Baadhi ya tweets muhimu sana za Mhe Bernard Membe wakati wa mchakato wa Katiba kuhusu uraia pacha

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
'Masuala kwenye rasimu ya Katiba yanayogusa Wizara ya Mambo ya Nje ni Muungano,Uraia,Sera ya Mambo ya Nje & suala la Ushirikiano wa Kimataifa'

'Jana niliwasilisha pendekezo kwa Tume ya Katiba kuomba suala la uraia pacha kuingizwa kwenye Katiba. Tume imetupokea vizuri sana'

'Tukiendelea kuwafutia uraia wa asili,tutazalisha watu wasio na uraia wowote iwapo nchi ya pili itawafutia uraia wao wa kujiandikisha'

'URAIA hauwezi kutuunganisha kama taifa, ispokuwa UTAIFA ndio unaweza kutuunganisha na kuwa na uzalendo kwa nchi yetu'

'Kuwaruhusu watanzania kupata uraia huko kutawapa fursa ya kujiendeleza na kustawi kiuchumi na kuwapa uwezo wa kuchangia maendeleo nchini'

' Katiba ilinde haki ya uraia, Sheria ya Uraia itafafanua vigezo na masharti kuhusu haki na wajibu wa Raia wa Tanzania mwenye uraia wa pili'

'Katiba itamke kuwa Raia wa kuzaliwa wa Tanzania hatapoteza uraia wake kwa kuwa tu amepata uraia mwingine'

'Hivyo, tunachosema kwenye uraia pacha ni, mtanzania asipoteze uraia wake wa asili kwa sababu yoyote ile ikiwemo kupata uraia mwingine nje'

'Hoja ya msingi kwenye uraia pacha ni, URAIA wa kuzaliwa ni Haki ya Msingi na Asili ambayo haitakiwi kuvuliwa na mamlaka yoyote ile'

'Ipo hoja ya Usalama, raia walio nje tunaowapa uraia hapa nchini wanaweza kuwa hatari kiusalama zaidi kuliko watanzania wenye uraia wa nje'

'Kama hofu yetu ni uzalendo, mizizi ya uzalendo wa mtu iko kwenye UTAIFA sio URAIA. Watanzania walio nje wana uzalendo mkubwa tu kwa nchi yao'

'Watanzania walio nje, pamoja na baadhi yao kuwa wamepoteza uraia wao, hawajapoteza utaifa. Bado ni watanzania kwa hulka,utamaduni na asili'

'Ili kuelewa mantiki ya uraia pacha, tunapaswa kwanza kuelewa tofauti ya utaifa (nationality) na uraia (citizenship)'

'Kilio cha Diaspora wetu kuhusu uraia pacha tumekikuta kila tulipowatembelea na kukutana nao. Wizara yetu ndio yenye wajibu wa kuwasemea'
 
Kwa kweli Membe anawafaa sana Chadema kuwa mgombea wao wa urais 2020 na atashinda saa mbili ya asubuhi. Nawashauri wanachadema wenzangu tumsajiri Membe sasa hivi tusichelewe!! Hahahaha!
 
Membe aliongea pointi zenye nguvu sana, nakumbuka hata Kiwete alimuelewa na wakati Bunge linataka kupitisha sheria ya uraia pacha, ndipo ikapendekezwa wasifanye hivyo bali waliingize jambo hilo kwenye Katiba mpya. Hilo lilikuwa kosa kubwa sana. Sasa tuna Magufuli na genge lake la Yes Men. Yaani hapo watu kama Raisi Magufuli hawaelewi kabisa. Wanachojua ni kutumia nguvu nyingi kupinga uraia pacha badala ya hekima
 
Jamaa huwa anafikiri kwanza kabla ya kuandika/kuongea kitu.
Hivi aliposema

1.Akipata urais maadui zake watatu watakimbilia Kenya alimaanisha nini mkuu.

2.Magu alivyoingia akapiga marufuku safari za nje yeye akawa wa 1 kuunga mkono akisema'eti tulikua tunapishana angani kama vile nyumba imeungua nyumbani'.-
Alimaanisha nini hapo wkt yeye alikua mnufaika wa safari no. 2 baada ya JK.
 
Back
Top Bottom