Baadhi ya mambo 10 yanayoijenga taswira ya siku 365 za Rais Samia madarakani

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Na Mwl Udadis

Mwenye macho haambiwi tazama. Kazi iliyofanywa na Rais Samia katika kipindi hiki cha mwaka mmoja ni ishara ya uwezo mkubwa wa kiuongozi. Tuangazie baadhi ya mambo yanayojenga taswira ya uongozi huu;

1. Kuimarisha uhusiano wa kimataifa na utekelezaji wa sera ya diplomasia ya uchumi. Hii ni moja ya sekta muhimu sana iliyotendewa haki na uongozi wa awamu ya sita katika kipindi kifupi.

2. Kuimarisha umoja wa kitaifa na misingi ya siasa safi inayofuata taratibu na sheria ya vyama vya siasa.

3. Kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji na kwa wafanyabiashara ndani na nje ya nchi. Hivi karibuni kupitia Dubai Expo tumeshuhudia Makubaliano ya uwekezaji wenye thamani ya USD Bilioni 7.49 ikitarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 200,000.

4. Kuzipa nguvu taasisi zote ikiwemo za kifedha na sekta binafsi kwa ujumla kama wadau muhimu katika uchumi wa nchi.

5. Kuimarisha Uchumi kwa kutekeleza mipango ya muda mfupi na muda mrefu inayotoa majibu kwa changamoto zinazowagusa wananchi.

6. Kuimarisha Taasisi za utoaji haki ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uhuru wa vyombo vya sheria ikiwemo muhimili wa Mahakama.

7. Kutoa vibali vya ajira kwa Taasisi mbalimbali za serikali, kulipa malimbikizo na madeni ya watumishi wa umma. Pia, kupandisha watumishi madaraja kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma.

8. Kuimarisha huduma za jamii kama vile Elimu, Afya, Maji, miundombinu n.k. Kwa mara ya kwanza katika historia wanafunzi wote 907,803 waliopaswa kuanza masomo Kidato cha kwanza walipata nafasi ya kuanza masomo kwa wakati kutokana na ujenzi wa madarasa 15,000.

9. Kutekeleza miradi ya kimkakati yenye kulenga kustawisha uchumi wa nchi yetu kwa muda mrefu ujao.

10. Kutambua juhudi za wabunifu na Kutekeleza mipango ya makusudi itakayo wezesha Tanzania kunufaika na mapinduzi ya 4 ya viwanda.

Watanzania Tumekubali Kaziinafanyika
 
Unatafuta teuzi nin.... Ingia mitaani uangalie tra na almashauri wanavyovimba na kuonea raia... Kila.mtu ana ndevu.

Fair hazipo, vitu vinapanda, miradi endelevu ipo slow na usimamiz mbovu, waovu hawachukuliwi hatua... Magumash mengi.

Majaliwa kafikia wap ile ripoti ya mauaji police
 
Back
Top Bottom