Mkuu ni kweli kabisa kwamba Mitaji ni Tatizo, Ila si kwa kiwango tunacho taka kuaminishwa, wewe kama Entrepreners ni lazima pamoja na mambo mengine uwe na Mbinu za kupata mitaji, na tatizo lina kuwa mitaji kwa sababu tuna penda kufanya biashara kubwa sana kitu ambacho ni ndoto, mtu anataka aingie kwenye biashara na amfikie Mengi au jamaa wa Azam, sio rahisi,
Nchi kama Kenya wapo watu wanoenda hata Kupiga Debe ilimuradi wapate mitaji, wapo wanao enda kufanya vibarua vya kufyeka ilimuradi wapate mitaji, Je, ulisha wahi jaribu hivyo na kukosa mtaji? AU unataka mtaji wa Milioni 100?
Tatizo tunataka kuanzia juu wakati wenzetu wote waliaznia chini na kufika hapo walipo sasa ingawa iliwachuku miaka mingi,
so ni vizuri kuanza na ulicho nacho, na kusonga mbele kwa sababu maswala ya mitaji yatakukuta mbele ya safari na si kusibiri mtaji ndo safari ianze, kwa sababu hata kama kuna sehemu Mikopo au mitaji inatolwe wanao pewa kipaumbele wa kwanza ni ambao tiyali walisha anza na si ambao wana mawazo.
Mashallah naona mawazo mazuri sana humu hata yanipa morali ya kufanya jambo angaa nijipatie rizk ya siku.nataka anza biashara ya kuuza juice na barafu ila jokofu ndio ndogo.