Baadhi ya solutions za matatizo ya automatic gearboxes

Watu wengi wanaobadilishia ATF kwenye magereji wanabadilisha between 9,000km to 15,000km.

Yaani ATF inatoka bado mpyaaaa. Huko ni kuchezea hela.
Na kuharibu gearbox tu hawajui kwamba kuna particles mle ndani hazitaki kumwagwa mwaga kila mda na pia hata wanapimwaga ukiwauliza kama wanaweka atf protector kabla ya kuweka atf nyingine jibu watakwambia hapana
 
Mkuu ukija Dar fanya mpango uonane na wadau, kuna mambo mengi ya kufanya haswa hapo kwenye Automatic gearbox, mimi ni mhanga mafundi wameshaniulia gearbox moja.

Alhamisi au ijumaa ijayo ntakuja Dar mkuu. Na nitakuwepo kwa siku kadhaa. Nna sehemu nyingi za kwenda. Mfano kama j3 naenda mbeya.
 
Mtaalam gari ya automatic kukosa nguvu wakati wa kupanda mlima, shida ni nini?

Mkuu gari kukosa nguvu zipo sababu nyingi sana. Inaweza kuwa sababu za engine kama(spark plug, coil on plug, spark plug wires, fuel pump, fuel pressure regulator, baadhi ya sensors n.k.

ia shida inaweza kuwa kwenye gearbox kama(kuslip kwa torque converter, kuharibika kwa frontal oil pump, kuisha kwa baadhi ya clutches n.k. Ninaweza kukupimia.

Upo mkoa gani mkuu?
 
Mkuu gari kukosa nguvu zipo sababu nyingi sana. Inaweza kuwa sababu za engine kama(spark plug, coil on plug, spark plug wires, fuel pump, fuel pressure regulator, baadhi ya sensors n.k. Pia shida inaweza kuwa kwenye gearbox kama(kuslip kwa torque converter, kuharibika kwa frontal oil pump, kuisha kwa baadhi ya clutches n.k. Ninaweza kukupimia.

Upo mkoa gani mkuu?
Pamoja
 
Kuna tofauti kubwa kati ya manual gearbox na automatic gearbox.

Katika Manual gearbox fluid iliyomo mule ndani ina kazi moja kubwa ambayo ni Lubrication na ndio maana wanatumia Oil ya kawaida...
Wewe una ujuzi kuliko waliotengeneza hiyo gearbox? Wewe unadhani hawajui hata maximum temperature ya gear box? Mkuu, elimu zenu zitumieni vizuri, msiwe kama wanaobadili jinsia, wanaona Mwenyezi MUNGU amekosea kuwaumba. Usiwe fundi mzuri anayewapotosha wateja kwenye mambo madogo wakati mambo mengi unatoa elimu nzuri
 
Binafsi nataka niimwage yote niweke ile ya Toyota kabisa halafu niwe nabadili kila baada ya km 20.000.
Mkuu kwenye ATF hakuna huo utaratibu, jitahidi kusoma Manual ya gari yako. Kuna gear box nyingine hupaswi kabisa kubadilisha fluid Hadi hapo gear box itakapokuwa kuwa imekufa
 
Naunga mkono hoja.

Kutobadili ATF ni kuua gear box.
Sio kweli. Watengenezaji wanajua kuliko wewe ndio maana wanapokuuzia gari wanakupa waranti kabisa ikiwa ni pamoja na sharti kuwa ATF ibadilishwe km kadhaa, unazani wao ni wajinga? Yaani ni kama wale wakikaa kwenye vijiwe wanaambiana gari ikifika km kadhaa unatakiwa ubadilishe oil viscosity tofauti na maelekezo ya kwenye Manual, who told you this?
 
Huwa namwaga ATF nikifanya service ya km 3000.

Sasa nitamwaga kila baada ya km 15.000.
Hahaha! Kweli wewe ni mzee wa kula kuku vipaja then nyama inayobaki unatupa unasema ni mifupa! Mkuu, soma Manual, ATF hazibadilishwi kama Oil labda kama unaweka ATF fake fake. ATF ni km elfu 60, kama utawahi sana basi ni km 40,000
 
Nani aliwambia kila ukifanya service ya engine oil lazima umwage Atf pia? Nadhan mnashauliwa na mafundi kwa sababu tu mnaweka atf ambazo hazina ubora wowote ule na ambazo sio recommended
Wanaweka ATF fake ndio sababu. Anapaswa aweke ATF ya toyota 110,000. Watu wanaweka ATf za elfu 30 unategemea nini. Pia wanashauriwa na mafundi mchundo wazee wa filter za elfu tatu na oil ya SAE40
 
Watu wengi wanaobadilishia ATF kwenye magereji wanabadilisha between 9,000km to 15,000km.

Yaani ATF inatoka bado mpyaaaa. Huko ni kuchezea hela.
Infact ni upuuzi. Ni ufujaji! Hawasomi Manual za magari yao, wao wanafuata mkumbo tu, hawana hoja.
 
Bado nasoma naona maelezo ni mazuri na yanaeleweka. Baadhi ya mafundi wetu nafikiri hawana utaalamu wa izi mambo za gearbox... Nashukuru sana kwa somo hili naamini magari yetu sasa yatapona
 
Back
Top Bottom