Baadhi ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
Baadhi ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne.

Ukiacha Idara za Utawala, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inaundwa na Idara kuu tano ambazo ni Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Idara ya Huduma kwa Jamii. Pia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.

Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, kuhifadhi na kuwarekebisha wafungwa, kutoa huduma za zimamoto na uokoaji, kudhibiti uingiaji na utokaji nchini kwa raia na wageni, kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Huduma kwa Jamii na kuandaa na kutoa Vitambulisho vya Taifa.
Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne, Wizara hii imefanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuiwezesha nchi yetu kuwa na amani na utulivu. Kwa wastani tunaweza kusema kuwa nchi yetu imekuwa na usalama ambao umewawezesha wananchi na wageni kuendelea kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi, licha ya matukio ya hapa na pale.

Wizara ya mambo ya ndani, kwa kupitia Jeshi la Polisi, imeweza kudhibiti vitendo vya uhalifu vilivyokuwa vimeanza kukithiri hapa nchini. Vitendo hivyo ni pamoja na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha, wizi katika mabenki, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, yaani albino na makosa mengine ya kijinai. Ingawa kutokea changamoto nyingine hivi karibu amabapo kuna wahalifu wameanza kuteka siraha katika vituo vya polisi na kuuwa askari.

Kwa mfano, kwa juhudi zilizofanywa na Jeshi la polisi, makosa ya kuwania mali (unyang'anyi wa kutumia silaha, wizi katika mabenki, uvunjaji, wizi wa mifugo n.k) yalipungua kutoka 53,268 mwaka 2005 hadi 45,470 mwaka 2013. Mengine yaliyopungua ni mauaji ya albino kutoka 20 mwaka 2008 hadi moja mwaka 2013. Watuhumiwa waliohusika katika matukio haya walikamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Kwa ujumla kutokana na juhudi zinazofanywa na Wizara, makosa makubwa ya jinai yamekuwa yakipungua kwa wastani wa asilimia sita (6) kila mwaka.

Katika juhudi za kuongeza nguvu kazi, idadi ya askari na askari wanafunzi katika Jeshi la Polisi imeongezwa kutoka 26,000 mwaka 2006/2007 hadi 44,000 kufikia Desemba, 2013.

Nyumba mpya 491 kwa ajili ya askari Polisi zimejengwa kote nchini yakiwemo maghorofa 84 yaliyojengwa Dar es Salaam, matatu Zanzibar na mengine matatu, Pemba. Pamoja na kuendelea na ujenzi katika maeneo mengine nchini, Jeshi la Polisi lilisaini makubaliano ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 350 za kuishi askari katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni . Aidha kwa msaada wa Serikali ya Marekani, Chuo cha Polisi Wanamaji kimejengwa mjini Mwanza.

Kwa upande wa vitendea kazi, magari mapya 373 na pikipiki 1,128 zimenunuliwa. Boti 10, magari 97 na pikipiki 484 zimepatikana kutoka kwa wafadhili na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuimarisha operesheni za Jeshi la Polisi.

Jeshi la Magereza:
Katika kuimarisha shughuli za utunzaji na urekebishaji wafungwa, Wizara kupitia Jeshi la Magereza imefanikiwa kukarabati majengo na miundombinu ya magereza, likiwemo Gereza lenye ulinzi mkali la Butimba, na ukarabati wa majengo mengine ya ofisi za Utawala umefanyika katika magereza ya Uyui, Lilungu, Maweni, Isanga, Keko na Ukonga. Ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa mabweni ya wafungwa umefanywa katika magereza 24 nchini kwa lengo la kuhakikisha kuwa usalama wa wafungwa unaimarishwa.

Aidha, ujenzi wa jengo la ghorofa la kuishi familia 16 za askari katika Gereza la Mahabusu Iringa umekamilika. Ujenzi wa nyumba za maofisa na askari unaendelea katika magereza 17 nchini. Pia nyumba nne (4) pamoja majengo na mengine matatu (3) yamenunuliwa kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) wilayani Lushoto mkoani Tanga kwa ajili ya matumizi ya Jeshi. Aidha ukamilishaji wa nyumba zilizojengwa kwa njia ya ubunifu unaendelea katika magereza 11 nchini.
Ili kutoa nafasi zaidi kwa wafungwa wanaopokelewa magerezani, idadi ya nafasi za kuwalaza wafungwa zimeongezwa kutoka 22,699 mwaka 2005 hadi nafasi 29,552 mwaka 2011.

Jeshi la Magereza pia limeanzisha na kutekeleza jukumu la kuwapeleka mahabusu kwenda Mahakamani na kurudi gerezani kwa kutumia mabasi ya kisasa. Zoezi hili lilianza rasmi tarehe 19 Mei, 2008 kwa mahabusu waliopo mkoa wa Dar es Salaam na wale wa mkoa wa Pwani. Kwa sasa zoezi hili limeendelezwa katika mikoa ya Arusha na baadhi ya wilaya za mkoa wa Dodoma, na litaendelea kutekelezwa kwa awamu nchi nzima.
Mafunzo mbalimbali yameendeshwa ndani ya Jeshi la Magereza na watumishi 5,889 walihitimu kozi mbalimbali hadi mwishoni mwa mwaka 2013.

ITAENDELEA

 
Jeshi la polisi mmefanikiwa kuwafanya askari wa usalama barabarani kuwa matajiri kwa kupokea hongo.
Pia mmefanikiwa sana kuilinda Ccm kufanya mikutano yao kwa amani bila vibali na kuwakandamiA wapinAni wasifanye mikutano kwa kisingizio cha itelijensia. Hamko fair kwa hilo. Mtajisifu ila wananchi qanawaona kwa mtaAmo mwingine. Waacheni Ccm wapambane qenyewe maana hamkuanIshwa kwa malengo ya kulinda chama tawala.
 
sijaona mafanikio ya wizara hii kwenye idara 5 zinazosimamiwa kama ilivyoainishwa kwenye post hii
1. polisi-hatuoni ueledi wowote wa polisi katika kuhandle mambo mbalix2 kama vile mikutano ya vyama pinzani na ccm
2. magereza-hatuoni wafungwa wakiwa na maadili yoyote mara watokako kifungoni kama ilivyoandikwa humu zaidi ya kuwaaona wakiwa afadhali hata kabla hawajaenda jela
3. zima moto na uokozi wa maisha/mali, hapa ndo kabisa. mara nyingi tumeshuhudia magari yakienda kuzima moto bila kuwa hata na maji na mwishowe kuishia kutukanwa na waathirika.
4. uhamiaji, niongelee sehemu moja tu. suala la ajira lilifanyika kindugu mpaka hata leo hawajatangaza tena nafasi hizo
5. vitambulisho vya taifa, hapa kila sehemu ni ovyo. sina hata pa kushika.
 
teh teh teh!polisi goigoi,kutesa watu,upokeaji wa rushwa,kubambikiza kes,ajira za kindugu.ni hayo tu
 
LESIRIAMU, KUWA MKWELI NDUGU MIKUTANO YOTE HII INAYOFANYA PAMOJA NA MAANDAMANO KILA LEO BADO MNASEMA MNAKATAZWA KUFANYA MIKUTANO WAKATI HUU MPO KANDA YA ZIWA KATIKA KAMPENI, NDUGU UKWELI HUMUWEKA MTU HURU
 
Back
Top Bottom