Baadhi Ya Matangazo Yanawazalilisha Wanawake!!

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,685
22,694
Habari wana-MMU!!

Kutokana na tatizo la FISTULA kushika kasi hapa nchini mwetu kuna wadau mbalimbali wamejitokeza wakitambulika kama mabalozi wa FISTULA huku wakiwaamasisha wanawake mara waonapo dalili za tatizo hili waripoti katika vituo husika vilivyopendekezwa kwa ajili ya kutoa huduma ya tatizo hili,.


Tatizo linakuja hapa kwenye namna wanavyohamasisha wahanga wa tatizo hili,.

Kuna mwanamke anasikika akimsema mwanamke mwenzake aliyepatwa na tatizo hili eti ''amelowa kama kuku mwenye kideri''


Kwa kweli tunatambua kuwa lengo lenu ni zuri ambalo linapaswa kuungwa mkono na kila mtu mwenye kujali ila Jaribuni kubadilisha maudhui ya tangazo lenu lililobeba maudhui ya udhalilishaji dhidi ya wanawake!!
 
hiyo sentensi kwenye blue manake nini

mkuu ulishawahi kulisikia hili tangazo?

Kideri ni ugonjwa unaowakumbuka kuku na dalili zake ni kuku kupoteza nguvu na kujiharishia hovyohovyo bila kikomo!!

Hope umenielewa!!
 
mbona wabunge bungeni wanaongea kauli mbovu mpaka unahisi tv ita stuck..

Ndo nchi ilipofika.. Kuropokaropoka tu.. hovyohovyo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom