Kwa mujibu wa mdau mmoja, Disemba 12, 2019 aliona kwenye taarifa ya habari ya chombo kimoja wakitangaza kuwa familia moja imepoteza watoto wao wanne kwa kile kinachodaiwa kuwa walikula mihogo yenye sumu.
Aidha, mada hii imekuwa inazungumzwa sana mitaani, huku ikiacha mashaka makubwa kwa kuwa mihogo ni chakula kinachotumika kwa kiasi kikubwa, kama kingekuwa na sumu basi watu wengi wangekuwa wamepoteza maisha.
Tuelewe nini kuhusu madai haya? Ni kweli kuwa mihogo huwa na sumu, au ni uzushi tu unaopaswa kupuuzwa?
Aidha, mada hii imekuwa inazungumzwa sana mitaani, huku ikiacha mashaka makubwa kwa kuwa mihogo ni chakula kinachotumika kwa kiasi kikubwa, kama kingekuwa na sumu basi watu wengi wangekuwa wamepoteza maisha.
Tuelewe nini kuhusu madai haya? Ni kweli kuwa mihogo huwa na sumu, au ni uzushi tu unaopaswa kupuuzwa?
- Tunachokijua
- Mhogo ni mzizi wenye nishati nyingi ambao kwenye mgawanyiko wa makundi ya viumbe hai na mimea huwekwa kwenye familia ya Euphorbiaceae. Kitaalam huitwa Manihot esculenta.
Vyanzo vya kihistoria vinataja asili ya mhogo kuwa ni bara la America ya kusini, kwa sasa mmea huu hupatikana kwenye zaidi ya nchi 80 duniani.
Kwa mujibu wa USDA, mhogo huwa na wanga, protini, vitamini C, aina mbalimbali za madini muhimu kwa afya, viondoa sumu na folate hivyo ni chakula chenye manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.
Kuhusu sumu
Mihogo michanga (ambayo haijakomaa vizuri), michungu pamoja na ile isiyopikwa (mibichi) huwa na kemikali sumu za Cyanide.
Wingi wa kemikali hizi hutegemea na aina husika ya mhogo pamoja na sehemu ilipolimwa, hivyo kwa kiasi kikubwa aina nyingi ya mihogo tunayotumia kila siku huwa na kiwango kidogo sana cha kemikali hizi kisichoweza kuleta madhara kwa afya ya mlaji.
Katika mazingira machache, baadhi ya mihogo inaweza kuwa na kiwango kikubwa cha kemikali hii kinachoweza kuleta madhara kwa afya. Ulaji wa sumu hii huambatana na dalili zifuatazo-
- Uchovu mkubwa na kuweweseka
- Kiungulia
- Maumivu makali ya kichwa
- Maumivu ya kifua na kushindwa kupumua
- Kifafa na kupoteza fahamu
- Shinikizo la chini la damu
- Shambulio la moyo na kifo
Ukubwa wa dalili na athari za sumu hii hutegemea wingi wa dozi iliyotumika, aina ya cyanide iliyohusika kwa wakati huo pamoja na kiasi cha muda aliotumia mhusika kwenye kuikusanya sumu hii mwilini mwake.
Ushauri
Ni muhimu kuweka mkazo kuwa siyo kila mhogo huwa na sumu hii, pia ile ambayo huwa nayo huwa ipo kwenye kiwango himilivu kwa mwili.
Hata hivyo, hii haitoi tafsiri kuwa hakuna kabisa mihogo yenye kiwango kikubwa cha cyanide kinachoweza kuua, au kuleta madhara mengine makubwa kwa afya.
Hivyo basi kwa kuzingatia hali hizi zote tatu, ni muhimu kufanya mambo yafuatayo-
- Epuka ulaji wa mihogo mibichi hasa ile yenye ladha ya uchungu
- Loweka mihogo kwenye maji kabla hujaipika
- Kabla ya kutengeneza unga wake inapaswa kumenywa, kulowekwa na kukaushwa vizuri