajili ya nini? Tatizo la kila mtanzania ni kuishi kwa mazoea bila kufuata sheria zinasemaje.

Kuna muda wa uchaguzi na kuna wa kufanya kazi baada ya uchaguzi.
Bahati mbaya, katiba haisemi hivyo na kimsingi hakuna sheria inayoelekeza hivyo. Vyama vya siasa kazi yake ni siasa na ni haki ya wanasiasa na raia wote kufanya mikutano kokote wanapotaka ndani ya jamhuri. Katiba haisemi na haijawahi kusema, fulani na fulani wanapaswa kuitisha mikutano kwenye jimbo hili na lile tu. Sio sawa kutetea huu ushamba na upuuzi.
 
Tumemaliza uchaguzi kinachofuata baada ya uchaguzi ni kutekelza yale ambayo kila mmoja aliahidi kwenye ilani yake ya uchaguzi kwenye maeneo mahususi.Hiyo mikatono yako unayotaka kufanya kama vile bado tuna uchaguzi haitafanyika.Tunashindwa hata kuelewa sheria tunazozitunga wenyewe.kila kitu kina taratibu zake.Shughuli zote za vyama hakuna chama kimoja kilichozuiliwa kufanya shughuli zake.Na hilo ndilo tatizo la kuishi kwa mazoezi eti mwisho wa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine.Tafuta Katiba yako ya kufanya hayo na wal si hii ya sasa.Kila chama kinatakiwa kujua huu ni wakati wa kutekelza ahadi za uchaguzi haijalishi ni chama gani au wapi.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Taifa ni hii mipaka ya kikoloni au Taifa maana yake nini?

Taifa lako ni afrika, siyo hii mipaka aliyochora Carl Peters, David Livingstone na mikataba ya Helligoland iliyokufanya uone Malawi, Msumbiji , Uganda na Kenya kama siyo Mataifa yako, kumbe ni Mataifa yako na una haki nayo kwa sababu ni Afrika!
Akili za chibuku siwezi bishana nazo
 
Nilichojifunza ni kwamba, kuna watanzania wa aina 2 ambao ni wakali sana kwenye suala hili la uraia pacha.
1. Wale ambao walitamani kwenda ughaibuni lakini zali halikuwa lao.
2. Wale ambao wamewahi kwenda ughaibuni lakini wakalazimika kurudi bongo kinyume na utashi wao.

Hakuna mamlaka yoyote duniani inayoweza kumnyang'anya mtu uraia wake wa kuzaliwa bila ya kufanya dhulma. Huwezi (kihalali) kumpokonya mtu kitu ambacho siyo wewe uliyempa. Mtanzania wa kuzaliwa, hakupewa uraia na serikali ya jamuhuri ya muungano. Kwahiyo basi serikali haina mamlaka halali ya kumpokonya.

Mwezi February 2019 narudi bongo na dola zangu 1800, ma bata ntakula bila ya kula nafaka.
 
Ok amevunja sheria gani mpaka sasa....au unaongea kwa hisia tu na kufuata mitandao....tutajie sheria ambayo Dr Magufuli amevunja mpaka leo hii....
1. Kavuruga minada ya korosho nchini kwa kutumia miguvu mahala isipohitajika.
2. Kajenga uwanja wa ndege chato, bajeti haikupitishwa na bunge.
3. Kashasema hawatalipwa mpaka waonyeshe mashamba. Dhulma
4. na mengine mengi tuu .....
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Halafu chadema acheni unafiki. Huyu membe si ndiye mlimwita Abubakar Membe? au siyo nyie?

Hapa rais ajae ni mzee Mizengo Pinda tuu
 
1. Kavuruga minada ya korosho nchini kwa kutumia miguvu mahala isipohitajika.
2. Kajenga uwanja wa ndege chato, bajeti haikupitishwa na bunge.
3. Kashasema hawatalipwa mpaka waonyeshe mashamba. Dhulma
4. na mengine mengi tuu .....
Rais wa Tanzania anauwezo wa kutumia pesa ya nchi hii kwa matumizi yoyote bila kupitishwa na Bunge na ndiyo maana hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa na wanasheria wasomi au mawakili wasomi wa nchi hii.

Lengo la Serikali ni kumwezesha mkulima wa korosho na si mlanguzi wa korosho na kama wewe ni mlanguzi wa korosho uliyenunua korosho toka kwa wakulima kwa bei nafuu halafu unategemea korosho zako zinunuliwe na serikali hiyo imekula kwako

Sema lingine....hiyo ndiyo Tanzania hutaki hamia nchi nyingine.
 
Nilishahama tangu 1992.

Kwahuwa wafanyabiashara wa kati umewaita walanguzi, basi sina muda tena na wewe. Ni dhahili tunaamini katika falsafa tofauti. Mimi naamini katika enterprise and free market economy. Lakini kama kufanya biashara ni ulanguzi kwako, soon na bucha za nyama mtazifunga kwa hoja ya kwamba mmiliki wa butcher aonyeshe zizi lake la ng'ombe.
 
Pamoja na kuamini ktk enterprise and free market economy katika nzima ya biashara na masoko lakini kumbuka hapo serikali haifanyi biashara lakini ni kumkomboa mkulima wa korosho kwa mwaka 2018 kutokana na wadau wa korosho kumlalia mkulima halisi wa korosho na hiyo ndiyo dhima kubwa ya serikali
 
Upo sahihi kabisa..., serikali yetu tukufu mwaka huu imemkomboa mkulima wa korosho.:D
 
Nilichojifunza ni kwamba, kuna watanzania wa aina 2 ambao ni wakali sana kwenye suala hili la uraia pacha.
1. Wale ambao walitamani kwenda ughaibuni lakini zali halikuwa lao.
2. Wale ambao wamewahi kwenda ughaibuni lakini wakalazimika kurudi bongo kinyume na utashi wao.

Hakuna mamlaka yoyote duniani inayoweza kumnyang'anya mtu uraia wake wa kuzaliwa bila ya kufanya dhulma. Huwezi (kihalali) kumpokonya mtu kitu ambacho siyo wewe uliyempa. Mtanzania wa kuzaliwa, hakupewa uraia na serikali ya jamuhuri ya muungano. Kwahiyo basi serikali haina mamlaka halali ya kumpokonya.

Mwezi February 2019 narudi bongo na dola zangu 1800, ma bata ntakula bila ya kula nafaka.
Hizo $1800 zitaishia kulewea pale samaki samaki tu au unataka kununua bodaboda uanze kuendesha mkuu.
 
uraia pacha na uzalendo ni sawa na maji na mafuta haviambatani Abadan huwezi kujiita mzalendo wa nchi flani hali yakua una uraia na nchi zingine. kwa kuruhusu uraia pacha tutapoteza wazalendo ambao wapo tayari kufa kwaajili ya taifa.
 
wewe ndiyo uko tayari kufa kwaajili ya taifa?
 
Hizo $1800 zitaishia kulewea pale samaki samaki tu au unataka kununua bodaboda uanze kuendesha mkuu.

Mimi ni muumini wa ujasiliamali na soko huru. Hiyo dola 1800 naweza kuizungusha na mademu zenu wakaja kwangu.
 
Back
Top Bottom