Baadhi ya Majeruhi Bado Wana Risasi Mwilini na Mwanamke Apoteza Mimba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baadhi ya Majeruhi Bado Wana Risasi Mwilini na Mwanamke Apoteza Mimba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by niweze, Jan 8, 2011.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari Kutoka Hospitali ya Mount Meru Arusha ni Kwamba Baadhi ya Waliojeruhiwa Bado Wana Risasi Mwilini na Wamepewa Dawa za Kutulliza Maumivu. Mwanamke Mmoja Amepoteza Mimba kwa Kupigwa na Mishtuko ya Kupigwa Risasi. Haya Ndio Matokeo ya Uchaguzi wa CCM - Uraisi na Umeya Arusha. Kitu cha Ajabu ni Kwamba Hawa Wananchi Wanasubiri Huduma Mahospotalini Lakini Viongozi wa CCM Wao Wanacheka na Kuendelea na Mipango ya Kulipa Dowans Haraka Haraka. Hizo Pesa Zinazotumika Kulipa "mikatab Hewa Si Zingesaidia Huduma za Walioumia?" Ooo Hii Ni Ngumu Kuelewa CCM. Wananchi Sijui Ushahidi Mwingine wa Aina Gani Tuonyeshwe Kwamba CCM Sio Binadamu. Ushahuri Tunautoa kwa Chadema, Tunawasii Kukaa Mbali na CCM na Kutojadiliana Chochote Mpaka Watoke Ikulu, Viti vya Ubunge na Vit vya Meya Mikoani.

  CHADEMA yagomea mazungumzo na CCM

  "Uhuru na Amani ya Tanzania ni Fake. Katiba Mpya Ndio Foundation ya Taifa Letu"

  Soma Hapa Chini. JK na CCM Wameuwa Tena Shinyanga. CCM Endeleeni Kutupiga Risasi na Iko Siku Zitarudi Usoni Kwenu.

  Polisi yaua raia Shinyanga, wananchi waja juu

  na Stella Ibengwe, Shinyanga. Tanzania Daima.

  WANANCHI wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wamefanya maandamano hadi ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kulaani kitendo cha askari polisi kumuua raia mmoja kwa kukutumia risasi. Mbali na hilo wananchi hao pia waliandamana kupinga baadhi ya askari kuwabambikiza kesi wananchi.
  Tukio la kuuawa kwa raia huyo lilitokea wakati polisi walipowavamia baadhi ya vijana waliokuwa wakinywa pombe katika eneo la mnada wa Mhunze Desemba 16, mwaka jana. Wananchi hao waliandamana wakiwa wamebeba mabango yaliyotoa ujumbe kwa serikali, wakiitaka ichunguze tukio hilo kwa umakini na kusikiliza kilio cha wananchi hao na kudai kuwa wao hawana hatia.Kufuatia tuko hilo wananchi hao wameiomba serikali kuwachukulia hatua askari waliohusika na uonevu huo sanjari na kukomesha unyanyasaji kwa raia na kuongeza kuwa hali hiyo inawatisha wananchi kushirikiana na polisi katika kukabiliana na uhalifu.Akizungumzia hilo Diwani wa Kata ya Kishapu Daudi Matungwa alikiri kutokea kwa tukio hilo lililosababisha mmoja wa wananchi hao aliyejulikana kwa jina la Luhende kupoteza maisha baada kupigwa risasi na polisi siku chache zilizopita. Alisema kabla ya kifo chake, alipelekwa hospitali ya rufaa Bugando Mwanza na alifariki Desemba 19, mwaka jana. Kufuatia kifo cha raia huyo diwani huyo alisema wananchi wa kijiji hicho baada ya kupewa taarifa ya kifo cha mwananchi mwenzao waliamua kususia mazishi hadi pale ambapo serikali ingetoa muafaka wa tatizo hilo ambapo baadaye mwili huo ulizikwa. Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga, Hussein Kashindye, alipoulizwa alikiri kupokea taarifa hizo na kwamba ofisi yake inayafanyia kazi.Naye mkuu wa wilaya ya Kishapu Abudullah Lutavi alithibitisha kupokea maandamano ya wananchi na aliwaasa kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu sio lazima risasi zitolewe,watu wa afya hawawezi kuacha kuwahudumia wanaharakati kwa sababu hata wao wanataka Change.
   
Loading...