Baadhi ya taarifa za BBC zinakera. Huenda ni mkakari mbaya wa waingereza

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,352
7,114
Kwa wale wenye mazoea kusikiliza bbc kiswahili utagundua pamoja na taarifa sahihi ziko taarifa nyingine ni kwa malengo maalum.
Kuna upendeleo dhidi kwa namna mambo ya kisiasa na kitamaduni wa nchi zinazoandamwa na uingereza na nchi za magharibi kwa ujumla. Pia mara nyingi zipo taarifa hazina maana au za kupotosha au kuhimiza maadili yasiyofaa kwa desturi za binadamu.
BBC huwezi kuwasikiliza bila kusikia mambo ya ushoga au ndoa za jinsia moja au mahusiana ya mapenzi yasiyokua na maadili wakizungumzia kama kitu cha kawaida.
Leo wametuletea habari ya mtu rwanda mwenye kaburi kuzika mbwa. Eti mtu huyo mwenye kaburi anaweka msalaba kaburi la mbwa, jambo la maudhi kwa mkristo.
Hebu watayarishaji vipindi watambue wasikilizaji wa kiswahili ni waafrika wana mila na desturi zao. Bila shaka wana maelekezo ya waajiri wao wenye malengo yao lakini wajitahidi maana wengi hua siku hizi hatuwasikikizi tena.
 
Hilo nililiona kitambo sana.
BBC huwa wanatangaza kile wanachotaka dunia isikie na sio kile dunia inatakiwa kusikia.
 
BBC au British broadcasting corporation ilianzishwa oktoba 1922 ilikueneza propaganda ya watawala wa uingereza.
BBC inachuki binafsi na mataifa yoteyenye sera zinazokinzana na siasa za uk. Mfano, Iran, Urusi, Afghanistan, Argentina, Rwanda etc.
Habari zao zina upendeleo.
Ni shirika la umma linaloendeshwa kwa Kodi za wananchi wa uingereza.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom