Baadhi ya raia zanzibar hawana imani na tume

Mr.Toyo

JF-Expert Member
Feb 9, 2007
433
117
BAADHI YA RAIA ZANZIBAR HAWANA IMANI NA TUME YA KUCHUNGUZA MV SPICE ISLANDER, WATAKA IBADILISHWE22/09/2011
0 Comments


[COLOR=#666666 !important][FONT=Verdana !important]Serikaliya Zanzibar imeshauriwa kuangalia upya tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kuzama meli ya MV Spice Islanders na kuua watu 204 Septemba 10, mwaka huu.

Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wananchi waliokuwa wakizungumza na Nipashe katika Manispaa ya mji Zanzibar, baada ya Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee kutangaza majina ya wajumbe wa tume hiyo.

Hassan Kombo mkazi wa Chukwani, alisema ameshangazwa na Serikali kuteuwa baadhi ya wajumbe ambao wana nyadhifa za uongozi katika mamlaka zinazotakiwa kuchunguzwa ikiwemo Shirika la Bandari (ZPC) na Mamlaka ya Usafiri baharini (ZMA).

Alisema kwa kuzingatia misingi ya utawala bora wajumbe ambao wana nyadhifa katika mamlaka zinazohitaji kuchunguzwa ni vizuri wakajiondoa na kuteuliwa na vyombo vyengine kushika nafasi hizo, “Haiwezekani hakimu kusikiliza kesi inayomuhusu baba yake lazima mgongano wa kimaslahi utatokea, wajumbe wa tume waangaliwe upya haki itendeke,” alisema.

Wajumbe ambao wametajwa na baadhi ya wananchi kuwa hawafai kuwemo katika tume hiyo ni mwanasheria Salum Taufik ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Shirika la Bandari na Shaaban Ramadhan Abdallah ambae ni mjumbe wa bodi ya Malamaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar.

Mwengine ni Kepteni Abdallah Yussuf Jumbe ambae imeelezwa kuwa ana uhusiano wa kifamilia na Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Zanzibar, Mustafa Aboud Jumbe, jambo ambalo linaweza kuathiri utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.

Juma Mussa Ali Mkaazi wa Bububu alisema haikuwa mwafaka kuteuliwa kwa mkuu wa Kikosi cha KMKM, Hassan Mussa Mzee na Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la wanamaji Meja Jenerali Saidi Shaaban Omari, wakati wao wanalaumia kwa kutofika kwa muda muafaka katika kazi ya uokozi baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Aidha alisema ameshangazwa na Serikali kuunda tume bila ya kuipa muda wa kukamilisha ripoti na hadidu rejea za maeneo yanayohitaji kufanyiwa uchunguzi na tume hiyo.

Mariam Ishaka, mkaazi wa Mbweni alisema mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Shaaban Ramadhan Abdallah, hakustahili kuteuliwa na kupewa nafasi ya Katibu wa tume hiyo ya uchunguzi wakati yeye ni mjumbe wa bodi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini.

[via Nipashe]
[/FONT][/COLOR]source: Baadhi ya raia Zanzibar hawana imani na tume ya kuchunguza MV Spice Islander, wataka ibadilishwe - Wavuti
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom