Baadhi ya Mambo makubwa mazuri Rais Magufuli aliyowafanyia Wananchi wa kawaida

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
Wapiga kura wengi ni watu wa kawaida wanyonge sio wakaa maeneo ya uzunguni, katikati ya miji na maeneo ya wenye nazo na wenye mavyeo

Rais Magufuli toka ashike strategy yake imekuwa kupeleka maendeleo kwa wapiga kura watu wa kawaida walio wengi

Baadhi ya Makubwa aliyowafanyia watu wa kawaida Ni haya

Mosi, Elimu bure kwa watoto wa watu wa kawaida kutoka msingi Hadi secondary

Pili, barabara nzuri kwenye maeneo ya watu wa kawaida mijini na vijijini.Mibarabara mizuri haikuweko mitaani uswahilini.Sasa hivi mitaa mingi uswahilini Ina barabara za uhakika Hadi taa za barabarani mfano Ni uswahilini dar es salaam

Tatu, vituo vya afya vyenye majengo ya uhakika na huduma za hali juu na upatikanaji wa madawa

Nne, Ni miradi ya maii ya uhakika kila mkoa.

Tano, upatikanaji kirahisi na uhakika wa huduma ya umeme mijini na vijijini usiokatika katika

Sita, uwajibikaji wa watendaji was seikali kwa watu wa kawaida. Kabla Wafanyakazi Serikalini walikuwa wakijiona miungu watu kuhudumia mtu wa kawaida walikuwa na nyodo Sasa hivi hamna nyodo mtu hata aende na suruali imekatika matakoni kea umaskini akienda ofisi ya serikali anahudumiwa Kama mfalme

Saba, kutoweka lockdown kwa sababu ya Corona Kama nchi zingine ili wananchi wapate rikizi zao na kugundua dawa ya kujifukiza kuwanusuru

Haya ni baadhi yako mengi.

Rais Magufuli apewe kura zote kipindi chake Cha pili
 
Hivi hizi lugha za kejeli mnazitoa wapi, watu mnawaitaje "Wananchi wa Kawaida" CCM huwa humo kwenye ubongo wenu mna nini?

Kwa hiyo hiyo hao wasio wa kawaida ni akina nani na wamefanyiwa nini? Na hao wasio wa kawaida ni akina nani na wamefanyiwa nini ambacho kinasema hiki ni cha wananchi wa kawaida?

Kama wananchi wa kawaida ni pamoja na wakulima, hivi kuwadhulumu wakulima wa korosho ndilo hasa stahiki yao hao unaowasema wananchi wa kawaida?

Tuje kwa watumishi ambao pia wanaweza kuwa wananchi wa kawaida, kula hela za wastaafu ni stahiki yao au kutowapandishia mishahara yao ndio hio stahiki yao?

Kuajiri watu kwa minajiri ya kuwa mwanachama wa CCM ndio hiyo stahiki yao hao wa kawaida? Hii Serikali inaongoza kwa kuajiri watendaji wa kata ambao ni makada wa CCM.
 
Hivi na sisi tunaodai chetu mifuko ya hifadhi ya jamii ni kundi la watu wa kawaida au tuko kundi la watu wa ajabu?
 
Wafanyakazi wa Umma (Hakuna nyongeza ya mshahara,kudhulumiwa/ kucheleweshewa mafao) eti ghafla nao wamegeuka kua sio wananchi wa kawaida.

Wanafunzi waliomaliza vyuo vikuu tangu 2015-2020 pia nao wamegeuka ghafla na kuingia kwny kundi la Wananchi wasio wa kawaida.
 
Magufuli ni mkombozi wa taifa yupo vizuri sana, Mungu ni mwema sana atamtunza
 
Nane: kugawa maburungutu ya hela za wananchi hadharani huku zikiitwa hela za jei pi em
 
Jambo jingine zuri alilofanya ni kuchukua fedha zote toka kwenye mifuko ya jamii huku wastaafu wakikaa bila mafao kwa miaka mitatu hadi minne.
 
Back
Top Bottom