Baadhi ya maboksi ya kupigia kura ya kura hewa tayari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baadhi ya maboksi ya kupigia kura ya kura hewa tayari

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Saharavoice, Oct 29, 2010.

 1. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kuna tetesi kwamba baadhi ya maboksi ya kupigia kura yana kura hewa ndani yake. inasemekana kwamba maboksi hayo yamefungwa kitaalamu kiasi kwamba si rahisi kugundua hila hizo. ukiunganisha na taarifa kwamba kila kituo kina majina 100 hewa then uvumi huu unaweza kuwa kweli.

  Angalizo: Mawakala wa vyama vya upinzani pimeni uzito wa kila box ili kujua kama uzito unawiana kwa sababu kwa mujibu wa baadhi ya wasimamizi wa Kura, kuna maboksi mazito na mepesi. swali la kujiuliza kama habari hii ina ukweli, Je maboksi yametengenezwa kwa standard tofauti?
   
 2. doup

  doup JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  nilishawahi kuwa mkuu wa kituo chaguzi ya 2000 huko nyuma; inatakiwa box liwe wazi kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza na lionyeshwe kwa mawakala wote, alafu kifuniko na kufuli viwekwe. sijui kama taratibu zimebadilika mawakala wawe macho na wafike vituoni mapema alfajiri na kuthibitisha hilo.

  Wagombea wawape mikakati mawakala wao, kuondoa wizi wa kura wa kienyeji.
   
 3. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mpenzi wa slaa na nimewahi kusimamia uchaguzi. Mabox ni transparent na kabla ya kuanza kupiga kura yanakaguliwa (utaratibu wa 2000) so sitaki kuamini habari hii
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hoja hii haina mashiko kihivo.
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  masanduku ni transparent, cha muhimu ni wasimamizi kuchukua idadi ya watu waliojiandikisha ambao wako kwenye list na baada ya uchaguzi, wafanye rikonsiliasheni ya idadi waliyonayo na ya kura zilizopo, na hilo la namba bila jina wanatakiwa waliweke wazi mapema kuwa halitakubaliwa kwa mtu mwenye namba tu bila kuwa na jina kupiga kura
   
Loading...