Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Nami naomba nichangie kidogo...

Mi nafikiri alichoandika mdau Chasha ni cha kweli. Tusianze kulalamikia mitaji kama excuse. Cha msingi ni kuwa na nia thabiti, ambayo kwayo inatoa nguvu kubwa sana. Ukiwa na nia, unaweza kutafuta mtaji through kupiga debe, kufanya vibarua and the like.

Nilijaribu kuongea na rafiki zangu pale Kariakoo, ambao wanauza maji, ambao walinieleza kuwa ukiondoa mtaji, wanaweza kutengeneza ziada ya Tsh. 12,000-13,000, na siku ya biashara mbaya wanatengeneza ziada ya Tsh. 4000 at minimal.

Aidha, wale akina mama wanaouza matunda nao wana make ziada ya kiasi kama hicho,ambapo wao wanachukua matunda kule Temeke Stereo kwa Tsh.50-70 kwa embe moja,lakini kariakoo wanauza kwa Tsh. 250-300, na kwa juhudi zao matunda haya yanaisha.

Niliozungumza nao wananieleza tayari wameshanunua plots (walianza biashara hiyo miaka mi3 iliyopita). Hawa waliongozwa na nia iliyowapa nguvu ya kusonga mbele, japo vipo vikwazo walivyokutana navyo, nawanavyokutana navyo, lakini wanasonga mbele.

Hivyo,nafikiri mtaji mkubwa aliokuwa nao mtu ni mind set,na mtaji mwingine ni kuwa na mahusiano mema na jamii, ambayo kwayo unaweza pata mawazo mengi mazuri, na inawezekana ukaaminika na mtu/watu w/akakupesha mtaji.

Nawasilisha mchango wangu
IJOZ na CHASHA mumenifunza kitu kikubwa sana
 
Moja ya njia ambazo huwa naaziangalia ili kuweza kupata wazo la biashara ni short and clear

FOOD, SHELTER AND CLOTHES

Ukisahavijua hivi nirahisi kuweza kujibu ni wap na utaifanayaje eyo biashara

1.Kwa biashara ya chakula
- hapa lazima uwe na target labda waweza weka target kwa wale wa makazini gov and private sectors
hapa waweza hata angalia mazingira na ufanyaje ili kuweza kuwavutia wao kuja kula kwako au kuagiza toka kwako

Zingatia
pishi bora ,vikorombwezo yaani (kachumbari pili pili) na hata kuwek kijitunda either ndizi au kijichungwa ili kumvutia mteja

Pili ni kwa wageni (tourists) waweza fungua mgahawa wakisasa na maalum kwa kuwapatia huduma ya chakula hawa tourist,

Kwa hapa Tanzania ili kuweza kuwin hili soko ambalo unataka kulitenegeneza cha kwanza ni kuhakikisha unaweka direction ambazo tourist hato pata tabu kufika katika restaurant yako

Pia weka vitu ambavyo tourist anapenda vile vya asili na pia yale mapicha yetu na vinyago kama urembo

Ni hayo tu, mengine yanajieleza.
 
Mko wapi wale wadau wa kudadavua

Mi nimesoma kuanzia mwanzo mpaka mwisho nahisi kama nastahili cheti asee, hii ni zaidi ya chuo.
 
Hiyo namba 6. Mimi nimeona fursa nyingi mtaani kwangu, ila tatizo hapa mtaani kuna uswahili mnooo. Hawanaga tabia ya kupenda kuungishana, wana roho mbaya ajabu, mtu yuko tayari akanunue biashara Mtaa wa 7 lakini sio kwako, nlipohamia mtaani wenyeji waliniambia hayo yote nikapinga, nikafungua saloon ya kike na kiume, aah wapi, akaja mpemba na roho yake ya paka, akachemka. Sasa watu hawa unatumia mbinu gani kuwawin.
 
Hiyo namba 6… .. Mimi nimeona fursa nyingi mtaani kwangu, ila tatizo hapa mtaani kuna uswahili mnoooo…. Hawanaga tabia ya kupenda kuungishana, wana roho mbaya ajabu,… mtu yuko tayari akanunue biashara Mtaa wa 7 lakini sio kwako,… nlipohamia mtaani wenyeji waliniambia hayo yote nikapinga,… nikafungua saloon ya kike na kiume, aah wapi… akaja mpemba na roho yake ya paka, akachemka…. Sasa watu hawa unatumia mbinu gani kuwawin
Dawa yao fanya kile ambacho hakipo kabisa watakuwa hawana ujanja. Ukifanya kile ambcho na wao wanafanya itakuwa ngumu sana.
 
Aisee mimi ni Kaka, Ok, ni kweli tuko hapa kusaidiana, Ila kiukweli inatakiwa watu wabadilike, kusoma thread kama hizi nakuishia kusifia haisaidii chochote, unatakiwa kuchukua maamuzi magumu kabisa, mimi naamini watu waote wano pita/kuingiaknye hili jukwaa ni wale wenye nia au tiyari ni wajasirimali
Madini
 
Write your reply... kwa aliepata chuo cha ustawi ngazi ya cheti na anahitaj chumba karibu na chuo cha ustawi wa jamii bamaga
 
Wapendwa, mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu ambao sasahivi nakaribia kuhitimu, hivo basi mara nyingi huwaga nawaza sana kuanza biashara ya bodaboda, kwa hiyo ningepnda mtu ambao akona experience ya hiyo biashara anieleze. Je, inanufaisha na challenges zake ni gani.

Thanks
 
314 Reactions
Reply
Back
Top Bottom