Baadhi ya tweets muhimu sana za Mhe Bernard Membe wakati wa mchakato wa Katiba kuhusu uraia pacha

Anaonyesha uwezo kupambanua mambo ktk mtazamo mkubwa, mtu mwenye narrow mind kama JIWE akiulizwa msimamo wake juu ya uraia pacha, angeropoka "hao wameishatusaliti"
Anefanya kazi ikulu ya kuchambua taarifa za kiitelejensia tangu 1978
 
Kwa kweli Membe anawafaa sana Chadema kuwa mgombea wao wa urais 2020 na atashinda saa mbili ya asubuhi. Nawashauri wanachadema wenzangu tumsajiri Membe sasa hivi tusichelewe!! Hahahaha!
Huu ushauri sijaupenda, CCM hata aseme vp atabaki tuu kuwa CCM na asili yake ile ile.
 
'Masuala kwenye rasimu ya Katiba yanayogusa Wizara ya Mambo ya Nje ni Muungano,Uraia,Sera ya Mambo ya Nje & suala la Ushirikiano wa Kimataifa'

'Jana niliwasilisha pendekezo kwa Tume ya Katiba kuomba suala la uraia pacha kuingizwa kwenye Katiba. Tume imetupokea vizuri sana'

'Tukiendelea kuwafutia uraia wa asili,tutazalisha watu wasio na uraia wowote iwapo nchi ya pili itawafutia uraia wao wa kujiandikisha'

'URAIA hauwezi kutuunganisha kama taifa, ispokuwa UTAIFA ndio unaweza kutuunganisha na kuwa na uzalendo kwa nchi yetu'

'Kuwaruhusu watanzania kupata uraia huko kutawapa fursa ya kujiendeleza na kustawi kiuchumi na kuwapa uwezo wa kuchangia maendeleo nchini'

' Katiba ilinde haki ya uraia, Sheria ya Uraia itafafanua vigezo na masharti kuhusu haki na wajibu wa Raia wa Tanzania mwenye uraia wa pili'

'Katiba itamke kuwa Raia wa kuzaliwa wa Tanzania hatapoteza uraia wake kwa kuwa tu amepata uraia mwingine'

'Hivyo, tunachosema kwenye uraia pacha ni, mtanzania asipoteze uraia wake wa asili kwa sababu yoyote ile ikiwemo kupata uraia mwingine nje'

'Hoja ya msingi kwenye uraia pacha ni, URAIA wa kuzaliwa ni Haki ya Msingi na Asili ambayo haitakiwi kuvuliwa na mamlaka yoyote ile'

'Ipo hoja ya Usalama, raia walio nje tunaowapa uraia hapa nchini wanaweza kuwa hatari kiusalama zaidi kuliko watanzania wenye uraia wa nje'

'Kama hofu yetu ni uzalendo, mizizi ya uzalendo wa mtu iko kwenye UTAIFA sio URAIA. Watanzania walio nje wana uzalendo mkubwa tu kwa nchi yao'

'Watanzania walio nje, pamoja na baadhi yao kuwa wamepoteza uraia wao, hawajapoteza utaifa. Bado ni watanzania kwa hulka,utamaduni na asili'

'Ili kuelewa mantiki ya uraia pacha, tunapaswa kwanza kuelewa tofauti ya utaifa (nationality) na uraia (citizenship)'

'Kilio cha Diaspora wetu kuhusu uraia pacha tumekikuta kila tulipowatembelea na kukutana nao. Wizara yetu ndio yenye wajibu wa kuwasemea'
Nonsense! Rubbish! Mie nimezaliwa Vudee Same, haematite kama niko Argentina au Stockholm, mimi ni Mzigua. UTANZANIA wangu ubatokana ba kuwa mzaliwaxwa Vudee. Usiniambie upuuzi wa REMITTANCES kwa vile ,ingawa baba yangu ba shangazi wamefariki, ndugu zangu wote wapi na nitawapa hela wakati wa njaa whether or not ni raia wa Tanzania au wa Wisconsin. Leo mie ni mkufunzi Chuo Kikuu cha Wisconsin, USA, Uzigua gautapitea kama, ila naweza tu kuupoteza Utanzania wangu kama nitaamua kuupoteza kwa kuka kuapo kama hiki hapa:

.....I, Mwanamkasi Ali Mngodo, hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America .....

Yaani hapa SSH nimemwita POTENTATE, sijui atajisikiaje Maskini. Halafu kweeli kwel8 anipe Passport yake nitembee bayo nikiinajisi?
 
Back
Top Bottom