Baadhi ya madhara yanayoweza kumpata kiumbe aliye tumboni kwa mama kutokana na unywaji wa pombe kipi

nhassall

Senior Member
Dec 17, 2010
195
41
Baadhi ya madhara yanayoweza kumpata kiumbe aliye tumboni kwa mama kutokana na unywaji wa pombe kipindi cha ujauzito ni pamoja na:

Kutoka/kuharibika kwa mimba
Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo
Mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa mbavu na kidari (sternum)
Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya mgongo uliopinda (kibiongo) na vidole vilivyoundana
Mtoto kuzaliwa akiwa na kichwa kidogo kuliko kawaida (microcephaly)
Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya pua
Kuzaliwa na matatizo ya taya
Mtoto kuwa na matatizo ya kutokuona mbali
Matatizo ya moyo kama vile moyo kuwa na tundu
Matatizo ya figo
Mtoto kuwa na ubongo mdogo na pia matatizo ya akili
Mtoto kuzaliwa akiwa na mdomo sungura (lip palate na cleft palate)

Matatizo ya kimaumbile ya masikio na ulemavu kwenye sehemu za uzazi (genital malformations).
Aina mojawapo ya kansa ya chembe nyeupe za damu (Acute Myeloid Leukemia). Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida moja la utafiti wa kansa la Marekani lijulikanalo kama Journal of the American Association for Cancer Research.

Ieleweke kuwa, madhara haya si ya muda bali ya kudumu ambayo yanaweza kusababisha kifo kwa mtoto, malezi na makuzi ya tabu na hata hisia mbalimbali katika maisha.

Kama wewe ni mjamzito, ni vizuri kuacha kunywa pombe. Hata hivyo wanawake ambao walikuwa wanatumia pombe wakati wa ujauzito wasiwe na hofu sana na habari hii. Kuna msemo uliozoeleka kitabibu kuwa si kila mvutaji wa sigara anapata kansa ingawa ukweli ni kuwa wavutaji wapo katika hatari kubwa zaidi.

Hali hii pia ina ukweli linapokuja suala la unywaji wa pombe wakati wa ujauzito kwamba si kila mtoto anaathiriwa na unywaji wa pombe ingawa hatari ya kuathirika ni kubwa zaidi. Hivyo basi ni muhimu kwa mama mjamzito kufanya maamuzi sahihi ya maisha ya mtoto wake
 

Jamani napenda kuchukua fursa hii ili tuweze kuelimishana kuhusu unywaji wa pombe kwa kina mama wajawazito. Jambo hili limekua likitokea sehemu nyingi Duniani ikiwemo nchi yetu Tanzania. Najua hapa tulonge kuna kina mama wengi tu pamoja na madaktari (kama wapo) ambao
wanaweza kutupa elimu juu ya hili.

Ni kwamba Pombe na Sigara kwa mama mjamzito nihatari sana kwa yeye mwenyewe pamoja na kiumbe kilichopo tumboni.. Wataalam

wanasema nivizuri kuiiandaa "kufanya maandalizi" kabla ya kubeba mimba.. maandalizi yenyewe mojawapo ni ku-simama kutumia

pombe/sigara au kilevi
chochote.. ikiwezekana kwa muda flan.. miezi 6, mwaka au zaidi KABLA ya kushika ujauzito.. ukifanya hivyo mtoto atazaliwa akiwa "mkamilifu". Huyu dada inaonekana yupo club. hiyo sehemu ina "kelele" ambazo kiumbe kilichopo tumboni kinazisikia kama kawaida..


Niliona program flani - "utafiti" walikuwa wana msikilisha mtoto aliye tumboni aina mbali mbali zamuziki na kuangalia anavyo re-act.. miziki ya

taratibu iliweza kuchukua nafasi kubwa sana kwa ni kiumbe kilikuwa kinaonekana kwenye "ultrasound" kikiwa kina relax na kupumzika vizuri

sana ... lakini miziki ya makele... mtoto alikua anaangaika huku na kule ikimaanisha hizo kele zilikuwa zinamsumbua na si nzuri kwani mtoto hapumziki.


Ndiyo maana wakati mwingine mwanaume/baba wa mtoto anashauriwa kuongea/kumuimbia mtoto wake kuanzia akiwa bado tumboni.. kwani

anamsikia vizuri kabsa! hiyo inajenga mahusiano na upendo mkubwa kati ya baba na mtoto kabla na baada ya kuzaliwa. Mtoto anamjua/mfahamu baba yake kuanzia stage ya awali kabisa..
 

Attachments

  • Pombe.jpg
    Pombe.jpg
    29.9 KB · Views: 68
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom