Baadhi ya taratibu na sheru za uendeshaji wa vicoba huwa nashindwa kabisa kuzielewa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,986
Kwa tafsi rahisi naweza kusema Vicoba ni vikundi vya watu/wajasiriamali kwa madhumuni ya kuweka akiba na kukopeshana na pia kugawana faida/gawio.

Hata hivyo,hili la kugawana faidi kwangu mimi naliona si jambo sahihi sana pale vikundi hivi vinapokuwa bado ni vichanga kwa maana ya uwezo wa kukopeshana kulingana na mahitaji.

Kwa mfano,wanasema kila baada ya mwaka mmoja,kikoba kinapaswa kuvunjwa na watu kugawana faida iliyopatikana kama ambavyo mabenki hutoa gawio kwa wana hisa wake.

Hapa kinachonishangaza watu kuwa tayari kuvunja na kugawana faida kila mwaka wakati vikundi hivi baadhi haviwezi hata kukopeshana kulingana na mahitaji ambapo wakti mwingine watu hulazimika kupewa mikopo kwa zamu kutokana na mahitaji kuzidi makusanyo ya vikao husika.

Sasa hap ndio huwa najiuliza katika hali hii watu waridhikaje kuvunja hivi vikoba kisa tu ni mwaka umetimia?

Kwanini wasifikirie kuongeza hisa/akiba wanazotoa kwa kila kikao na badala yake wanawaza tu kuvunja?

Kama ni kugawana faida,kwanini isiwe ni hatu ya baadae baada ya kikoba kuwa na mtaji wa kutosha kiasi kwamba wakati mwingine hela zinabaki nyingi tu baada ya wanakikundi kukopa?

Jambo au taratibu zingine za kushangaza ni zile za kuweka ukomo wa kutoa hisa/akiba kwenye kila kikao.

Kwa mfano,kuna vikoba vingine huweka kiwango cha juu(maximumu) ambachi katika kikao kimoja,mtu hutaruhusiwa kuweka zaidi ya kiasi kilichowekwa ili kuongeza akiba/hisa zako katika chama/kikundi.

Na utaratubu wa baadhi ya vikoba kuruhusu watu kukopa au kuweka hela siku ya vikao tu nao ni sahihi?

Kwanini wanakikundi wasiwe huru kuweka na kukopa wakati wowote kama hela ipo mradi tu kuna kuwa na records nzuri zinazowesha kujua nani kaweka kiasi gani leo na nani amekopa kiasi gani siku fulani,n.k?

Vikundi vingine zikiwemo Saccos,haviruhusu mtu kuchukua mkopo mpaka ule wa mwanzo uishe hata kama mtu amebakiza rejesho moja au mawili eti shariti ni mpaka amalize deni lote.

Kwangu mimi,utaratibu huu una maana tu pale kikundi kinapokuwa na mtaji mdogo ambapo inategemea wenye mikopo walipe na wengine waweze kukopeshwa ila si utaratibu sahihi kwa kikundi ambachon teyari kina mtaji mkubwa na fedha nyingi inabaki badala ya kukopeshwa kwa wanachama kisa tu taratibu haziruhusu hata kama utaratibu unazuia watu kukopa.

Sometimes huwa nahisi huenda watu wa mabenki na taasisi zingine za kifedha labda ndio zilizo nyuma ya baadhi ya taratibu/sheria hizi ambazo zinadumaza vikoba kwani vikoba ni tishio kwa kwa taasisi hizi zinazotoa mikopo kwa riba kubwa tofauti na hivi vikoba.

Naomba mawazo yenu juu ya mambo haya hasa kwa wataalamu wa mambo ya biashara,fedha au banking,n.k kwa lengo la kuboresha kwani penye watu wegi,hapaaribiki neno.

Naandikia nikiwa katika mkoa mmoja wa kaskazini mwa nchi hii.
 
Tatizo sio vikoba tatizo ni namna tunavyo tafsiri juu ya vikoba

Vikoba ni moja ya njia ya kuinuana kiuchumi lakini wengi wanao jikuta wako katika hivi vikoba hujikuta katika matatizo ya kiuchumi kuliko ilivyo kuwa kabla hajajiunga na hicho kikoba

Kwanza wengi huingia huko bila lengo maalum na mawazo chanya ya kuinua uchumi

Mwingne huingia huko kwa lengo la kuficha hela yake isitumike ovyo ili imsaidie mwisho wa mwaka sasa unapo anza kumwambia habari za kuongeza mtaji mwisho wa mwaka anahisi unataka kumtapeli hela yake haipo hapo

Unakutana na mwingne anaingia hapo kwenye kikoba kwa lengo la kufanya kama sehemu ya kuhamishia madeni kutoka katika kikoba kingne na hawa hutegemea wakati wa kuvunja kikoba ndio wakate hela huko huko ili asiwe na madeni kwenye kikoba

Ila kufikia lengo sahihi la kikoba mnapaswa kuungana watu wenye malengo yanayo fanana kidogo yaani wote mko Tayari kukuza uchumi hapo kikoba hata ukisema tusivunje mtu atakwambia haina shina hapo mnafanya kama vile mmevunja lakini kila kitu kinabaki kama zamani

Ila kuwapa watu wa hivyo ni ngumu sana
 
Mimi ninacho ambacho hakitavunjwa. Tuna mpango wa kuanzisha biashara za pamoja kuanzia mwaka huu mwishoni ili kujiongezea kipato.

Pia tunakopeshana wenyewe kwa riba ndogo saaaaana
 
Mimi ninacho ambacho hakitavunjwa. Tuna mpango wa kuanzisha biashara za pamoja kuanzia mwaka huu mwishoni ili kujiongezea kipato.

Pia tunakopeshana wenyewe kwa riba ndogo saaaaana
Kiasi gani hiyo ndogo sana mkuu?
 
Afadhali Leo umeleta mada isiyohusu siasa lakini bado hujaacha kasumba ya kulaumu pale uliposema unahisi taasisi za kifedha zipo nyuma ya hicho unachosema kuhusu kuvunja kikundi mwishoni mwa mwaka.
Kwanza sidhani kama kuna sheria iliyopitishwa na Bunge kuhusu vikoba ila ni utaratibu tu ambao kila kikundi unajiwekea.
Hakuna uniform formula Bali nyie mliopo mnaamua muendesheje kikundi chenu
 
vicoba havina formula , ni kama vile CHADEMA inavyoendeshwa bila mipango wala dira inaendeshwa kwa fikra za Mbowe
 
Mimi ninacho ambacho hakitavunjwa. Tuna mpango wa kuanzisha biashara za pamoja kuanzia mwaka huu mwishoni ili kujiongezea kipato.

Pia tunakopeshana wenyewe kwa riba ndogo saaaaana
Bado kipo?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom