Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Messages
291
Points
500

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2017
291 500
Habari Tanzania!

Sasa kwa wale ambao wanapenda kuchangamkia fursa hii kazi kwenu.

Wazo: Unaweza ukatafuta vijana wa aina ya biashara unayoitaka kuifanya yaani wewe mtaji wako ni wafanyakazi (wenye ujuzi au kinyume chake) ambao umewatafuta na kuwaweka katika kanzi data yako kwaajili ya mauzo kwenda kwa mtu binafsi au taasisi.

Jukumu lako: Unatakiwa utafute nafasi za kazi sehemu mbalimbali aidha kwenye mashamba, mashule, majumbani, mahoteli, migahawa, maduka, maofisini au utakavyoona. Baada ya kupata sehemu unaingia mkataba na hao watu au taasisi wanakulipa pesa kutokana na huduma yako ya kuwapelekea wafanyakazi uliowataini na kujiridhisha wanaweza kupiga kazi. Ukiwa unataarifa zao zote muhimu zinazohitajika kitaifa na kimataifa.

Utapiga hela na utafanikiwa sana. Najua wapo watakaosema huu ni utumwa ndio kazi yoyote ya kuajiriwa ni utumwa tu. Mfano timu za mpira wanafanya, recruitment agencies, taasisi za kimataifa kubadilishana wafanyakazi nk


Hii biashara inasoko sana Tanzania kwa ujumla. Kazi ni kwako.

Karibu

"wauza mawazo ya biashara"

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Messages
291
Points
500

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2017
291 500
Siku na iwe njema kwenu.

Leo nimejisikia kuongea na nyinyi wasomi wa ngazi zote kuanzia shule ya msingi, sekondari msingi, sekondari kuu, vyuo vya ufundi, vyuo vya kati na nyinyi wa vyuo vikuu.

Kama ulibahatika kusoma ngazi yoyote ya elimu tambua unajukumu la aidha wewe kwenda kwenye taasisi uliyosoma ukawafahamisha upo wapi na unafanya nini au shule yako ya awali au msingi wafanye tafiti wajue waliowafundisha wapo wapi, je walifanikiwa kufika ngazi ipi kielimu na je sisi kama taasisi tutawasaidia nini au kuwapata kwa njia gani nzuri tusonge mbele.

Wapendwa kama haya hayajafanyika ni vizuri tukafahamu na kutambua sasa elimu tuliyonayo ni batili na haitaleta mchango chanya ktk taifa letu.

Sababu kuu zipo za kujua taarifa zako;

1. Ili waweze kuboresha huduma yao ya kielimu kwa kutambua wapi wanakosea waboreshe na wapi wanapatia watilie mkazo.

2. Watajua nini wafanye na sehemu ipi panauhitaji wa hicho wanachotaka kukifanya.

3. Mwisho sio kwa umuhimu watajua namna bora ya kujua kama huwa wanaweza kuandaa wafanyabiashara, wakulima, viongozi, watumishi bora au kinyume chake.

NB

Wasomi wa vyuo vikuu ni vizuri sasa mkawa mnafanya tafiti za kumaanisha kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia tuachane na ujanja ujanja ambao hautalisaidia taifa zaidi ya kukusaidia wewe binafsi na familia yako ambayo ni sehemu ndogo sana ya sisi taifa Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Messages
291
Points
500

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2017
291 500
Hello Tanzanians!

Kwa vijana mliosoma IT & Computer science mnaweza mkatengeza Mobile Software Application (Mobile App) nzuri ambayo itakayoweza kutoa huduma na wewe mtengenezaji ukawa Controller wa hiyo huduma.

Mfano, ukaamua kutengeneza Mobile App ya huduma ya Car Parking Spaces kwa mkoa wa Dar es Salaam yote. Mtu ambaye aidha ni mwenyeji au mgeni katika jiji hilo ataweza kuweka oda ya parking ya gari au chombo chake cha usafiri ili asikose mahali pakuhifadhi usafiri wake na hii itasaidia kuongeza usalama kuwa mkubwa na kutengeneza ajira za kutosha.

Ushauri wa tozo: Kula 10% ya mteja (customer) na 10% ya mwenye huduma (Space owner) au kinyume chake.

Mifano ya huduma nyingine;

1. Uuzaji wa vyakula vya bei nafuu (migahawa badhifu yenye bei isioumiza).

2. Huduma ya choo na bafu

3. Kumbi za harusi na sherehe

4. Kumbi za starehe na bar

5. Nyumba za kulala wageni classic ila bei isioumiza.

6. Maduka yenye kutoa huduma ya bidhaa mbalimbali masaa 24 siku 7 za wiki (24/7).

7. Vibanda vya huduma ya chipsi safi, kongoro, supu mkia wa mbuzi, makange nk

8. Sehemu zenye watu watoa huduma za ucheshi nk

9. Car wash

10. Vehicles parking

11. Sehemu ya kupumzika yaani open space free charge area nk

12. Utajiongeza na wewe

Haya mawazo hayahitaji mtaji zaidi ya Tsh. 50,000/=. Kijana msomi kazi ni kwako.

Kuhusu soko ni mkoa uliopo na wilaya zake hii inaitwa kutembelea nyota.

Karibu "wauza mawazo ya biashara"

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Messages
291
Points
500

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2017
291 500
Umeongea kitu muhimu lakini si unajua ubunifu kwetu ni changamoto.

Mimi ningekuwa mtaalamu wa IT ninge "design " mobile app ya real estate itakayowezesha wenye nyumba na wapangaji kukutana with sufficient details bila madalali

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana brother. Ni kuamua tu maana kwasasa dunia ipo katika teknolojia.
 

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Messages
291
Points
500

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2017
291 500
Unamaanisha kuwa "Recruitment agent" kama wanavyofanya Radar, Em-Power, Erolink na wengine, au??

Sent using Jamii Forums mobile app
More than recruitment agencies brother. Maana kuna sehemu wanatafuta nguvu kazi na hakuna watu, maeneo mengine wanatakiwa wataalamu lakini napo hakuna watu.

Unatakiwa uwe mtu wa taarifa za ajira kutokana na kundi la watu unaotaka kufanya nao kazi ikiwezekana unaweza kuwafanyia relocations ya wafanyakazi mzee baba.

Yote yanawezekana.
 

iMind

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Messages
2,119
Points
2,000

iMind

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2011
2,119 2,000
Ndugu tambueni kuwa kutengeneza app si tatizo. Unaweza kutengeneza app ya wazo lolote lile. Ila changamoto ni
1. Kufanya watu watumie app
2. Kutengeneza fedha (Monetizing) from your app.

Katika idea zoteulizoandika hapo sioni hata moja ambayo inaweza kutumika through an app na ikatumia pesa.

Kwa mfano: Uta reserve parking za halmashauri kwa app. Je utazuiaje mtu asipaki kwenye hiyo parking? Unahitaji miundo mbinu ya ziada. Je ghalama ya kuweka hiyo miundombinu ni shs ngapi na nani ataigjaramia. Je kutakuwa na value for money? Je mtu atalipia muda ambao ame reserve parking na kuzuia raia wengine wasitumie hata kama yeyehajapali?
 

Forum statistics

Threads 1,381,904
Members 526,218
Posts 33,814,009
Top