Baadhi ya Mawaziri katika serikali ya Rais Magufuli wameanzisha mgomo wa kimyakimya?

s
Habari za muda huu.

Ni muda sasa nimekua nikifuatilia utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya 5 na kiukweli nimejiridhisha kwamba baadhi ya mawaziri hawako "active" kama uongozi wa juu wa nchi unavyotaka. Hili limethibitishwa na Mkuu wa nchi Mh. Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli wakati anaongea na baraza la biashara la Taifa kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Ni kama wameamua kunyamaza au "kumsusia" kazi zote Rais na Waziri Mkuu. Hili jambo si la afya njema katika uendeshaji wa Serikali na taasisi zake. Nitoe wito na kumshauri Mh. Rais ni muda mufaka sasa wa kufanya mabadiliko makubwa katika Baraza lako la Mawaziri kwa ustawi wa serikali unayoiongoza.

Ahsante na nakutakia kazi njema!
shida ni yeye alivyoanza kuingilia kila wizara na kubeba majukumu yote. Mawaziri waliingia uoga na mpk sasa iko hivyohivyo
 
Ni ujinga wa hali ya juu Kwa Tizeba ambaye ni waziri wa Kilimo ambayo ndiyo Engine ya Viwanda na Biashara au Mpina waziri wa mifugo ambayo ni mingi mno imatafuta soko kushindwa kushiriki kikao kama kile. Nadhani wasomi wa Tanzania wanasoma kupata Vyeti
Je kama wana sababu za msingi za kutohudhuria??

Je kulikua hamna wawakilishi wengine wa Wizara?
 
Nimeona analalamika sasa alitaka wafanyeje hakawii kukuambia utoe data kichwani usipotoa anakutumbua hazalani, sasa nani anataka kuzalilishwa namna hiyo, yeye amezoea kupika data sasa anataka wenzake wafanye kama yeye.

Nape alifanya kazi nzuri sana matokea yake akatumbuliwa, naona walichofanya ni kumwachia ngoma aicheze yeye na mwanawe bashite,
 
Je kama wana sababu za msingi za kutohudhuria??

Je kulikua hamna wawakilishi wengine wa Wizara?
Mahali pa kuwaonyesha na kutangaza Fursa waziri anakua busy? huo ni Upumbavu sasa, fursa kama hiyo ataipata wapi tena?
Kero za Biashara ktk sekta zao nani anajibu?
 
Badala ya kumshauri rais ajitafakari na kujipima utendaji wake wa kazi unamshauri afanye mabadiliko makubwa ya mawaziri ili akuteuwe wewe!!! Unazani kuhudhuria kikao ni kukubaliana nae? Wapimwe kwa utendaji wao wa kazi sio kuhudhuria vikao.
 
Ni ujinga wa hali ya juu Kwa Tizeba ambaye ni waziri wa Kilimo ambayo ndiyo Engine ya Viwanda na Biashara au Mpina waziri wa mifugo ambayo ni mingi mno imatafuta soko kushindwa kushiriki kikao kama kile. Nadhani wasomi wa Tanzania wanasoma kupata Vyeti
Engine ya viwanda? Mbona hilo halijidhiirishi kwenye bajeti ya serikali? Tokea mwaka 2003 (Maputo Declaration) serikali za CCM zimeshindwa kutenga 10% ya bajeti kwenye kilimo, kama Azimio lilivyoagiza. Mwaka huu bajeti na disbursement ni aibu, huku bilioni 500 zikitengwa kununua ndege!!
 
Mahali pa kazi kama una boss asiyependa kushauriana na wafanyakazi walio chini yake lazima kuna maeneo hayatafanya vizuri, kwani wasimamizi wake watafanya kazi kwa uoga.
 
Engine ya viwanda? Mbona hilo halijidhiirishi kwenye bajeti ya serikali? Tokea mwaka 2003 (Maputo Declaration) serikali za CCM zimeshindwa kutenga 10% ya bajeti kwenye kilimo, kama Azimio lilivyoagiza. Mwaka huu bajeti na disbursement ni aibu, huku bilioni 500 zikitengwa kununua ndege!!
Kwa hiyo hiyo ni sawa kwao kutohudhuria hicho kikao Kwa sababu bajeti haipangwi ya kutosha?
 
nadhani wa kubadilisha utendaji ni hao walioteuliwa kama unaona huwezi basi unajiuzulu. Kiongozi ndio mwenye dira ya tunakokwenda. ingekuwa busara sana kama wangejiuzulu
Huyu anataka akufukuze sio kujiuzulu maana hilo anaona kama umemdharau na lazima akuonyeshe cha mtema kuni kwa kukufatilia
 
mambo ya ajabu kabisa. wapo wengi tu siwaoni siku hizi jenista mhagama januari makamba n.k
Mkuu kwa January hapo kuna utata fulani.
Jinsi alivyo wasimamisha wale wafanyakazi wakarudishwa ni kama walimshusha na kumdhalilisha walio juu.

Japo January alikuwa kimya sana hata kabla sakata lile. Hakuwa na kasi.
 
Ni ujinga wa hali ya juu Kwa Tizeba ambaye ni waziri wa Kilimo ambayo ndiyo Engine ya Viwanda na Biashara au Mpina waziri wa mifugo ambayo ni mingi mno imatafuta soko kushindwa kushiriki kikao kama kile. Nadhani wasomi wa Tanzania wanasoma kupata Vyeti
Mpina amesoma nini KILAZA tu
 
Mahali pa kuwaonyesha na kutangaza Fursa waziri anakua busy? huo ni Upumbavu sasa, fursa kama hiyo ataipata wapi tena?
Kero za Biashara ktk sekta zao nani anajibu?
Ukiona mtu kama yule Luhanga Mpina yupo "busy" kwa John Pombe ujue kuna tatizo mana yule ni mmoja kati ya mawaziri waliokua na viherehere sana kutoka hadi alivokua naibu waziri mpaka akapandishwa cheo...

Sasa ukiona wale viherehere wote wana mgomo baridi ujue John Pombe mwenyewe ndo tatizo watakua wamemchoka
 
Back
Top Bottom