Baadhi ya misimamo ya watu wenye akili zaidi ya wastani

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,134
2,010
Good Morning people,

Kwanza kabla sijafika mbali napenda niweke bayana mambo yafuatayo.
  • Mosi: binadamu tumetofautiana talanta kutokana na katiba ya miili yetu ilivyoumbwa. Hivyo sio jambo jema kukashifu mwingine kutokana na mapungufu ambayo yapo nje ya uwezo wa asili wa miili yao. Waraka huu sio wa kukashifu uchukuliwe kama dirisha la kuangalia utendaji wa mawazo wa binadamu wenzetu.
  • Pili: mgawanyo wa talanta waweza wekwa bayana Normal Distibution curve, katika jamii yoyote ile, hii curve is very important katika maswala ya takwimu. Hii curve inamwinuko katikati na kusinyaa inapotoka na inapoishia. Ambapo inamaanisha kwamba kushoto kuna udhaifu, wakati katikati inaonyesha wastani wa kiwango na kulia kwake kunaonyesha waliopitiliza. Mfano ukiangalia urufe kutoka jamii mbalimbali utaona kuna mbilikimo, alafu warefu wa wastani ambao wapo wengi na mwisho wanafunga super tall magiant wachache.

Sasa baada ya kusoma point hizo mbili muhimu nakukaribisha kwa moja ya kiungo muhimu kwa binadamu Ubongo, ambao watu wamezidiana kutokana na uwezo wake katika kunyambua taarifa unazopokea kutoka kwenye mifumo ya fahamu. Sasa kuna wale ambao wapo chini ya wastani ( zezeta) , kuna wale ambao wapo kwenye wastani ( mediocre) na kuna wale walio juu ya wastani ( genius),
kutokana na tamaduni nyingi hapa duniani kuweka akili ni kama sehemu ya heshima kwa mtu hivyo inalindwa kwa nguvu zote mtukane matusi mengine ila sio ya kuhusiana na akili patachimbika. Hali ambayo imepelekea kutokuaminika kwa wale ambao akili zipo juu ya wastani, bora maisha ya saa hivi, maana hapo kale wengi waliishiwa kuuwawa kutokana kutokuendana na wanajamii wenzao, kumbuka hili ni kundi la watu ambao wapo wachache wasingeweza kujitetea kutoka kundi ambao wapo wengi ( mediocre)
Kutokana na umakini wa watu hawa wanajikuta wanajua misingi mikuu ya elimu/knowledge ambayo haiwezi badilika, tangia wakiwa wadogo. Misingi
  • Elimu ambayo inakuja na mbongo zetu, Moja: hesabu, huwezi kamwe pata mbili jumlisha mbili iwe tano, MBILI: space and time huwezi fikiri jambo lolote bila kuhusisha space and time ukishaona unaongelea mambo ambayo space and time havipo ujue unaongea moshi na pumba.
  • Elimu ambayo inakuja na experience, kadiri anavyokuwa anaona matendo ambayo ni possible kutokea ambalo anaambiwa hawezi kubali mpaka apate udhibitisho kamili kama kweli latokea.
Kutokana na misingi hapo juu nitaanza kuorodhesha mambo ambayo hayawezi kukubaliwa nitajitahidi kwenda na order kutokana na matukio kama wengi ambavyo tunaamini yalitokea. Nitatoa ufafanuzi kwa baadhi ya mambo mengine SITOJICHOSHA. Na nimepanga kuendelea kudunduliza mambo ambayo watu wenye akili kupita wastani hawawezi kukubali kila pale napopata jambo jipya.
  • Dunia haikuumbwa kwa siku sita. Nani alikuwepo akahesabu?
  • Binadamu hakufinywangwa,
  • Mwanamke hakutoka ubavuni kwa adamu.
  • Nyoka hawezi ongea. Kwa sababu hana koromeo
  • Wanyama wote wasingeweza kutosha kwenye safina. simba na chui walikula nini ndani ya safina?
  • Ukienda juu hukuti mbingu na ukichimba chini hukuti kuzimu. Mnara wa babeli? International space station?
  • Hauwezi ukakaa ndani ya tumbo ya nyangumi ukapona. Au unafikiri tumboni kwa nyangumi kuna miti imeota?
  • Bikira hawezi akazaa pasipo kupata mbegu za kiume. Binadamu lazima awe na mchanganyiko wa mbegu ya mama na ya baba. ambae hana sio binadamu
  • Upepo kutenganisha bahari na watu kuvuka. Nguvu ya upepo isiwapeperushe?
  • Kiumbe mwenye nguvu kusikiliza maombi yetu na kutekeleza. Kwa hio anaupendeleo kwa kila wanaoshinda? Aache mipango aliyokupangia kutokana na uweza wake mkuu akupe unayotaka wewe na uweza wako mfupi?
  • Yesu kufufua watu. Ao waliofufuka wanasemaje huko walikokua??
  • Yesu kutembea juu ya maji. Realy?
  • Yesu kupaa mawinguni. Realy?
  • Binadamu tumezaliwa na dhambi ya kurithi. Realy kosa atende mwingine uadhibiwe mwingine ? ni haki gani ipo hapo?
  • Wadhambi kuchomwa moto milele. Ni adhabu gani hio isiyokuwa na mwisho? Huyu ndo kiumbe mwenye upendo kwa alivyoviumba avicommit milele kwenye mateso? Kwani mwisho ushawahi kufika mpaka watu wawe na experience ya huo moto?
  • Peponi kuwa na furaha na raha. Utajuaje raha pasipo kuonja uchungu?
  • Uwepo wa roho.
  • Kuwepo kwa TRUE LOVE. Or SOUL MATE. Why sikuzote watu walio in same location ndio wanafall in love? Kwa nini mtu ambaye yupo njombe aseme mpenzi wake yupo dar atakuja?
  • Hakuna sisimizi anaweza mtambua binadamu, wala kuongea na wenzake
  • Jua halizami kwenye matope
  • Kuamini asilimia mia idea za kisiasa au kiuchumi. Kutokana na uwezo mkubwa wa kuchambua mada mbalimbali huwezi kuta anasapoti idea moja fully coz kuna makosa lazima atayaona
  • Kusimamisha jua. Kusimama kwa jua hakuzuii usiku n mchana
Nimeanza na hayo kwa sasa ila yapo mengi, kuyatambua tumia misingi niliyoainisha hapo mwanzo. Kama kawaida upuuzi ni jambo ambalo linafungamana na binadamu katika karibia kila age ingawa elimu inatolewa Lakini bado upo na sisi hii hutokana na sababu ambazo zipo nje yetu kama biological being ambao bado tuna evolve.
 
Akili yako chenga sana unajadili mambo makubwa usiyoyaelewa.

Ati dunia haikuumbwa siku sita kisa na Mkasa hakuna aliyekuwa anahesabu siku hizo.

Hivi wewe ukimuona mtoto usiyewahi kumuona. Ni kitu gani kinakufanya umuone anaumri wa kati ya miaka fulani au fulani.

Unajua kwa nini wiki inasiku saba. Na siku inamasaa 24. Na lisaa linadakika sitini. Unajua kama hujui habari za muda hapa utajivua nguo nakuhakikishia.

Hujui siku saba ni utimilifu wa muda katika kiwango cha wiki.

☞ Akili yako umeifunga kwenye mambo madogo.

Wewe unashangaa Yesu kupaa juu lakini haushangai Bombadie au Boeng zikiruka angani. Hilo kwako linawezekana lakini kwa Yesu haliwezekani. Huwashangai kunguru na njiwa wakiruka angani lakini unashangaa Yesu kupaa. Bado unajiona unaakili.

☞ Meli zenye ukubwa tena kubeba mizigo mikubwa zinaelea baharini hushangai. Unashangaa Yesu kutembea juu ya Maji.

☞ Unazungumzia Ati Hawa hakutoka kwenye ubavu wa Adamu. Kipi hakiwezekani. Unajua kama una elimu ndogo hasa ya kidunia ni rahisi kupinga haya mambo. Hivi hujui wapo viumbe ambao hawatumii mfumo wa kawaida kama wanyama wa kawaida.

Lipi lisilowezekana hapo.

☞ Ati mtu kuzaliwa na dhambi ya asili. Sasa wewe ulitaka kusema nini. kwamba watu wasizaliwe na dhambi za asili wakati wazazi wao tayari walikuwa na dhambi.

Simba huzaa simba. Ulitaka wewe mlevi uzae mtu asiye mlevi.

Ndio Maana Yesu alizaliwa kwa kukosa mbegu ya Kibidanamu ambayo ni ya mwanaume ambayo kiasili inadhambi. ilikumuepusha na dhambi ya asili.

☞ Kuhusu Moto wa Milele. Wewe ulitakaje kwa mfano. Ushapewa muongozo kuwa Tenda mema kwako na kwa wenzako. Hapo ulipewa uhuru. Sasa Kama utashindwa kutumia uhuru wako kuchagua kutenda wema. Kwa nini utumie uhuru wa Mungu kukuhukumu atakavyo. Amekupa Option mbili. Wema na ubaya. Naye akajioa option mbili kwenye hukumu. Ukitenda wema atakulipa pepo ya milele yenye furaha. Na ukitenda mabaya atakulipa moto wa milele wenye uchungu.

Yeye hajakuamulia uchague mabaya. Nawe usimchagulie kukuhukumu moto ukitenda mabaya.

Upendo ni uhuru wa kuchagua. Pia upendo upo katika haki. Kama Alikupa uhuru kwa sababu anakupenda. Nawe umpe uhuru wa kukuhukumu kwa sababu unampenda.
Kumbuka yeye ndiye Mungu.

Yaani uwatese wenzako. Uwadhulumu wenzako. uibe wake za watu. Ufanye kila Ovu alafu uje na hoja za kipumbavu ati mbona moto wa milele. Akili zingine kama wehu.

☞ Kuhusu Suala la Mnara wa Babeli. Kwanza ujue kabisa Mnara ule ulijengwa kwa mitazamo ya kizamani kuwa Mungu anaishi mawinguni. Wakati Mungu hanaanapoishi. Mungu yupo mahali popote pale kwa muda wowote. Hii ni kutokana na mtazamo kuwa Mungu na viumbe wake wasioonekana kwa macho ya nyama alidhaniwa anaishi kwenye mbingu yaani huko juu mawinguni.

Ndio maana walijenga mnara wakitaka waende mpaka huko juu wamfikie Mungu. Jambo ambalo lilikuwa ni kama ujuha. Mungu aliwashukia kuwaadhibu kwa kuwaharibia usemi ili watimize amri yake ya kusambaa kwenye dunia. Na hilo lilifanyika. Hii ni kusema kuwa Mnara ulijengwa kwa mtazamo wa watu wenye uelewe mdogo wa Anga. Sio kama Mungu ndiye aliyewaambia Wajenge kumfikia.

Kama Mungu ndiye angewaambia basi hoja yako ingekuwa na mashiko. Kuwa iweje wajenge mpaka mbinguni ilhali mbinguni hapaonekani. Mbinguni ni wapi ilhali anga halina mwisho(infinity). Lakini kwa vile lilikuwa wazo la wapumbavu ndio maana walijenga ili wamfikie Mungu.

☞ Unasema Nyoka hawezi kuongea. Upo sahihi kabisa. Lakini hajafikri kwa upeo mkubwa. Siku hizi mpaka Radio zinaongea. Simu zinasema. Maroboti yasiyoviumbe yanaongea. Labda nikuambie kuwa Nyoka hawezi kuongea kwa sababu ala zake za sauti kama vile mdomo, ulimi, meno, ufizi, kaa kaa gumu na laini pamoja na Koromeo havimsapoti kuongea.

Lakini vipi kama akiingiliwa na kiumbe kingine ndani yake kikaongea badala yake. Hujawahi ona Watu wanaoanguka mapepo au wenye maruhani. Unakuta ni mwanamke lakini akiingiliwa na mapepo anaongea sauti nzito ya kiume tena besi ya kutosha.

Sio nyoka tuu aliyewahi kuongea kwa mujibu wa Biblia. Yupo pia Farasi wa Balaki kama sijakosea aliongea. Na aliongea kwa sababu maalumu.

Nikukumbushe tuu kuwa kisichowezekana kwako usifikiri kwa wengine hakiwezekani achalia mbali Mungu.

Hapo ni ishu ya setting na kuingiliwa tuu.

☞ Binadamu hakufinyangwa. Hujatuambia akifanywa nini.
Unajadili mambo yaliyokuzidi uwezo alafu unajiona unaakili kubwa.

Kwa kawaida Mpumbavu hujiona anaakili.

Kwa akili yako ndogo ambayo nina uhakika hata shule imekushinda hasa masomo ya Sayansi. Sijui unawezaje jadili Mambo ya Falsafa ambayo ni makubwa kuliko Sayansi.

Nakushauri; Unapojadili mambo haya cha kwanza fikiria mtoto wako siku akisoma atakuchukulia kuwa baba yake alikuwa na akili au Mpumbavu.

Hauwezekani mtu ashangae Mtu kutembea juu ya maji ilhali anaona Meli kubwa zikipita juu ya Bahari.

Kingine kapande ndege hata ya kutoka Dsm to Mwanza alafu utaona kama inawezekana Yesu kupaa angani au vipi.

Kumbuka. Elimu zipo nyingi. Ipo elimu ya kibinadamu, elimu za wanyama, elimu za viumbe wasioonekana.

Ni sawa na ng'ombe kubisha kuwa haiwezakani kutembea na miguu miwili kisa yeye anatembea na miguu minne.

Kila elimu inatokana na Matakwa na mahitaji ya kiumbe husika.

Unajadili mambo kama mtoto mdogo. Yaani ni kama Samaki ajadili na samaki wenzake kuwa hakuna maisha nje ya maji wakati kuna zaidi ya mamilioni ya wanyama wanaishi nchi kavu.

☞Uwepo wa roho. Hapa sijui ulikuwa unataka usemeje. Lakini kama ulikuwa unakataa basi utakuwa umechanganyikiwa.

☞ Ati utajuaje utamu bila uchungu. Yaani kuna watu mnaakili kama wendawazimu maana hata mtoto mdogo hawezi fikiri kwa namna hiyo.
Kama ungejua Setting kwenye technolojia wala usingeongea huo upuuzi.

Mwili wako umesettiwa kwa muda huu kuhisi vitu kinzani. Yaani vitamu na vichungu. Vizuri na vibaya. Lakini Mungu kabla ya uasi wa Adamu aliuseti mwili wa binadamu one way side. Yaani kujua upande mmoja wa wema tuu. Kisha kwenye lile tunda alilowaambia wasile ndio akaweka two way side yaani wema na ubaya.

Nataka kusema nini. Mtu anaweza kuwekewa Setting ya kuhisi raha tuu pasipo kuhisi huzuni. Kuhisi utamu tuu pasipo kuhisi Uchungu.

Hivyo sikulaumu kwa maana uelewa wako ndivyo ulipofikia kwa habari kama hizo. Akili yako inajadili mambo usiyoyaweza.

Sio kila kiumbe kina two way side. Vipo vyenye One way na vingine mpaka three way side.

Ni sawa na Milango ya ufahamu. Binadamu kaumbwa na milango mitano ya kawaida ya fahamu. Wapo viumbe wanamilango chini ya hapo na wapo wenye zaidi ya hapo. Sasa wewe kwa akili yako ndogo unaweza kuja na akili yako ndogo ukasema kuwa haiwezekana kiumbe kisiwe na milango mitano mitano wakati vipo viumbe na watu wenye milango chini ya hapo au zaidi ya hapo.


●Hatimaye, nikupongeze hata hivyo kwa kujitahidi walau kuonyesha uelewa wako mdogo ili upate msaada. Bila shaka utakuwa umesaidika.
 
Mtoa mada amesema kwamba ukisikia mtu anaongelea habari zisizo katika space and time ni pumba.

Katika Physics inawezekana kwa ulimwengu wenye space bila time kuwepo, au wenye dimension moja ya space na tatu za time (tofauti na wetu wenye dimension moja ya time na tatu za space), au usio na space wala time kuwepo.

In fact kuna argument kwamba hata ulimwengu huu kimsingi hauna space wala time, una transformational processes tu.

 
Mbona umedili Sana na Mambo ya dini..? Inamaana yenyewe ni fikra zilizo chini ya wastani au ndo wastani wenyewe..?
Mwanzoni umeanza vyema ila ulipo haribu ni kudili na hao wa dini!!! Kwani huwezi kueleza fikra za juu pasipo kutumia dini..?
Fikra za juu huleta majibu dhahiri kwa yale maswali magumu,fikra za juu huathiriwa na asili kuliko kusadikika na ndio maana nadharia za kusadikika huwa hawazihusudu! Hayo ni maoni yangu.
 
Jokajeusi,
Daah ubishi na ujinga wako una bahati kwelikweli MOD waliamua kuuficha huu uzi kwangu.
Ila embu tumia akili yote uliyojaliwa mtu na unyayo kutembea juu ya maji , unaonekana mtalam embu niambie unyayo uliloana au haukuloana .

Alafu uache tabia ya kumsemea mungu sidhani kama amewahi kuongea na wewe
 
Kiranga,
Yeah kuna vitu vingi vya kufikirika kwenye physics lakini kwa kuwa sisi binadamu tuna experience ya three dimension space na time tu . Tukiongelea hivyo vingine ni kujifurahisha kwa sababu havina maana kwetu, hatuwezi pata maana ya kueleweka kutoka hivyo vitu.
 
KENZY,
Kwasababu ndio mara nyingi binadamu anavunja mipaka yake ya kufikiri kwenye mambo ya dini
 
Yeah kuna vitu vingi vya kufikirika kwenye physics lakini kwa kuwa sisi binadamu tuna experience ya three dimension space na time tu . Tukiongelea hivyo vingine ni kujifurahisha kwa sababu havina maana kwetu, hatuwezi pata maana ya kueleweka kutoka hivyo vitu.
Unajuaje havina maana?

Unaelewa kwamba hesabu zinazotumika kutuonesha hivyo vitu ndizo hizo hizo zinatupa vitu kama GPS na internet?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajuaje havina maana?

Unaelewa kwamba hesabu zinazotumika kutuonesha hivyo vitu ndizo hizo hizo zinatupa vitu kama GPS na internet?

Sent using Jamii Forums mobile app
mathematics kama yenyewe ipo original haibadiliki kamwe ila sasa mafafanuo yake katika dunia yetu ndo shida zinapoanza

mambo kama four dimensions being au being before time they cant make any sense kwetu. Chukulia four dimensions hakuna binadamu ambaye anaweza ona hizo dimensions zimekaaje
 
Back
Top Bottom