Baadhi ya maeneo jijini hayana umeme kwa karibu masaa 36. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baadhi ya maeneo jijini hayana umeme kwa karibu masaa 36.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Greek, Feb 16, 2011.

 1. Greek

  Greek Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili halivumiliki sasa, Jamani huku dar sasa kuna baadhi ya maeneo hatuna umeme kwa jaribu masaa 36 sasa. Mimi nipo kigamboni na mara ya mwisho umeme tuliuona jana asubuhi. What the hell is this..?
   
 2. Greek

  Greek Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili halivumiliki sasa, Jamani huku dar sasa kuna baadhi ya maeneo hatuna umeme kwa jaribu masaa 36 sasa. Mimi nipo kigamboni na mara ya mwisho umeme tuliuona jana asubuhi. What the hell is this..?
   
 3. M

  Matarese JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Vumilia tu mwanangu, ndio maisha bora kwa kila mtu mwenye amani na utulivu
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mgawo wa umeme utakuwa historia ya nchi yetu! Ngeleja anafanya kazi nzuri sana.
   
 5. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tusubiri wabunge wamalize kugombea posho na pesa na kununulia magari mkuu ndipo wafanye jambo

  Nilianzisha thread hapa kwamba bunge lifungwe kwa sababu wanazungumza na kulalamika kama ambavyo sisi raia tunazungumza na kulalamika kupitia vyombo vya habari. Hatuhitaji bunge ambalo linakwenda kurudia mazungumzo yetu mjengoni kisha tunawapa mishahara minono na posho na magari!!

  Kabla bunge halijakaa kila mtu alikuwa na matumaini kwamba litakapokaa basi tatizo la umeme litapatikana na Ngeleja angelazimishwa kujiuzulu. Badala yake mgao wa umeme umepandishwa cheo na kuwa Bila Umeme Daima wakati wabunge wako mjengoni wanakula bata!!!

  Tangu jana hata simu ziliisha charge imebidi sasa hivi nije ofisini kuwasha jenereta ili nicharji simu. Siwezi tena kununua vyakula vya kutosha wiki au mwezi, vitaoza. Kwa hiyo inabidi kwenda sokoni kila siku! Hatuwezi kusikiliza radio wala kutazama tv. Usalama ndio usiseme usiku ilivyo giza. Huwezi amini uko Dar na hasa kwamba unaishi katika karne hii.

  Niambieni maandamano yanaanzia wapi, i am sooooo pissed off
   
 6. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Mbona mnazidi kuvumilia maana sijasikia mkiandamana kwenda ofisi za Tanesco kuwashinikiza wawapuynguzie hayo makali. Nadhani kwa namna moja shida za kukaa gizani mmezizoea.
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuna habari kuwa Bwawa la Mtera na mabwawa mingine yanavujisha maji ,kwani mvua ni nyingi sana lakini kina cha maji hushuka kwa haraka sana,ingawa ni siri wataalamu wamegundua kuwa maji huwa yanapungua kwa haraka sana ,kilichogundulika ni kwa kuta za mabwaha hayo kuzeeka na kupoteza nguvu ya kuzuia maji yasipenye kwenye kuta ,kubwa zaidi na la kukatisha tamaa ni kuwa hakuwezi kufanyika repairing ,kutatua tatizo ni kuvunja na kuyajenga upya ,tokea yajengwe hakuna ukarabati wa aina yeyote wala hakuna utunzaji ni kutumia tu mpaka lipasuke na ndio hivyo yamekwisha expire. ,Nyerere alisema mali mnayo lakini mnaikalia ! akimaanisha uranium.
   
 8. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Umemeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. K

  Kingofkinzudi Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo la umeme sasa ni kubwa. Rufiji basin peke yake inauwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kutumika tanzania na kubaki. Feasibility study zilifanywa toka miaka ya 1980. Na RUBADA ikaundwa kusimamia investment kwenye Rufiji basin. Lakini hakuna mipango na utekelezaji madhubuti. Katika ubepati instability ni opportunity kwa hiyo naona kuwa mabepari wanaocreate hii instability ya kukosa power ili watumie opportunity hiyo kumake business.
   
 10. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,231
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Nipo Njiro Arusha,umeme ulikatika kuanzia jana yapata saa nne usiku na hadi natoka mchana wa saa saba umeme ulikua bado umezimwa!
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jana nilipita iringa ruaha kama imeanza kufulika vile hasa ukipita pale darajani ipogolo
  Au mtera imetoboka?
  Ila tuwe wavumilivu kwa kuwa tuliiweka wenyewe CCM na ndo maisha bora hayo yakisimAMIWA NA SHILIKA LA MGAO WA UMEME
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pengine tutumia thread hii kutathmini ni maeneo gani ambayo yamekuwa hayana umeme kwa saa 36 zilizopita. Endeleza hii orodha;

  Kigamboni
  Njiro Arusha
   
 13. Greek

  Greek Member

  #13
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kwani jamani tatizo haswa linalo sababisha mgao wa umeme ukiondoa siasa na ushabiki ni nini? Unajua viwanda na biashara nyingi zimeanza kufungwa kutokana na tatizo hili as a result watu wataanza kupunguzwa kazi huku bei za bidhaa zikizidi kupanda. Nadhani watu wakuanzisha maandamano ndio tutawapatia hapo coz hatawakuwa na jinsi zaidi ya kuandamana kwa nguvu zote.
   
 14. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Nchi imeoza sana hii, nawambia jamani amkeni
   
 15. Glue

  Glue Senior Member

  #15
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kwakweli umeme umekuwa ni janga la taifa. Watanzania wanazidi kuwa masikini siku hadi siku huku viongozi wetu wakitudanganya kama watoto wadogo. Huku kwetu mwananyamala, wakiamua kuzima, wanazima mpaka siku mbili sasa cjui tatizo ninini? Watu wanatishwa eti kwa sababu hawakuichagua ccm(udiwani) so its like a revenge. Nadhani tetesi hzi zina kaukweli kwani maeneo ya jirani ambayo ccm ilishinda, hali ni tofauti kabisa. Hvi kweli tanzania kuna haki?
   
 16. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Nimeonge na jamaa yangu yuko rombo amenambia hawajapata umeme tangu juzi nkamwambia ndo maisha bora kwa kila mbongo. Nakumbuka rais wa wanaccm aliwahi kusema kuwa kufika 2008 au 2009 shida ya umeme bongo ingekuwa historia leo ni twenty eleven!
   
 17. m

  msitaki Member

  #17
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  tusubiri toune..walisema maji yaliisha..haya yetu macho..
  :twitch:
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kwani ratiba ya mgao inaonesha mtapata umeme mara ngapi kwa wiki?
   
 19. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Yeye ndiye sasa amekuwa historia ya rais anayesema uongo tz kuliko waliomtangulia
   
 20. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mkuu si unajua hata madarakani kaingia kwa uwongo? Ndo maana anaishi kwa kudanganya tu!
   
Loading...