Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Uko sahihi mkuu, nini maoni yako kuhusu app ya kukutanisha wapangaji na wenye nyumba regarding your view

Sent using Jamii Forums mobile app
Kimsingi kabla hujafikiria kutengeneza app yoyote, ni lazima kwanza ujue una lenga kutatua tatizo lipi hasa. Unafanya uchambuzi wa tatizo, solution unayotoa..na kwa namna gani itaondoa au kupunguza tatizo.

Nadhani app ya kuwakutanisha wapangaji na wenyenyumba kwa kupitia madali au moja kwa moja ni wazo zuri.

Lakini narudi pale pale..inahitaji mkakati madhubuti kufanya watu watumie.

Ubaya wa app za namna hii siyo regular. Yaani mtu anaweza kuihitaji mara moja kwa miaka 3.
 
Hakuna jambo gumu hapa duniani ni wewe kuamua tu amini ninachokuambia brother.
Ingia playstore uone jinsi kulivyo na app nyingi ambazo hazina download hata 10 zaidi ya miaka kadhaa.

Biashara ya app siyo tu kujua ku develop nankujifungia una develop app na kuiweka play store umemaliza. Biashara ya app biashara kubwa ambayo inahitaji mamillion ya fedha na business plan nzuri.

Vijana wengi wanakwama kwa sababu anadhani akijua ku develop app tu basi amemaliza. Mwisho wa siku wanaangukia pua.
 
Usijikatishe tamaa, mimi nimetoa wazo ambalo nimeshalifanyia utafiti brother usiniulize kwanini sijafanya.

Faida: Utapata 20% ya project yako vizuri tu kwa tozo ya 10% toka kwa mteja na 10% toka kwa mmiliki.

Ajira: Tafuta vijana 2 au 3 wafanye door to door marketing kwa target ya hao wamiliki, inawezekana naongea nikiwa ninauhakika inakwenda.

Mbinu kibiashara: Brand Mobile App yako kupitia Social media zinazotumika sana hapa Tanzania ukianzia na INSTAGRAM, FACEBOOK, TWITTER na LINKED IN. Utanishukuru baadae.

Wewe: Utakuwa unaweza kuangalia wapitiaji wa mtandao wako kila mara.

Faida ya ziada: Mobile App yako ikiwa na traffic jam nzuri kampuni kubwa watajileta wenyewe wafanye matangazo mengine kupitia Mobile App yako. Japo hii usiiweke maanani sana japo baadae ukiwa vizuri utaenjoi.

Mrejesho: Ndani ya wiki moja mkipiga kazi utapata wateja, kutokana na uzoefu wangu wa tafiti brother. Walipe vijana promise & good commission nakuambia utamake life.

Karibu "wauza mawazo ya biashara"
 
iMind, Biashara ni kutengeneza fursa sio kutatua shida maana kutatua changamoto ni kazi ya Serikali sio biashara bali huitwa ustawi kwa wote.

Fanya tafiti, tengeneza hiyo Mobile App kiasi ingia field wewe mwenyewe utaniambia itakavysound vizuri Brother. Shida vijana hamfanyi tafiti mnataka kufanya kitu ambacho mpate sifa kwa jamii na huku huingizi chochote. Vijana wenzenu wanamake kwa kutengeneza hizo hizo Mobile App za wauza Kuku na Keki huku Mkoani na maisha yanaenda poa.

Haahaa, acheni mawazo hasi vijana pambaneni kila jambo linawezekana.
 
Mi mwezi ujao nitaenda kuwaambia lile darasa letu tuliomaliza miaka ile nusu tuko majobless tunapiga roba za mbao huko mtaani na tukijitahidi sana tunakua waendesha bodaboda kwa mkataba na boss.

Ndio maisha yetu hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vizuri, watajua makosa na mazuri yao kupitia wewe kama mfano na wengine watakao enda na pia watajua ni wapi warekebishe maana hata mpango wa elimu unataka hivyo.
 
Wasomi wengi mkuu wameshakata Tamaa kwani , kwan matarajio yao yamekua tofauti , unavyoendelea kuandika haya unazidi kuwachanganya tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio tatizo waende tu ktk shule walizomalizia elimu zao ili wajue hawana uwezo wa kutengeneza vijana wenye uwezo wa kupambana na soko la ajira.

Ninaimani watafanya maboresho ya kimkakati kupitia program zao ili kuliepuka hilo tatizo au kulitatua kabisa.
 
Biashara ni kutengeneza fursa sio kutatua shida maana kutatua changamoto ni kazi ya Serikali sio biashara bali huitwa ustawi kwa wote.

Fanya tafiti, tengeneza hiyo Mobile App kiasi ingia field wewe mwenyewe utaniambia itakavysound vizuri Brother. Shida vijana hamfanyi tafiti mnataka kufanya kitu ambacho mpate sifa kwa jamii na huku huingizi chochote. Vijana wenzenu wanamake kwa kutengeneza hizo hizo Mobile App za wauza Kuku na Keki huku Mkoani na maisha yanaenda poa.

Haahaa, acheni mawazo hasi vijana pambaneni kila jambo linawezekana.
"Biashara ni kutengeneza fursa na sio kutatua shida "

Hapo umemaliza kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu uwafuate hao hao wanaolia mishahara kiduchu hivyo waongezewe unafikiri watakusaidia nini, na ndiyo haohao walikua wanaombea mfeli wakiamini serikali itawaongeza mshahara ili waongeze juhudi za kufundisha, me naona hakuna msaada wowote utakaoupata kutika Kwa hao walimu sijui
 
Ingia playstore uone jinsi kulivyo na app nyingi ambazo hazina download hata 10 zaidi ya miaka kadhaa.

Biashara ya app siyo tu kujua ku develop nankujifungia una develop app na kuiweka play store umemaliza. Biashara ya app biashara kubwa ambayo inahitaji mamillion ya fedha na business plan nzuri.

Vijana wengi wanakwama kwa sababu anadhani akijua ku develop app tu basi amemaliza. Mwisho wa siku wanaangukia pua.
Mkuu iMind unayoongea ni kweli lakini ninapna una hofu sana ushindani ni lazima uwepo na ubunifu na marketing ndio solution

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu uwafuate hao hao wanaolia mishahara kiduchu hivyo waongezewe unafikiri watakusaidia nini, na ndiyo haohao walikua wanaombea mfeli wakiamini serikali itawaongeza mshahara ili waongeze juhudi za kufundisha, me naona hakuna msaada wowote utakaoupata kutika Kwa hao walimu sijui
Saidia Baba nchi yako, huwezi jua ya kesho.
 
Habarini wana jukwaa hili. Naimani mko poa sana wa afya.

Niingie moja kwa moja kwenye mada, nina ndugu yangu anauza stationary na wadau wengi wanaoumzunguka eneo lake ni waendesha kirikuu (vigari vidogo vya mizigo).

Nimewaza sana, je ni biashara gani naweza invest ukiachana na vinywaji, chakula, karanga na chai?

Mawazo yako naomba Biashara ya mtaji mdogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibu!

Niende moja kwa moja katika mada;

1. Utajiri
Siri kubwa duniani ya utajiri ni wizi. Dunia hii waliofanikiwa na kuwa matajiri ni wezi narudia tena utajiri wahi dunia upo katika uwezo wa kuiba chochote itategemea unapenda uibe nini ili iwe nini katika maisha yako.

2. Biashara
Biashara na utajiri ni vitu viwili tofauti na usihadaike na maneno ya watu kuwa ukifanya biashara unaweza kuwa tajiri hapana. Isipokuwa ukiwa mwizi kwa kivuli cha biashara ndio utaweza kuwa tajiri.

Biashara ni ajira kama zilivyo ajira nyingine. Watu wote unaosimuliwa au kuwaona hapa duniani ambao ni matajiri tambua hao ni wezi wazuri sana. Uzuri wa wizi unatofautiana na juhudi uliyonayo.

Kibwagizo, ukiwa mwizi hutakaa uwe na amani kwenye maisha yako yote na kila atakayekupinga kihisia au kimawazo au kiuwezo hautaweza kumvumilia utamuona ni adui mkubwa.

Mwisho

Kuwa makini na mwangalifu katika maisha yako acha kutamani kuwa mwizi acha tamaa ya utajiri.

Rejea;
a) Nchi tajiri
b) Watu matajiri
 
Back
Top Bottom