Baadhi ya Sababu zinazopelekea Huduma Mbovu/mbaya kwa wateja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baadhi ya Sababu zinazopelekea Huduma Mbovu/mbaya kwa wateja

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by CHASHA FARMING, May 31, 2012.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  BAADHI YA SABABU ZA HUDUMA MBAYA KWA WATEJA
  [​IMG]

  SABABU ZINAZO PELEKEA HUDUMA MBAYA KWA WATEJA

  1. Wafanyakazi hawajafundishwa


  Hii inaweza kuwa ni sababu namba moja kabisa na kubwa ya customer service mbovu, wajasiriamali wamekuwa wakiajiri watu bila kuwapa elimu matokeo yake wafanya kazi wanatuma ozoefu wao tu
  Mfano: Kuajiri Ndugu, jamaa, marafiki, mke/mme hawa watu mara nyingi huwekwa kwa kigezo cha undugu na si kigezo cha kuwa na uelewa wa kutosha kusimamia biashara

  SULUHISHO: Nilazima tuwekeze katika kufundisha wafanyakazi wetu jinsi ya kuwahudumia wateja hii ni kwa biashara ambazo huwa zina intaraction kati ya wateja na wauzaji kama Hoteli, Dukani, Baa na kazalika

  2. Kuto kujari

  Hapa ni kwamba mjasiriamali haoni umuhimu wa kuwa na watu wa kutoa huduma au kuwahudumia wateja vizuri, hili ndo tatizo letu tunacho anagalia ni pesa imeingia jioni yanafanyika mahesabu kwisha kazi, Hata kama mfanyakazi kapigana au kutukanana na mteja tajiri hajali anacho jari ni pesa inaingia

  3. HUJUMA

  Wafanyakazi kuwa na hasiria au kuwa na furastration ni sababu nyingine ya kuamua kufanya wanavyo jua, nazani, mafanya kazi anaweza amua kujibu mteja anavyo jisikia yeye kwa sababu tu akukomoe wewe tajiri wake, Hujuma dhidi ya tajiri mara nyingi huwa ni chnazo cha poor customer service

  SULUHISHO: Wewe kama mkurugenzi ni lazima kuongea na wafanya kazi wako mara kwa mara kusikiliza matatizo yao na kuyatatua ili wasihamishie hasira zao kwa wateja


  4. Wafanyakazi kuto kuwa na Imani na bidhaa au huduma

  Hii mara nyingi hutokea pale ambapo matangazo ya dumua fulani au bidhaa hayaendani na uharisia matokeo yake wafanya kazi wanakuwa wanaogopa hata kuwahudumia wateja au wanabaki kusema subiri tukuitie mtu akupe maelezo zaidi

  Au utakuta matangazo yanasema vingine na wafanyakazi wamefundishwa vingine, utakuta bei ya Tangazo la Wali kuku ni buku 3, lakini ukiingia ndani mfanaya kazi anakupa bei nyingine kabisa buku 4

  SULUHISHO: kuwa mkweli katika ubora wako na matangazo yako ya masoko na ikitokea tatizo li fix mara moja na wateja wajue

  [​IMG]


  5. Matatizo Binafisi ya Mfanya kazi yanapo jionyesha kazini

  Utakuta mfanyakazi anamatatizo binafisi ya kifamilia au hata ya kiafya na yale matatizo yanakuwa yanaonekana hadi kazini,

  MFANO: Mfanyakazi kugombana na rafiki yake/mke wake/mme wake na kazalika na ule ugonvi unakuwa bado kichwani mwa yule mfanyakazi na unauhamishia kazini na hapa huenda akawa anatpoa huduma huku ana hasira, mawazo na kazalika

  SULUHISHO: Hakikisha unonana na wafanyakazi wako kabla hawajaanza kazi, au hakikisha unakuwa unawachunguza mara kwa mara ili kuona kama mfanya kazi ana mabadiliko fulani make matatizo yanaweza yakamkuta akiwa kazini kupitia simu. Saa zingine hakikisha wafanya kazi wanapo ingia kazini wanazima simu zao na wawashe muda wanaondoka, make kitendo cha simu kuwa oni wakati anawahudumia wateja anaweza pata ujumbe wa kufiwa au kupigwa chini na mpenzi wake na kupelekea hata kupia yowe kazini


  6. Lawama nyingi kwa mfanayakazi

  Unnweza kuta kila mfanya kazi wako akikosea kidogo unampandishia, unamulaumu sana, unatishia kumfukuza kazi na kazalika, hili nalo hushusha morali ya yeye kufanya kazi vyema

  SOLUTION: kuongea na wafanya kazi wako vizuri na hata kama amekosea subiri amalize kazi kabisa ndo umuite na umugombeze na si kumgombeza papo kwa papo


  7. KUSHINDWA KUTATUA MATATIZO YAO KWA WAKATI

  Kushindwa kutatua matatizo yao kutapelekea wakose molari na kazi na hivyo kukuletea hasara ndani ya kampuni

  8. Wafanyakazi kuto kuona Umuhimu wao au majukumu yao

  Mfanyakazi anaweza asione umuhimu wa yeye kuwahudumia wateja vizuri kwa sababu haoni umuhimu wa kufanya hivyo kwanza kampuni si yake wala ya Baba yake so haoni umuhimu wowote ule

  SULUHISHO: Kumbuka kwamba wafanyakazi ndo hubeba image ya kampuni hivyo waelimishe wafanya kazi wako umuhimu wao kwenye kampuni, waambie hii kampuni bila wao si kitu, waambie huduma yao nzuri ndo itasababisha kampun I ipate pesa za kuwalipa mishahara

  9. Top management kuto kutatua matatizo mengine yanayo husu wateja, mfano huduma au bidhaa

  Mfanya kazi anaweza amua kuwa na hasira au kuacha kabisa kuwahudumia wateja endapo kuna matatizo yanakuwa hayatatuliwi na kampuni kwa wakati,

  MFANO: Simu ya kampuni ni mbuvu na management imeshindwa kuitengeza kwa wakati, hii inaweza pelekea mtoa huduma kwa wateja kukasirika

  SULUHISHO: Jitahidi kutatua kwa wakati matatizo yote yanayo husiana na huduma kwa wateja


  10. Mishahara midogo, hakuna malupulupu

  Utakuta wafanya kazi wanacho zalisha ni tofauti na wanacho lipwa hapa ni lazima wakate tamaa na waamue kutoa huduma duni kwa wateja

  SULUTION: Walipe vyema wafanyakazi wako ili basi na wao watoe huduma bora kwa wateja

  11. UCHOVU
  Wafanya kazi kuchoka sana wakiwa kazini inaweza kupelekea kutoa huduma duni kwa wateja
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  wafanyakazi kutokuwa na uchungu na biashara za wamiliki
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  1. Kuleta matatizo ya familia ya nyumbani kaizini.
  2. Kutopewa training ya kutosha ( mtu hata hajui products anazouza vizuri hapa huduma lazima iwe poor)
  3. Maslahi duni

  Hizi kwangu ndio top 3
   
 4. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkubwa! Chasha ,salute kwako
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mfumo wa kuwa kila kitu ni mali ya umma.
   
 6. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu asante. Hili ndilio tatizo kubwa tulilo nalo hapa kwetu. Ule mfumo tuliokuwa nao wa 'undugu' ndio uliotufikisha hapa.

  Dhana ya kuwa yupo 'mhudumu' na 'anayehudumiwa' haipo na hakuna anayeonekana kujali.
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Upande wa serikali ni ile kitu inaitwa Permanent employment , ingekuwa mikataba miaka 3 inafanyiwa review tungekuwa na watendaji wazuri sana serikalini.
   
Loading...