Baadhi ya tweets muhimu sana za Mhe Bernard Membe wakati wa mchakato wa Katiba kuhusu uraia pacha

Anaonyesha uwezo kupambanua mambo ktk mtazamo mkubwa, mtu mwenye narrow mind kama JIWE akiulizwa msimamo wake juu ya uraia pacha, angeropoka "hao wameishatusaliti"
Sasa mtu ambaye hata hajui tofauti ya Libya, Kuwait na Iraq kwa location atajuaje hayo mengine? ukweli mzee baba ufahamu wake nje ya kukariri ni mfinyu sana na unatia ukakasi. Na yaweza kuwa ndio sababu kubwa ya kugomea kwenda nje.
Kuna siku atatoka pale na wenzake hawataogopa kutupa siri za mtungi
 
Hivi aliposema

1.Akipata urais maadui zake watatu watakimbilia Kenya alimaanisha nini mkuu.

2.Magu alivyoingia akapiga marufuku safari za nje yeye akawa wa 1 kuunga mkono akisema'eti tulikua tunapishana angani kama vile nyumba imeungua nyumbani'.-
Alimaanisha nini hapo wkt yeye alikua mnufaika wa safari no. 2 baada ya JK.
Maelezo ya mtu hayatafsiriwi kwa kutafuta sentensi mojamoja na kuzipa maana.
Kiukweli CCM hakuna anayefaa lakini kuna wengine kama huyu BM ni nafuu mara 50 kuliko tuliye naye sasa.
 
Acha tuitwe nyumbu tu mkuu,tunastahili kabisaa.

Kwa kitu gani cha msingi alichofanya Membe akiwa CCM miaka yake yoote akiwa kiongozi ambacho tumefaidika nacho wananchi wa kawaida?Sijui kwanini tunakua wepesi kusahau.

CCM endeleeni kutawala milele na milele,Amen

Kwangu mimi,2020 Tundu Lissu all the way.
 
Anaonyesha uwezo kupambanua mambo ktk mtazamo mkubwa, mtu mwenye narrow mind kama JIWE akiulizwa msimamo wake juu ya uraia pacha, angeropoka "hao wameishatusaliti"
Wala hatuwahitaji waendezao tu hao!
 
Hivi aliposema

1.Akipata urais maadui zake watatu watakimbilia Kenya alimaanisha nini mkuu.

2.Magu alivyoingia akapiga marufuku safari za nje yeye akawa wa 1 kuunga mkono akisema'eti tulikua tunapishana angani kama vile nyumba imeungua nyumbani'.-
Alimaanisha nini hapo wkt yeye alikua mnufaika wa safari no. 2 baada ya JK.
Wala hatuwahitaji waendezao tu hao!
wivu
 
'Masuala kwenye rasimu ya Katiba yanayogusa Wizara ya Mambo ya Nje ni Muungano,Uraia,Sera ya Mambo ya Nje & suala la Ushirikiano wa Kimataifa'

'Jana niliwasilisha pendekezo kwa Tume ya Katiba kuomba suala la uraia pacha kuingizwa kwenye Katiba. Tume imetupokea vizuri sana'

'Tukiendelea kuwafutia uraia wa asili,tutazalisha watu wasio na uraia wowote iwapo nchi ya pili itawafutia uraia wao wa kujiandikisha'

'URAIA hauwezi kutuunganisha kama taifa, ispokuwa UTAIFA ndio unaweza kutuunganisha na kuwa na uzalendo kwa nchi yetu'

'Kuwaruhusu watanzania kupata uraia huko kutawapa fursa ya kujiendeleza na kustawi kiuchumi na kuwapa uwezo wa kuchangia maendeleo nchini'

' Katiba ilinde haki ya uraia, Sheria ya Uraia itafafanua vigezo na masharti kuhusu haki na wajibu wa Raia wa Tanzania mwenye uraia wa pili'

'Katiba itamke kuwa Raia wa kuzaliwa wa Tanzania hatapoteza uraia wake kwa kuwa tu amepata uraia mwingine'

'Hivyo, tunachosema kwenye uraia pacha ni, mtanzania asipoteze uraia wake wa asili kwa sababu yoyote ile ikiwemo kupata uraia mwingine nje'

'Hoja ya msingi kwenye uraia pacha ni, URAIA wa kuzaliwa ni Haki ya Msingi na Asili ambayo haitakiwi kuvuliwa na mamlaka yoyote ile'

'Ipo hoja ya Usalama, raia walio nje tunaowapa uraia hapa nchini wanaweza kuwa hatari kiusalama zaidi kuliko watanzania wenye uraia wa nje'

'Kama hofu yetu ni uzalendo, mizizi ya uzalendo wa mtu iko kwenye UTAIFA sio URAIA. Watanzania walio nje wana uzalendo mkubwa tu kwa nchi yao'

'Watanzania walio nje, pamoja na baadhi yao kuwa wamepoteza uraia wao, hawajapoteza utaifa. Bado ni watanzania kwa hulka,utamaduni na asili'

'Ili kuelewa mantiki ya uraia pacha, tunapaswa kwanza kuelewa tofauti ya utaifa (nationality) na uraia (citizenship)'

'Kilio cha Diaspora wetu kuhusu uraia pacha tumekikuta kila tulipowatembelea na kukutana nao. Wizara yetu ndio yenye wajibu wa kuwasemea'
Naona uraia pacha tu hamba kingine cha muhimu ktk katiba mpya? Ana lake jambo na uraia pacha.
 
An exposure..., kitu ambacho viongozi wengi na watanzania kwa ujumla tumekosa.
 
'Ipo hoja ya Usalama, raia walio nje tunaowapa uraia hapa nchini wanaweza kuwa hatari kiusalama zaidi kuliko watanzania wenye uraia wa nje'
Hapa napata shida sana...! Kama raia kwa kuzaliwa anaweza ku'chukua' ela zilizotengwa kwa ajiri ya miradi ya maendeleo kwa watanzania na kwenda kuzificha nje ya nchi kwa manufaa yake...je huyu akiwa na uhakika wa kutobugudhiwa kwa kuwa na uraia wa nchi mbili si ndo ataenda kuwaleta maharamia waje wapore kila kitu...! .Hii ni scenario mojawapo mimi mshamba wa mambo haya ninayoona inaweza kuleta wasiwasi. Naweza kuwa nimewaza hisivyo kabisa.
 
2020 Membe anatosha
Screenshot_20181206-181524.png
 
Kwani sababu za kumtosa Membe kipindi kile kugombea ilikua nini jamani?? Isije kua kuna kashfa zake hatuzijui.

Tuliambiwa anaitwa Bakari Membe Na ni Mtoto wa kambO wa Mzee Mrisho wa Msoga
So tusiruhusu Nchi yetu Kwa Taifa la Kifalme

Waliosimamia kucha kumkataa Membe ndio wanasimamia kucha sasa kutaka awe Rais

Magufuli, John Joseph anatosha
 
'Masuala kwenye rasimu ya Katiba yanayogusa Wizara ya Mambo ya Nje ni Muungano,Uraia,Sera ya Mambo ya Nje & suala la Ushirikiano wa Kimataifa'

'Jana niliwasilisha pendekezo kwa Tume ya Katiba kuomba suala la uraia pacha kuingizwa kwenye Katiba. Tume imetupokea vizuri sana'

'Tukiendelea kuwafutia uraia wa asili,tutazalisha watu wasio na uraia wowote iwapo nchi ya pili itawafutia uraia wao wa kujiandikisha'

'URAIA hauwezi kutuunganisha kama taifa, ispokuwa UTAIFA ndio unaweza kutuunganisha na kuwa na uzalendo kwa nchi yetu'

'Kuwaruhusu watanzania kupata uraia huko kutawapa fursa ya kujiendeleza na kustawi kiuchumi na kuwapa uwezo wa kuchangia maendeleo nchini'

' Katiba ilinde haki ya uraia, Sheria ya Uraia itafafanua vigezo na masharti kuhusu haki na wajibu wa Raia wa Tanzania mwenye uraia wa pili'

'Katiba itamke kuwa Raia wa kuzaliwa wa Tanzania hatapoteza uraia wake kwa kuwa tu amepata uraia mwingine'

'Hivyo, tunachosema kwenye uraia pacha ni, mtanzania asipoteze uraia wake wa asili kwa sababu yoyote ile ikiwemo kupata uraia mwingine nje'

'Hoja ya msingi kwenye uraia pacha ni, URAIA wa kuzaliwa ni Haki ya Msingi na Asili ambayo haitakiwi kuvuliwa na mamlaka yoyote ile'

'Ipo hoja ya Usalama, raia walio nje tunaowapa uraia hapa nchini wanaweza kuwa hatari kiusalama zaidi kuliko watanzania wenye uraia wa nje'

'Kama hofu yetu ni uzalendo, mizizi ya uzalendo wa mtu iko kwenye UTAIFA sio URAIA. Watanzania walio nje wana uzalendo mkubwa tu kwa nchi yao'

'Watanzania walio nje, pamoja na baadhi yao kuwa wamepoteza uraia wao, hawajapoteza utaifa. Bado ni watanzania kwa hulka,utamaduni na asili'

'Ili kuelewa mantiki ya uraia pacha, tunapaswa kwanza kuelewa tofauti ya utaifa (nationality) na uraia (citizenship)'

'Kilio cha Diaspora wetu kuhusu uraia pacha tumekikuta kila tulipowatembelea na kukutana nao. Wizara yetu ndio yenye wajibu wa kuwasemea'
Kwani Benard Membe ndii Nani?
 
Back
Top Bottom