Baadhi ya tweet za Rais Dkt. Magufuli leo twitter katika siku ya kumbukizi ya kifo ya Sokoine

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Rais Dkt Magufuli Atoa Neno Katika Siku Ya Leo Ambapo ni kumbukumbu ya kifo cha aliekuwa waziri mkuu sokoine
IMG_20180412_105137_074.jpg
IMG_20180412_105137_077.jpg
IMG_20180412_105137_075.jpg
 
Tweet ya tukio la namna hii linalomhusu aliyekua kiongozi wa kitaifa inakuaje rais anatajataja tu jina la marehem bila kutaja wadhifa aliokua akiutumikia, ....??

Ukiwa na mindset ambayo ni "village based" unaona kama kila mtu duniani hapa ni mwananzengo tu ndo maana mambo makubwa yanazungumzwa na mtu mkubwa but unfortunately in a very local design
 
Bila kusau kuyaenzi yale yote mema aliyoshiriki kuyaanzisha na viongozi wenzake wa nyakati hizo. Nakumbuka kulikuwa na nyumba za watumishi wa umma, ajira za kumwaga, elimu haina mwisho kwa kila mwenye nia bila kujali hali yake ya maisha, elimu bure kwa wote hadi vyuo vikuu, n.k.
 
Rais Dkt Magufuli Atoa Neno Katika Siku Ya Leo Ambapo ni kumbukumbu ya kifo cha aliekuwa waziri mkuu sokoine

Ndugu Raisi, comment zangu ni hizi;

marehem = marehemu
Oparesheni Nguvukazi = Operation Nguvu Kazi
watanzania = Watanzania

Na mwisho, kusema ukweli na kumuenzi Sokoine kwa kujenga umoja wetu basi na tuanze kwa kuishi na watu wa vyama vya upinzani kwa kuwaona kuwa ni ndugu zetu wenye nia njema kwa taifa letu kama sisi. Sidhani kama Sokoine angekuwa anawafunga na kunyanyasa wapinzania kama unavyoruhusu au kuagiza wewe.
 
Tweet ya tukio la namna hii linalomhusu aliyekua kiongozi wa kitaifa inakuaje rais anatajataja tu jina la marehem bila kutaja wadhifa aliokua akiutumikia, ....??

Ukiwa na mindset ambayo ni "village based" unaona kama kila mtu duniani hapa ni mwananzengo tu ndo maana mambo makubwa yanazungumzwa na mtu mkubwa but unfortunately in a very local design
Haina shida hilo mkuu ,kwani wewe hujui mpaka leo alikuwa nani sokoine????
 
Mheshimiwa Rais wangu mpendwa, wakati tukikumbuka na sio kuadhimisha, tupinge ufisadi kwa vitendo kwa kuacha kununua wabunge na madiwani wa upinzani na tuboreshe zahanati zetu, tutoe pembejeo kwa wakulima na kusambaza maji kwa watu wetu nk
 
Tweet ya tukio la namna hii linalomhusu aliyekua kiongozi wa kitaifa inakuaje rais anatajataja tu jina la marehem bila kutaja wadhifa aliokua akiutumikia, ....??

Ukiwa na mindset ambayo ni "village based" unaona kama kila mtu duniani hapa ni mwananzengo tu ndo maana mambo makubwa yanazungumzwa na mtu mkubwa but unfortunately in a very local design

John Pombe Magufuli ni Rais wa ajabu...!!
Rais hajui Kiingereza wala hawezi kujieleza kwa Kiswahili FASAHA si kwa KUANDIKA wala KUZUNGUMZA...!!!Sentensi zimeandkwa kwa kuungaunga kwa Kiswahili cha Kisukuma..(KISWAKISU)....!
Halafu anajiita Dokta na kutamba huku wenzake akiwaona ni vilaza....Phew!
 
Back
Top Bottom