Baadhi ya miradi mikubwa hapa nchini inatokana na mawazo na mahitaji ya watanzani wenyewe au ni watu kutoka nje?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,993
144,329
Mimi sometimes huwa najiuliza hivi baadhi ya miradi mikubwa hapa nchini huibuliwa na watanzania wenyewe kwa kuamini wanaihitaji au ni mawazo ya watu kutoka nje ya nchi ili baadae waje wapate tender na kisha wavune hela kutoka kwetu?

Haiwezeni watu hawa wakawa wanawatumia hata baadhi ya watanzania wenzetu kupenyeza mawazo haya serikalini?

Kwa mfano,tatizo la foleni Dar-es-Salaam ni kutokana na kutokuwepo kwa fly overs au ni ukosefu wa barabara nzuri za kuunganisha Manispaa za Jiji sambamba na highway zilizopo?

Je,si kuwa tulikosea ku-plan huu mji au wataalamu waliofanya hiyo kazi hawakuona mbali?


Hivi hata tatizo la mafuriko katika miji yetu ikiwemo Dar,ni kwasababu ya mnvua nyingi au ni ubovu tu wa miundombinu pamoja na kukosekana kabisa kwa miundombinu katika baadhi ya maeneo ya kusafirisha maji ya mnvua?

Huwa tunafanya utafiti wa kutosha na kujiridhisha kuwa kwa sasa tunahitaji aina fulani ya mradi?

Nikiomba nakala ya utafiti wa uhitaji wa baadhi ya miradi naweza kupewa?

Kwenye nchi za wenzetu huwa tunakwenda tu kutalii na hatujifunzi lolote?

Ni kweli tumekosa exposure au sometimes ni ushamba tu unatusumbua?
 
Na bado safari za nje kila Siku kwenda kujifunza!!!
Unavyodhani Mkuu ununuzi wa ndege ni matakwa ya wa tz!?? Au ujenzi wa kiwanja cha ndege Chato!???? Bado RAIA akihoji unapewa jibu mubashara (unawashwa washwa)

Sera zetu zimekaa upande wa kushoto
 
Ndo hayo mkijiwekea akiba ya baadae kwa miundombinu ya barabara baadae mnakuja jenga
Sehemu za mabonde msijenge ndo kwanza mnagaiana viwanja
Vyote vya akiba vilisha tumiwa sasa vinahitajika yanaletwa maelezo kama haya
 
Hata ile miradi mipya kama ofisi za Mabasi ya mwendokasi kujengwa kwenye mkondo wa maji jangwani nayo ni ushauri kutoka nje ?
 
Back
Top Bottom