Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Kwa sasa hivi hapa Tz watu wanazidi Kuwa maskini sio kwa sababu ya kukosa business proposals, kwa sababu hata wasomi wa universities wanazagaa mitaani wakiwa hoi kwa umaskini.
 
WanaJF suala la ukosefu wa mtaji ni sensitive sana. Nashauri mtu kama una tatizo la mtaji basi uanze hata kwa kufuga kuku wa kienyeji wachache ambao watakuwa wanaongezeka polepole na kukuwezesha kupata mtaji.
 
Wana JFsuala la ukosefu wa mtaji ni sensitive sana. Nashauri mtu kama una tatizo la mtaji basi uanze hata kwa kufuga kuku wa kienyeji wachache ambao watakuwa wanaongezeka polepole na kukuwezesha kupata mtaji
Duh, kwa sisi tunaoishi katika nyumba za kupanga apo ni ngumu sana.
 
Nilicho gundua Casha ni Aibu na wala sio ukosefu wa mawazo ya biashara.
mi naamini watu wengi wana mawazo mazuri ya kuanzisha biashara bila hata mtaji wa shilingi moja ila shida kubwa ni Aibu kumfikiria mtu atanionaje

Ebu soma historia hii
kuna kijana mmoja alitoka katika familia duni sana kimaisha alikuwa anaishi na bibi yake alikuwa hana mama wala baba wazazi wake walitangulia mbele ya haki akiwa mdogo kwa hiyo alilelewa na bibi yake kwa tabu na masha alisoma mpaka kidato cha nne
alipomaliza shule alihangaika asijue la kufanya mpaka siku moja alipokaa chini na kufikiri kwa undani zaidi nitafanya nini katika maisha yangu magumu kiasi hiki,
wakati akitafakari akatokea mama moja akamuomba akamtupie taka kwani taka zake zilikua zimejaa kwenye viroba alivyohifadhia taka.
kijana alikua hana kiburi bila ya kujivunga akanyanyuka na kwenda kutupa taka aliporudi yule mama akampa 1000 akatokea na mama mwingine akamwambia na mimi naomba ukanimwagie na zakwangu akaenda na yule mama akamlipa pia 1000 kwa jioni ile akawa tayari ana 2000 iliyo muwezesha kupata mlo wa jioni
siku ya pili aliamka asubuhi na kuanza kupita kila nyumba na kuanza kuulizia kama wanahitaji huduma ya kumwagiwa taka cha kushangaza kwa siku nzima alifanikiwa kupata sh.20000 alifurahi sana ingawa majirani walimuongelea ,walimdharau, na wengine walimbadilisha jina kabisa na kumuita mwaga taka hakujali alichojali ni nini anapata na maisha yake anayaendesha vipi,hakujali alijipa moyo na kusema hata wakiniita mwaga taka hawanisaidii shida zangu nazijua mwenyewe
aliendelea na kazi yake ya kupita nyumba hadi nyumba kukusanya taka mpaka akafanikiwa kutengeneza mkoko teni wa kuzolea taka hakuishia hapo akatengeneza mikokoteni mingine zaidi na kuanza kuajiri vijana wenzie ili wamsaidie akaendelea mpaka akafikia kiwango cha kufungua ofisi mtaani kwao ,akanunua magari ya kuzolea taka sasa ni tajiri mkubwa watu hawamwiti tena mzoa taka bali ni bosi mzee mkubwa mkuu ndio majina yake kwa sasa
ana magari ya kisasa kabisa ya kuzolea taka na kuzisaga na kuwa mbolea anauza mbolea na kukusanya taka vyote vinamuingizia hela
nachojaribu kusema ni kwamba watu wengi huzuia malengo yao kwa Aibu ya kumuogopa fulani, utamkuta msichana kamaliza shule ana ujuzi mzuri wa kutengeneza chapati au maandazi na mtaani kwao hakuna vitu hivyo anaogopa kutengeneza kisa aibu
kwa hiyo biashara sio mtaji ni uwezo wa kufikiri tu na kuweka Aibu pembeni
Very correct. aibu uua ndoto nyingi sana, na kikwazo kikubwa kwa kuthibiti.
 
Mwenyewe nilianza na kupakia tofari, kukoroga zege, kupiga tofari, kusaidia fundi. Kimxingi kila Nazi ngumu na nyepex nilikua nafanya. Kipindi hicho nilikua na elimu ya F6. Nilipokea matusi ya kila aina kwani nilio kua nafanya nao hawakuelewa elimu yangu na sikuona umuhimu wa kujitambulisha . nilikua nalaza so chini ya 20000/siku. Saizi nimeajiri kampuni ya ujenzi kunijengea frem 12 mji mdogo huko sumbawanga na najiandaa na kilimo cha hekali 15 na mambo mengine mengi nafanya
Hayo in kwa ufupi tu . NB : "unions umexoma alafu hupati Nazi , jua huna ndoto za kuajiliwa Bali kuajili. Chukua hatua " nitafute kwa uxhauli zaidi.
 
Nami naomba nichangie kidogo...

Mi nafikiri alichoandika mdau Chasha ni cha kweli. Tusianze kulalamikia mitaji kama excuse. Cha msingi ni kuwa na nia thabiti, ambayo kwayo inatoa nguvu kubwa sana. Ukiwa na nia, unaweza kutafuta mtaji through kupiga debe, kufanya vibarua and the like.

Nilijaribu kuongea na rafiki zangu pale Kariakoo, ambao wanauza maji, ambao walinieleza kuwa ukiondoa mtaji, wanaweza kutengeneza ziada ya Tsh. 12,000-13,000, na siku ya biashara mbaya wanatengeneza ziada ya Tsh. 4000 at minimal.

Aidha, wale akina mama wanaouza matunda nao wana make ziada ya kiasi kama hicho,ambapo wao wanachukua matunda kule Temeke Stereo kwa Tsh.50-70 kwa embe moja,lakini kariakoo wanauza kwa Tsh. 250-300, na kwa juhudi zao matunda haya yanaisha.

Niliozungumza nao wananieleza tayari wameshanunua plots (walianza biashara hiyo miaka mi3 iliyopita). Hawa waliongozwa na nia iliyowapa nguvu ya kusonga mbele, japo vipo vikwazo walivyokutana navyo, nawanavyokutana navyo, lakini wanasonga mbele.

Hivyo,nafikiri mtaji mkubwa aliokuwa nao mtu ni mind set,na mtaji mwingine ni kuwa na mahusiano mema na jamii, ambayo kwayo unaweza pata mawazo mengi mazuri, na inawezekana ukaaminika na mtu/watu w/akakupesha mtaji.

Nawasilisha mchango wangu
Mkuu umeongea iliyo kweli kabisa
 
Mimi naweka tu mkazo kwamba mtaji ni wazo na sio pesa nikijitolea mfano mm mwenyewe natama sana kufanya biashara nakumbuka kipindi cha nyuma kabla cjaanza kuzishika pesa nilikuwa nasema nikipata laki moja naanza biashara lakini cha ajabu saivi nashika hadi million tatu mkononi na sina biashara yoyote naishia kusema tatizo ni mtaji nabaki kunywa pombe tu na kubadilisha nyumba za kupanga kila siku kutoka za bei ya chini kwenda juu na kununua furniture kali akati hazinisaidii ila ni kutaka muonekano kwenye jamii...lakini najua ningekuwa na wazo zuri la biashara myb mpaka leo ningeshakuwa millionea....kwaiyo tujipange jamani hizi show off hazina faida...
Kama naona ulivyolewa halafu unaongea....

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Huu uzi hauna maana yoyote mnamjaza ujinga mleta mada tu kwa kuiba vitu google na kuleta humu bila kufanya upembuzi wowote
 
Huu uzi hauna maana yoyote mnamjaza ujinga mleta mada tu kwa kuiba vitu google na kuleta humu bila kufanya upembuzi wowote
Unaumia sana? Hahaa nenda na wewe tafuta ulete humu. Onesha yako ambayo ni halisi basi
 
314 Reactions
Reply
Back
Top Bottom