Katika kipindi cha Utawala wa CCM kuna Sheria zilitungwa na kupitishwa na Wabunge wa CCM bila kutumia Busara. Leo hii zinaigharimu Serikali ya CCM.
1) Sheria ya FAO LA KUJITOA na KIKOKOTOO KIPYA. Sheria hii ni Sheria yakipuuzi Sana. Sheria hii haimuhusu Rais wala Mbunge Ila inawahusu watumishi wa Umma na wa Private Sekta Tu. Kama Sheria hii ni Nzuri Kwanini isiwahusu Wabunge waluoitunga na Rais aliyeisign?? Kwa Sheria hii ukiacha kazi leo Kwa hiari yako Ili ujifanyie Mambo yako, mafao yako hupati Hadi ufikishe umri wa Miaka 60. Ikumbukwe hii ni fedha ya Mfanyakazi, anapaswa kuwa na Uhuru nayo mana ni Haki yake. Ila wabunge wa CCM Kwa majigambo na Kebehi nyingi wakaipitisha na Rais Akaisaini Ili itumike. Aidha, kuhusu KIKOKOTOO Kwa wastaafu. Huu ni Mwiba mwingine Kwa watumishi wastaafu wa sekta zote isipokuwa Wabunge na Marais.
2) Sheria ya "MALUPULUPU" ya Viongozi wa Kisiasa. Tumeona juzi Maraisi wetu wanajengewa Majumba ya Kifahari, wanalipwa mshahara 80% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani, wanatibiwa nje ya Nchi Kwa mabilioni ya Wananchi fukara kama alivyotibiwa Ndugai Kwa Kulala hotelini. Mishahara Yao mikubwa Ila haikatwi Kodi. Sheria hizi ni kandamizi na ni za kinyonyaji. Nchi zilizoendelea hazina upuuzi huu wa kifalme, Mathalan, Kwanini wasikatwe Kodi wkt kila mwananchi ana wajibu wa Kulipa Kodi??? Viongozi wa kisiasa ni watumishi kama wengine so wanachofanyiwa wao wafanyiwe pia na watumishi wengine. Otherwise, tuachane na Sheria za kinyonyaji hizi. Yani mumuhudumie mtu akiwa madarakani, na akistaafu pia mumuhudumie? Pension yake inafanya kazi gani? Mbaya zaidi wawapo madarakani hawawagi waaminifu, wanatuibia via mikataba ya kishenzi.
3) Sheria ya Vyombo vya Habari. Hapa pia kuna Sheria ya Kikoloni. Kimsingi Sheria hii inaviziba mdomo Vyombo vyetu vya habari. Wabunge wa CCM walipitisha Sheria hii Kwa dharau na Kebehi nyingi na kujisahau kuwa Nchi hii ni Mali ya Wananchi.
4) Sheria ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Sheria hii ilipitishwa kibabe na kupandisha makato Hadi kufikia 15% ya mshahara Kwa Mwezi kinyume na mikataba. Aidha, kuna urasimu na ubaguzi mwingi wakati wa kuomba hiyo Mikopo. Sheria hii inagusa familia nyingi za wafanyakazi na waombaji wa Mikopo (Wanafunzi).
Wakati tunaikaribia Siku ya tarehe 28/10/2020. Tutafakari namna Sheria hizi kandamizi zilivyotungwa, wahusika waliozitunga na kuzipitisha na Malengo Yao hasa. Halafu tupime kama wanasifa ya kuendelea kutuongoza.
Haiwezekan ujinasibu kiwa unawapenda wafanyakazi halafu unapitisha Sheria ya FAO la KUJITOA au LiKIKOKOTOO la ajabu. Tena ni Kwa watumishi wa chini Tu na sio wabunge waliotunga Sheria hiyo.
Huwezi sema unawapenda wananchi wakati Unawanyonya Kwa kupitishwa Sheria za kinyonyaji na zenye kuakisi ubinafsi mkubwa.
Huwezi sema nchi ipo Huru wkt mnatunga Sheria zinazodhibiti Uhuru wa wananchi wa kuexpress hoja zao.
Haiwezekan useme unawapenda Wanafunzi halafu unawabagua kwenye kupata Mikopo wakati Baba zao wanalipa Kodi kubwa kuliko wale wanaopata Mikopo kisa Tu walisoma Private.
Sheria hizi ni mfano wa Sheria nyingi zilizotungwa na Bunge letu linaloongozwa na idadi kubwa ya Wabunge wa CCM ambazo zinaashiria hawajui wajibu wao na wawapo Bungeni mana wanadhani wapo pale Kwa NIABA Yao wenyewe. Yaani wanasahau kupigania maslahi ya Wananchi waliowatuma. Hivyo, tukumbuke Sheria hizi wakati tunasogelea sanduku la Kura tarehe 28/10/2020.