Baadhi ya tweets muhimu sana za Mhe Bernard Membe wakati wa mchakato wa Katiba kuhusu uraia pacha

Membe amewashika kende, ofisini kwetu kila mtu amesema anamchinja JPM, ndugu najua ata wewe unajua kuwa Magufuli ameharibu mnoooView attachment 958637
Dr Magufuli hajaharibu kama unavyofikiria ila hii inaonyesha kabisa watanzania waliowengi wanaishi maisha yasiyokuwa na mfumo rasmi wa kuingiza income waliowengi walishazoea maisha yasiyofuata sheria na taratibu si wafanyakazi wala wafanyabiashara hata wasiokuwa na kazi rasmi wote wanapenda na wanaishi maisha ya kuvunja sheria.

Ukiamua sasa kila mmoja kufuata taratibu haya ndiyo matokeo yake kila mmoja atakuchukua na ndiyo hasira za kila mmoja juu ya maamuzi ya Dr Magufuli.
 
Huyu mtu anaonekana ana exposure ya kutosha anafaa kuwa rais wetu!

2020 twende na membe!
#KazinaBata
Msimuache huyo aisee atawafaa sana wana nzengo wa ufipa..jwanza pesa ya kampeni anayo ile ya ghadafi..anzeni tu kutengeneza tsheti za friends of membe.
 
Maelezo ya mtu hayatafsiriwi kwa kutafuta sentensi mojamoja na kuzipa maana.
Kiukweli CCM hakuna anayefaa lakini kuna wengine kama huyu BM ni nafuu mara 50 kuliko tuliye naye sasa.
Kwani sentensi moja si muendekezo wa maneno mengine..au kwake yeye kila sentensi moja huwa haitegemei zingine kwenye muendelezo..?ccm wanaofaa wengi sana..huko kwenu atawafaa sana membe..hakikisheni kila uchaguzi mnakamata kichwa kimoja toka ccm..
 
Msimuache huyo aisee atawafaa sana wana nzengo wa ufipa..jwanza pesa ya kampeni anayo ile ya ghadafi..anzeni tu kutengeneza tsheti za friends of membe.
kabisa kwa mlango wa ccm huyo hana nafasi kabisa nafasi yake iliishia 2015...mbeleni mlango ulishafungwa kwake asahau kabisa.
 
Acha tuitwe nyumbu tu mkuu,tunastahili kabisaa.

Kwa kitu gani cha msingi alichofanya Membe akiwa CCM miaka yake yoote akiwa kiongozi ambacho tumefaidika nacho wananchi wa kawaida?Sijui kwanini tunakua wepesi kusahau.

CCM endeleeni kutawala milele na milele,Amen

Kwangu mimi,2020 Tundu Lissu all the way.
Atleast kama unajitambua tambua..kuna watu tulikimbia chadema sababu ni chama ambacho wanachama wake wlikuwa wanapambana usiku na mchana hadi kufa ila misingi yake ikapinduliwa..tukajua tu hawa wwanaleta siasa za siasa wamefikia ukingoni
 
'Masuala kwenye rasimu ya Katiba yanayogusa Wizara ya Mambo ya Nje ni Muungano,Uraia,Sera ya Mambo ya Nje & suala la Ushirikiano wa Kimataifa'

'Jana niliwasilisha pendekezo kwa Tume ya Katiba kuomba suala la uraia pacha kuingizwa kwenye Katiba. Tume imetupokea vizuri sana'

'Tukiendelea kuwafutia uraia wa asili,tutazalisha watu wasio na uraia wowote iwapo nchi ya pili itawafutia uraia wao wa kujiandikisha'

'URAIA hauwezi kutuunganisha kama taifa, ispokuwa UTAIFA ndio unaweza kutuunganisha na kuwa na uzalendo kwa nchi yetu'

'Kuwaruhusu watanzania kupata uraia huko kutawapa fursa ya kujiendeleza na kustawi kiuchumi na kuwapa uwezo wa kuchangia maendeleo nchini'

' Katiba ilinde haki ya uraia, Sheria ya Uraia itafafanua vigezo na masharti kuhusu haki na wajibu wa Raia wa Tanzania mwenye uraia wa pili'

'Katiba itamke kuwa Raia wa kuzaliwa wa Tanzania hatapoteza uraia wake kwa kuwa tu amepata uraia mwingine'

'Hivyo, tunachosema kwenye uraia pacha ni, mtanzania asipoteze uraia wake wa asili kwa sababu yoyote ile ikiwemo kupata uraia mwingine nje'

'Hoja ya msingi kwenye uraia pacha ni, URAIA wa kuzaliwa ni Haki ya Msingi na Asili ambayo haitakiwi kuvuliwa na mamlaka yoyote ile'

'Ipo hoja ya Usalama, raia walio nje tunaowapa uraia hapa nchini wanaweza kuwa hatari kiusalama zaidi kuliko watanzania wenye uraia wa nje'

'Kama hofu yetu ni uzalendo, mizizi ya uzalendo wa mtu iko kwenye UTAIFA sio URAIA. Watanzania walio nje wana uzalendo mkubwa tu kwa nchi yao'

'Watanzania walio nje, pamoja na baadhi yao kuwa wamepoteza uraia wao, hawajapoteza utaifa. Bado ni watanzania kwa hulka,utamaduni na asili'

'Ili kuelewa mantiki ya uraia pacha, tunapaswa kwanza kuelewa tofauti ya utaifa (nationality) na uraia (citizenship)'

'Kilio cha Diaspora wetu kuhusu uraia pacha tumekikuta kila tulipowatembelea na kukutana nao. Wizara yetu ndio yenye wajibu wa kuwasemea'
Hizi ni fikra pevu kutoka kwa raia aliyepevuka. Zilistahili kuenziwa lkn, sio wote tuwezao kuiona mantiki yake. Werevu wanalijua hilo.
 
Dr Magufuli hajaharibu kama unavyofikiria ila hii inaonyesha kabisa watanzania waliowengi wanaishi maisha yasiyokuwa na mfumo rasmi wa kuingiza income waliowengi walishazoea maisha yasiyofuata sheria na taratibu si wafanyakazi wala wafanyabiashara hata wasiokuwa na kazi rasmi wote wanapenda na wanaishi maisha ya kuvunja sheria.

Ukiamua sasa kila mmoja kufuata taratibu haya ndiyo matokeo yake kila mmoja atakuchukua na ndiyo hasira za kila mmoja juu ya maamuzi ya Dr Magufuli.
Yeye anaishi kwa kufuatisha sheria? Au Raia wako chini ya Sheria yeye yuko juu ya Sheria? Angefuatisha sheria yeye ili awe na haki ya kuwahukumu wengine wasiofuatisha sheria. Ila Yeye ndo namba moja wa kuvunja sheria halafu anataka wengine wafuatishe, yeye ni nani? Anakula moto? Au damu yake imechanganyikana na petrol ikisukumwa na moyo wenye turbo?
 
  • Thanks
Reactions: Pep
G
Membe aliongea pointi zenye nguvu sana, nakumbuka hata Kiwete alimuelewa na wakati Bunge linataka kupitisha sheria ya uraia pacha, ndipo ikapendekezwa wasifanye hivyo bali waliingize jambo hilo kwenye Katiba mpya. Hilo lilikuwa kosa kubwa sana. Sasa tuna Magufuli na genge lake la Yes Men. Yaani hapo watu kama Raisi Magufuli hawaelewi kabisa. Wanachojua ni kutumia nguvu nyingi kupinga uraia pacha badala ya hekima
hahahaaa Genge la "Yes Men"
 
Yeye anaishi kwa kufuatisha sheria? Au Raia wako chini ya Sheria yeye yuko juu ya Sheria? Angefuatisha sheria yeye ili awe na haki ya kuwahukumu wengine wasiofuatisha sheria. Ila Yeye ndo namba moja wa kuvunja sheria halafu anataka wengine wafuatishe, yeye ni nani? Anakula moto? Au damu yake imechanganyikana na petrol ikisukumwa na moyo wenye turbo?
Ok amevunja sheria gani mpaka sasa....au unaongea kwa hisia tu na kufuata mitandao....tutajie sheria ambayo Dr Magufuli amevunja mpaka leo hii....
 
Kwa kweli Membe anawafaa sana Chadema kuwa mgombea wao wa urais 2020 na atashinda saa mbili ya asubuhi. Nawashauri wanachadema wenzangu tumsajiri Membe sasa hivi tusichelewe!! Hahahaha!
Jikite kwenye hoja za membe, hayo ya kusema anafaa kugombea kwa tiketi ya chadema mtayajadili kwenye vikao vyenu vya uvccm
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom