Baadhi ya Polisi wanachochea migogoro ya wakulima na wafugaji badala ya kudhibiti

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,212
2,808
Serikali iangalie kiundani swala hili kwani imekuwa ni kawaida sasa badala ya kupungua ndo kila siku migogoro hiyo inazidi

Wafugaji mara nyingi wanakuwa wana umoja sana kiasi kwamba wapo tayari kwa lolote kivyovyote. Wafugaji wanachangishana fedha za kutosha tu kwajili ya kusolve ishu za kuhusiana na mifugo yao

Mfano Kibrashi iliyopo Kilindi Tanga ng'ombe waliingia kwenye mashamba wakulima wakakamata na kuwapeleka ofisini. Mwenyekiti akawasiliana na Mwenyekiti mwenzake wa upande wa walipotokea ng'ombe na wakaelewana kuja kuyajenga (kuyamaliza) siku inayofuata

Cha ajabu kabisa ni kuwa polisi wakavamia siku ile ile wakiwa full prepared wakawatoa wale ng'ombe kwa kufosi na kama haitoshi wakawapa mkong'oto wakulima na mabomu ya machozi juu

Sasa mtu unabaki unajiuliza kwa hali hii migogoro itaisha kweli hii? Maana yanakuja yaleyale ya vita ya dunia watu wanapigana kumbe Mmarekani anafaidika au yale ya uasi unaoendelea nchi nyingi duniani na machafuko huku wengine wakivuna na kufaidika
 
Back
Top Bottom