Baadhi ya Lecturers wa Mzumbe wana degree Feki - VC wao naye FEKI

Jesus Christ! what an I...t am I talking to!!?

Mzumbe has always been a second choice to Tanzanians students. Division one wanawahi Udsm two na three wanaenda kuchukua diploma Mzumbe. Hiyo ilimkumba hata Warioba wenu, hakuwa na sifa ya kusoma Udsm ikabidi aanze safari ndefu ya diploma kisha post diploma.

Kuwa na Grand points ya 3.8 kwenye first degree (second upper class) kwa UDSM kuna kupa nafasi ya kuajiriwa kama mwalimu wa chini (tutorial assistant). Baisi alikuwa na masters inayotambuliwa na USA(ulivyosema) hiyo ni a PLUS kupewa part time kazi. TATIZO ni nini hapo.

Ndugu Nungwi hata uandishi wako unaonyesha ni wa kishabiki na usio na point za kupangilia. hivi unajua kuwa Faculty of commerce UDSM itakuwa Business school soon? au huelewi naongelea nini?

Nenda duniani kote mueleze mtu nina Bcom ataelewa bila kukuuliza ni nini, ila BAFU inabidi akuulize kama ni kuoga au ni nini?

Check statistics za wanaoingia UDSM uone pass mark zao.

Wanaomaliza UDSM ni hot cake kwa makampuni ya kigeni na mashirika makubwa, hawana haja na low paying jobs serikalini na ndiko walikojaa akina kamala, warioba na hao pruducts za Mzumbe ambao baadaye wanawafanyia mtimanyongo wa UDSM. Hiyo ndio siri ya wanasiasa wengi kuwa product za Mzumbe na degree feki. Wanakimbilia siasa kwasababu kazi zao hazilipi.

Na ndio maana nchi hii haiendelei na wala haitoendelea!!!

FD
 
Samahani waheshimiwa niliiposti kusikohusika.nungwi
Junior Member Join Date: Sep 2006
Posts: 7




--------------------------------------------------------------------------------

Heshima zenu wakuu, Fikiraduni,Ogah,DR wenu Assad,Mtz,mwanasiasa na wote bila kumsahau AL-jazeera.

waheshimiwa mie sikukimbia nadhani nyote mnajua tatizo la Taifa(UMEME).

kuna mengi Mzumbe inazushiwa eti kuwa wasomi wake wanakimbilia siasa tu. je UDSM mbona mnao wanasiasa mahiri kama akina Mbatia hadi uenyekiti wa Taifa wamechukua? bila kuwasahau wagombea wenu wa Urais professor shayo na DR. mvungi ambao kura zao ukizichukua zote nchi nzima haziwezi kufikia kura za jimbo la mheshimiwa DR.Nchimbi tu wala sikupelekeni kwa Dr. Kamala. hiyo ndio product Ya Mzumbe university. kazi ya mzee Warioba samahani sijampa haki yake Dr. warioba.
mmedai UDSM makini na hakuna upuuzi wa kijinga.
je hiyo Business school inayotaka kuanzisha itaongozwa na kibaisi Chijoriga?
Maana UDSM kuna vibaisi wakumwaga.
Marcelina Chijiriga kaingia UDSM 1980 na mara baada ya kumaliza masomo yake akabakishwa afundishe pale baada ya kupata Marks za chupi.
akaenda Katholik university lueven-Belgium kufanya MBA KWA SCHOLARSHIP. mwaka wa kwanza tu kapigwa za uso(kafeli) na akakatiwa scholarship anaona noma kurudi bongo akamuua kurudia mwaka kama Private student then akafaulu kimkandamkanda.

Mwaka huu search committes za chuo ziliundwa kutafuta Deans wa vitivo mbalimbali kwenye kitivo cha commerce DR.Assad alichuana na Dr.chijorija na ASSAD akaibuka mshindi kwenye interview, kamati ikapendekeza jina la Assad then majina yakapelekwa kupigiwa kura na staff wote wa faculty
Again mzushi wenu Assad akamshinda DR. wa marks za chupi cha ajabu professor Luhanga akampendekeza DR. Marcelina Chijoriga awe DEAN wa commerce. AIBU!!!!
je Augutino Moshi uliyedai kuwa UDSM hakuna uchafu huo ni nini? fikiraduni mambo haya ya kubebana kijinga huwezi kuyaona Mzumbe university na hata mzee wetu kiona mbali DR. WARIOBA hana ujinga huo ambao professor wenu kaufanya? ndio maana serikali huchukua watu wa mzumbe kutokana na misingi mizuri Waliyopikiwa.
Mnadai itakuwa BUSINESS SCHOOL VERY SOON JE KWA MARKS ZA CHUPI?
 
Maswali mazito kwenu na DR. wenu ASSAD.
Ilikuwaje yeye katika makala yake mbona hakuandika alivyopigwa bao na professor Luhanga licha ya kushinda na kustahili nafasi ya kuwa Dean wa Commerce akapewa DR. Chijoriga(Marks za Chupi)?
pia kuna mtu juu anadai Mzumbe university inatumia public funds sasa lazima iwe makini.
mbona hatuambii jinsi Chijoriga alivyopoteza pesa za serikali kwa kufeli MBA yake-Belgium?
hata Taratibu za kupeana nafasi za UDSM zinamizengwe mingi na ubabaishaiji tu. huyo professor(LUHANGA) wenu hawezi kumfikia mzee wa hekima DR.Warioba,
hata huyo Assad wenu angekuwa Mzumbe angenjoy kazi yake. kama pia yeye ni mwandishi mzuri atuandikie mada ya yeye kuikosa nafasi ya UDEAN?
hata hii topik heading yake inadhihirisha kuwa kuna kigenge cha watu wenye chuki na Mzumbe. otherwise ingeandikwa Lecturers feki elimu ya juu.
PhD ya chijoriga haitofautiani na ya Ngirwa ambaye nitajadili soon.kwani nae alikuja nayo feki toka Austria.
Mwisho Dr,Assad acha chuki na Mzumbe yaliyokukuta yasingekupata kama ungekuwa kwa mzee Warioba(kiona mbali) lakini umekuwa mvivu wa kufikiri.
pia naomba mchango wako Augustino Moshi kwa kuuongopea umma kuwa UDSM ni malaika hakuna ubabaishaji?
 
Nungwi mi naona we unatuzingua hapa, unataka kudivert attention. Naomba utueleze wanabodi kama tuhuma hizi kuhusu member wa academia Mzumbe ni ni za uongo? Personally nilishasema kwenye one of my previous post how I admire MU, that Uni has a potential for high reputation. Tatizo ni hao watu wachache with their bogus qualifications, Nungwi hii kitu ruins the academic reputation of MU regardless of how great Mzumbe is or will be!

Naomba tusifanye mud slinging ya watu, nimecheki kwenye web profiles za Chijoriga na Baisi http://udec.udsm.ac.tz/associates.php

Dr. Marcellina Chijoriga is a Senior Lecturer in the Department of Finance, Faculty of Commerce and Management, University of Dar es Salaam. She holds a B.Com degree in Accounting from the University of Dar es Salaam, Tanzania, an MBA in Finance from the Catholic University of Leuven, Belgium, and a Ph.D. in Economics and Finance from the University of Economics and Business Administration Vienna, Austria. She also holds a Postgraduate Diploma in Institutional Economics from the University of Connecticut-USA and a Diploma in Business Administration from the College of Business Education, Dar es Salaam.

Mutahyoba Baisi is a Lecturer in the Department of Finance in the Faculty of Commerce and Management at the University of Dar es Salaam. He has worked for the University of Dar es Salaam since 1982 when he graduated with a B.Com honors. Prior to joining the University Mr Baisi worked as a Trade and Industrial Assistant with the Ministry of Industries and Trade for two years. Mr Baisi holds an MBA in International Business and Finance from the University of Antwerp ( Belgium) and an MBA in Finance and Accounting from Florida A & M University (USA). Currently, he is finalizing his PhD in Finance at the University of Dar es Salaam.

Sasa hawa jamaa ni chuo kipi walichosoma ambacho hakitambuliwi kama ilivyo hao "vihiyo" wako?

Naomba usishabikie mambo tu kwa vile wewe ni alumni wa Mzumbe, we all want MU to reach its anticipated academic achievement for the beterment of our nation.
 
Suala la uteuzi wa deans na directors kwa uelewa wangu huwa linakuwa kama lifuatavyo. Members wanapiga kura (Academics and some student respresentatives) halafu the best three wanapelekwa juu, usually senate and then council kama sikosei. Hapo wote watatu wana equal chance ya kupewa udean au udirector depending on what those two organs will decide. Ndio maana mtu anaweza kuongoza kwenye kura halafu akapigwa chini, but in most cases aliyeshida kura ndio anapewa hicho cheo. The same happens kwa heads wa department though final decision yao sidhani kama inafika senate. That could explain why Chijoriga was picked in place of Assad, though I'm not sure.
 
Hivi huyu Assad si yuko kwenye Tume ya Kupitia Mishahara ya Watumishi wa Umma iliyoundwa na JK? Ndiye huyo mwenye kampuni yake ya Ukaguzi wa Mahesabu jijini Dar?
 
Nungwi,

Kinachoongelewa ni sifa za degree za Phd za baadhi ya waalimu wa MU. Na sio wanavyotenda kazi. Tunazungumzia uhalali wa wao kufundisha na kutoa Phd ilhali wao hawana Phd. Tunamuheshimu Mr narudia Mister Warioba VC wenu, tuna waheshimu akina Kamala na wengineo. Hapa tunahoji tu Phd na uhalali wa kufundisha.

Usipindishe mada. Kufeli au kurudia na kufaulu hakufanyi degree kuwa FEKI.
Ulileta UONGO KUWA BAISI ANA PHD. Umeshindwa kuutetea uongo wako. data zimemwagwa na wazee, umebakia unaandika visivyoeleweka.

Mwanangezi, kuhusu Dr Assad kuwa na kampuni au kuteuliwa sijui. kwangu mimi thats personal. Hapa naangalia sifa yake na umahiri wake wa ufundishaji.

Hata ukiangalia mada inasema "baadhi ya ma lecturers wa Mzumbe......" ina maana tuna i respect Mzumbe ila tunasema Ma Dr FEKI, waende shule. PERIOD!

Ndugu Nungwi, ukijibu kwa staili ya hapo juu sitakuelimisha tena, maana utakuwa unabishana mpaka kufa with no reasonable reasons.

Kazi njema, sorry mzee kuhusu umeme, sisi huku majuu tunapeta tu!

Alamsik

FD
 
Mimi ni mwanachama mpya niliona ni vyema kuchukua fursa hii kwakilisha yafuatayo kwenye hii forum kuhusiana na mada nilioitaja hapo juu.

1. Kwanza kabisa naomba tukubaliane kuwa academics is not politics. Academics ina vigezo vyake; viwango na taratibu. Politics ina hamasa (emotions) na bla blaa. Na katika hayo, tukubaliane pia kuwa anybody can be a politician (In Tanzania, kama Amina Chifupa amekuwa Mbunge, "Dr" Kamala kupata uwaziri sio ajabu!! Huo ndio mfumo wa taifa letu), lakini academics kwa upande mwengine ina wenyewe; na sio kila anaetamani tu awe!! Wanatafuta hadhi za UDOKTA ili wakaombee kura, wakatese kwenye vikao vya harusi, kwenye round bar nk.

2.Tanzania ina uhaba wa Vyuo vikuu; na tunahitaji atleast chuo kikuu kimoja kwa kila mkoa; hivyo sidhani kama forum hii ilikuwa ina dukuduku na Mzumbe kuwa chuo kikuu, kama ustawi wa jamii kinatoa Degree, kwanini mzumbe isitoe? Hoja kubwa hapa ni CREDIBILITY. Any Organization is judged by its management, perfomance and output among others. UDSM kina kashfa zake, ila hizo kashfa ziko contained within; na ukipekuwa utazikuta RUNDO; lakini pamoja na hayo, hizo kashfa hazi-compromise integrity ya chuo. MU inaongoza kwa kashfa za BOGUS DEGREES, na kiongozi mtendaji wa chuo mwenyewe amewaonyesha subordinates wake mfano kwa kuwa na Bogus Degree. Sasa kama hali inakuwa namna hio, nataka niwaulize mashabiki wa MU maswali yangu yafuatayo.
(a) Mfano MU imetangaza kazi za Tutorial Assistants, na Assistant Lecturers. Katika waombaji kuna wenye Degrees na Masters kutoka PWU; je wapewe dhamana ya kusomesha wanafunzi wetu?
(b) Mtu anaedanganya kwa ku-kopia mtihani na anaedanganya kwa kununua mtihani ana makosa au la? na ni hatua gani zinazochukuliwa na MU ikibainikia kuwa kuna mwanafunzi alidanganya kwenye mtihani?
Siku zote, mtu inabidi awe mwaminifu kwa muajiri wake, hususan masuala ya credentials yanapohusika. Je Council ya MU inatambua qualifications za PWU?
Kama inazitambua, inabidi kuna kazi kubwa ya kufanya. Je HEAC inatambua degree za PWU?Kama inazitambua, kazi inazidi kuwa pevu; na itabidi hatuna tena mtetezi; kwani itabidi ipelekwe kwa waziri wa elimu wa juu ambaye inawezekana akawa "Dr" Kamala au Muheshimiwa Chifupa!! Likifika BUNGENI ndio kabisa!! Kwani litawakuta akina "DR" Nchimbi, "Dr" Mzindakaya "DR" NGula "Dr" Mlaki pamoja na madokta wengine; litajadiliwa kwa marefu na mapana kama lilivyojadiliwa suala la "Darwin Nightmare" na Katuni aliechorwa na Masudi KIPANYA!! Bunge letu lina muda wa kutosha wa kujadili kila mada.

3. Kama kweli Tanzania inatafuta maendeleo, basi inabidi tuanze kufanya kazi ya kusafisha uozo wa BOGUS DEGREES, kuanzia MU kwenda Mbele. Akina Kamala, Warioba Machangu, Mugoya, Mafwenga etc watangaziwe kuwa forgery zao zimebainika, na Doctoral titles zao ziwe stripped-off kwenye academic forums. Watese nazo huko kwengine. Na waajiri wao watafute ushauri wa kisheria ili kuwabana zaidi. Hii itasaidia kupunguza kasi la hili wimbi kali la VIHIYO. Kama Mkuu wa Chuo, Waziri, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mbunge ni VIHIYO, kweli vijana wa Kitanzania watakuwa motivated kusoma au kusaka Degree zao kwenye PWU and the likes?lazima tuweke mfano mzuri wa kuigwa na vijana wetu na wenzetu. Tukifanya maskhara tutageuka kuwa TAIFA LA VIHIYO!!!!

4.Ninachopendekeza kwa wana-forum ni kuwa na uzalendo wa kitaifa. Tusilete siasa katika academics. Tusizungumze ki blaa blaaa, tusimsakame Dr Assad. Hii khabari ya BOGUS DEGREES kutambuliwa katika ngazi tofauti tofauti nchini ni khatari kwa taifa letu. Tujadili athari zake kwa maendeleo ya taifa; pamoja na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kulimaliza hili suala. Dr Assad aliamua KUPIGA MAYOWE baada ya kuona JAHAZI LINAZAMA; hakumtaja mtu kwa jina. Alifanya hivyo kwa uchungu wa maendeleo. Tusiwe mashabiki wa uozo, kwani LONG TERM impacts zake kwa credibility ya vyuo vyetu itakuwa ni kubwa. Tukumbuke kuwa Pesa za walipa kodi ndizo zinazotumika MU. Lazima zitumike kwa njia inayoridhisha.

TAMATI

Mniwie radhi kwa kutoa mchango mrefu. Hili limetokana na kwamba nimeguswa sana na hili suala. Mnisamehe pia kwa kuwaomba muache ushabiki, kwani haulisaidii taifa; msinione JEURI au MJUBA.

Naomba maoni yenu


Msema Kweli
 
Mzee Fikira DUni alizungumzia kuhusu kuwaheshimu Misters Kamala ana Warioba. Hio ni social respect ambayo wamevuna kutokana na michango waliotoa kwa nyakati tofauti.

Tukubaliane kuwa mtu hata uwe msafi kama weupe wa maziwa, ukifanya zonge moja tu, basi ule usafi wako unapotea ghafla!!

Sasa hawa ndugu zetu, wamechafua; na hilo lieleweke kuwa hivyo, na sio vyenginevyo. Ni HADAA ya wazi kwa JAMII NZIMA ya KITANZANIA, na ni kejeli kwa wale ambao wanatumia miaka kusotea PhD zao.

Suala ninalouliza hapa, tuendelee kuwapa heshima watu wanaoendeleza hadaa na kejeli?? Mimi binafsi yangu, heshima yangu inapungua kwao; na itarudi kuliko mwanzo endapo wao wenyewe wataamua kuchukua hatua ya kuzikana hizo fake credentials kwa maslahi ya umma.

Naomba maoni
 
Augustine Moshi said:
UDSM sio rahisi hata kidogo wadanganyike na digrii ya mtu. Wakubwa wa pale ni wasomi waliobobea mno. Nawaelewa vizuri, kwani nimeshafundisha sana pale.

Ukija na ka PhD UDSM, huwa wakubwa wa pale wanawasiliana moja kwa moja na chuo ulichotoka. Hawaangalii tu vyeti vyako. Na kama umepata cheti mahali pasipoeleweka kama PWU, wala hawatakutazami.

I know for a fact that UDSM has a strict vetting system. I was vetted in the same way when I returned there, in 1987, with a PhD in Mathematics. They verified everything with my university, Carleton (Canada) before accepting my PhD.

Hakuna vihiyo UDSM. Wakijitokeza wanafukuzwa kazi, hawaachwi pale. Vyuo vipya vinavyoanzishwa viige mfumo wa UDSM


Augustine Moshi

Hats off,Mzee.PhD ya "namba" si mchezo (especially for a poor me who got a luck escape with a D in maths in O'level).Congratulations.And I,being a UDSM graduate myself,do agree with you that it's highly unlikely for mtu mwenye degree feki to escape the UDSM's strict vetting system.However,hata kwenye mfumo bora kabisa bado kuna possibility ya wajanja (crooks?) kujipenyeza na pengine kutakuwa na mtu mmoja wawili ambao academic credentials zao ni questionable.As mchangiaji mmoja alivyosema hapo juu,reputation ya UDSM bado iko juu.

Ranking ya African universities (nafasi zao in world ranking in brackets) [source:http://www.webometrics.info/top100_continent.asp-cont=africa.htm]


1 UNIVERSITY OF CAPE TOWN 546
2 STELLENBOSCH UNIVERSITY 548
3 UNIVERSITY OF PRETORIA 554
4 UNIVERSITY OF THE WITWATERSRAND 636
5 RHODES UNIVERSITY 683
6 UNIVERSITY OF THE WESTERN CAPE 894
7 UNIVERSITY OF SOUTH AFRICA 1,256
8 UNIVERSITY OF KWAZULU-NATAL 1,478
9 AMERICAN UNIVERSITY IN CAIRO 1,518
10 UNIVERSITY OF THE FREE STATE 1,933
11 NORTH WEST UNIVERSITY POTCHEFSTROOM 2,029
12 UNIVERSITY OF PORT ELIZABETH 2,217
13 UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM 2,566
14 PORT ELIZABETH TECHNIKON HIGHER EDUCATION 2,764
15 UNIVERSITY OF LA REUNION 2,891
16 UNIVERSITY OF ZIMBABWE 3,318
17 CAPE TECHNIKON 3,498
18 UNIVERSITY OF NAMIBIA 3,612
19 MAKERERE UNIVERSITY 3,628
20 UNIVERSITY CHEIKH ANTA DIOP 3,641
21 POLYTECHNIC OF NAMIBIA 3,752
22 UNIVERSITY OF MAURITIUS 3,799
23 NELSON MANDELA METROPOLITAN UNIVERSITY 4,397
24 ARAB ACADEMY FOR SCIENCE & TECHNOLOGY 4,446
25 UNIVERSITY EDUARDO MONDLANE 4,457
26 TSHWANE UNIVERSITY OF TECHNOLOGY 4,484
27 UNIVERSITY OF NAIROBI 4,508
28 UNIVERSITY OF JOHANNESBURG 4,611
29 CAIRO UNIVERSITY Flag of eg 4,748
30 GERMAN UNIVERSITY IN CAIRO 4,791
31 UNIVERSITY OF ZULULAND 4,806
32 UNIVERSITY OF BOTSWANA 4,818
33 KIGALI INSTITUTE OF SCIENCE TECHNOLOGY AND MANAGEMENT 4,963
34 ECOLE MOHAMMADIA D'INGENIEURS 4,997
35 UNIVERSITE CADI AYYAD 5,038
36 NATIONAL UNIVERSITY OF RWANDA 5,140
37 AL AKHAWAYN UNIVERSITY 5,301
38 DURBAN INSTITUTE OF TECHNOLOGY 5,313
39 BURAO UNIVERSITY 5,353
40 ADDIS ABABA UNIVERSITY 5,355
41 MANSOURA UNIVERSITY 5,374
42 NORTH-WEST UNIVERSITY 5,411
43 UNIVERSITY OF GHANA 5,420
44 MEDICAL UNIVERSITY OF SOUTHERN AFRICA 5,572
45 UNIVERSITY OF THE NORTH 5,578
46 UNIVERSITE DE NOUAKCHOTT 5,703
47 UNIVERSITY OF KHARTOUM 5,741
48 AL AZHAR AL-SHARIF ISLAMIC RESEARCH ACADEMY 5,849
49 PENINSULA TECHNIKON 5,875
50 MOGADISHU UNIVERSITY 5,927
51 TECHNIKON WITWATERSRAND 6,011
52 SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE 6,090
53 ECOLE DU PATRIMOINE AFRICAIN 6,121
54 UNIVERSITY OF MALAWI 6,159
55 UNIVERSITY OF OUAGADOUGOU 6,199
56 UNIVERSITY OF FORT HARE 6,254
57 UNIVERSITY OF IBADAN 6,304
58 UNIVERSITE SENGHOR 6,321
59 UNIVERSITY OF HARGEISA 6,329
60 UNITED STATES INTERNATIONAL UNIVERSITY 6,347
61 MOI UNIVERSITY 6,353
62 MANGOSUTHU TECHNIKON 6,416
63 MONASH SOUTH AFRICA 6,429
64 ARAB OPEN UNIVERSITY 6,523
65 UNIVERSITY ABOU BEKR BELKAID 6,524
66 NATIONAL UNIVERSITY OF LESOTHO 6,579
67 OCTOBER 6 UNIVERSITY 6,591
68 UNIVERSITY OF SWAZILAND 6,624
69 OBAFEMI AWOLOWO UNIVERSITY 6,645
70 JOMO KENYATTA UNIVERSITY OF AGRICULTURE AND TECHNOLOGY 6,674
71 KABARAK UNIVERSITY 6,699
72 ASSIUT UNIVERSITY 6,705
73 KWAME NKRUMAH UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY 6,714
74 MOHAMMED FIRST UNIVERSITY Flag of ma 6,749
75 UNIVERSITE M'HAMED BOUGARA DE BOUMERDES 6,751
76 UNIVERSITY OF ALGER 6,756
77 KENYATTA UNIVERSITY 6,761
78 UNIVERSITY OF BENIN 6,769
79 UNIVERSITY OF NORTH-WEST MAFIKENG 6,817
80 UNIVERSITY OF YAOUNDE I 6,829
81 UNIVERSITY OF BATNA 6,860
82 UNIVERSITE DJILLALI LIABES 6,906
83 STRATHMORE UNIVERSITY 6,926
84 BOTSWANA COLLEGE OF AGRICULTURE 6,969
85 HELWAN UNIVERSITY 6,982
86 DAYSTAR UNIVERSITY 7,006
87 UNIVERSITY OF VENDA 7,059
88 AFRICA UNIVERSITY 7,084
89 UGANDA CHRISTIAN UNIVERSITY 7,176
90 UNIVERSITY OF LAGOS 7,181
91 SOUTH VALLEY UNIVERSITY 7,258
92 UNIVERSITY OF BLIDA 7,294
93 VAAL UNIVERSITY OF TECHNOLOGY 7,337
94 CENTRAL UNIVERSITY OF TECHNOLOGY FREE STATE 7,359
95 MODERN SCIENCES & ARTS UNIVERSITY 7,362
96 UNIVERSITE CHOUAIB DOUKKALI EL JADIDA 7,364
97 EGERTON UNIVERSITY 7,366
98 UNIVERSITY OF JOS 7,369
99 MINIA UNIVERSITY 7,434
100 INSTITUT DE FORMATION EN TECHNOLOGIE ALIMENTAIRE
 
Abramat,

Well said. Mimi nataka ni work out gharama za degree zao, nanunua Phd kisha narudi home kufundisha Mzumbe University. Najua nitachukua ajira saaafi sana.

Tena Nungwi akija pale nam supervise Phd yake, na lazima aisotee kwa miaka sio chini ya mitatu! aha hahahahah

Tanzania haitoendelea kamwe bila kuondoa watu wote waliopo kwenye entire system.

FD
 
Abramat!
Mchango wako ni mnene na umegusa penyewe kabisa! tatizo la bogus degrees ni cancer katika society kwa ujumla lakini hasa katika academia ambapo kutakiwa kuwa centres of academic excellence. Matokeo yake ni kuwa hata investors watagwaya kuemploy graduates, check out this from sunday observer;

Case to grant investors free hand on recruitment
2006-09-17 08:29:39
By Correspondent Michael Haonga


Tanzanians have been called upon to let investors employ whoever they believe can deliver irrespective of whether they were nationals or not.

The appeal has emerged from a two-week survey on whether or not privatised firms should absorb Tanzanians instead of foreigners in jobs where the two categories have the same qualifications.

Recently the country was swept with an outcry that some privatised firms had employed foreigners in jobs where locals were even better qualified than those absorbed.

Interviewees on the subject said there were a number of factors to be considered in arriving at who should be employed than just considering aspects of nationality and qualifications because matters of who the investor could vest confidence in should be considered.

’’Before advancing a blanket arguement that Tanzanians with qualification equivalent or even higher than foreign applicants should be employed in privatised or other firms in the country, it is important to have answers on whether that was the only factor that mattered,’’ noted one respondent.

He said even failures that saw nationalized companies fail to deliver are not only on account of having them under incompetent and unqualified nationals devoid of elements of corruption and other manipulative measures for personal gains.

It was noted that before coming up with such blanket protectionism related to employment in the privatised firms, it was necessary to address the issue of why public corporations and industries failed to deliver even though they were manned by well qualified nationals.

The respondents demanded that even though some sort of increased social welfarism may be necessary as well as protectionism, it should not be let to reach proportions whereby investors start to fear to invest in the country because they would not be allowed to employ people whom they trust and believe could deliver in line with their set targerts.

Noted too was the contention that change of working culture, seriousness and instilled productivity commitment did not evolve suddenly by having qualified nationals but also it was a process and depended on the exposure and the environment in which one had worked and attained the qualifications to that end.

Others argued that let those with an-art-of the trade in various fields prevail regardless of whether they were nationals or expatriates provided set production targets were being met.

SOURCE: Sunday Observer http://www.ippmedia.com/ipp/observer/2006/09/17/74569.html
 
Sina tatizo na umuhimu wa kuzingatia viwango vya taaluma katika asasi zetu za elimu ya juu. Hakika, wale wote waliotuhumiwa, kwa kuanzia waheshimiwa wabunge na wengine wenye madaraka, ilipaswa wafuatiliwe, na ikibainika wana hatia, waadhibiwe mara moja kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria.

Nina tatizo na hiyo stori hapo juu kutoka Sunday Observer. Ndiyo stori za kiujanjaujanja; stori ambazo mwandishi mzoefu lakini si mwadilifu, anaweza kubuni mwenyewe kulingana na hisia zake na ikachapishwa. Tuliokuwa karibu na vyombo hivyo tunayafahamu hayo.

Habari haisemi ni watu wa aina gani wamehojiwa kwenye utafiti huo wala idadi yao. Haisemi pia nini lilikuwa lengo la kufanya utafiti huo. Kichwa chenyewe ni kama mwandishi anapigia chapuo kwamba wawekezaji wawe huru kuajiri mtu wanayemtaka wakati baadhi ya hoja za hao waliohojiwa zinaonyesha kuwa kushindwa kwa baadhi ya makampuni yanayoendeshwa na wazalendo kunatokana na sababu nyingi na mbalimbali na si tu uwezo au ujuzi walionao.
Ni wangapi waliunga mkono wazo hilo na wangapi walipinga ili kufikia hitimisho hilo?

Pamoja na upungufu uliomo katika habari hiyo, sipingi haja ya Watanzania kufunga buti (kugangamala) katika elimu, lugha, na kujiendeleza katika mambo mbalimbali ili kuweza kushindana katika soko la ajira katika zama hizi za utandawazi. Pia tujenge utamaduni wa kuheshimu/kuthamini kazi badala ya kuwa watu wa stori tu!
 
Firaduni.
nilikuwa mkoani Mbeya kwa taarifa yako kuna kampus mpya ya Mzumbe university akifungua mheshimiwa Shein.
Na mzee DR.Warioba yuko mbioni kuweka kitu kipya na Dar.
Hizi data siwezi kuziamini kirahisi ngoja nizifanyie kazi hisia zangu zinanipata labda kitengo cha computer cha UDSM ndio kime compile.
Najiweka sawa mheshimiwa
 
Nawaomba wale wenye hisia hizi, hapa ndio mahala pa kujadili, kuna mada yangu ya Reginald Mengi imevurugwa na hoja hizi naomba muhamie huku na kule acheni tujadili mambo mengine. Samahani kwa usumbufu
 
Ndugu yangu Nungwi,

Pole na safari, karibu tena. Mjadala ulipooza with your absence, shusha vitu mjadala upambe moto!
 
Haya haya wanabodi mmerudisha hili tena?...
Je, mnataka nilianzishe vagi au?... babu ubishi nipo wala sintakimbia tena.
 
Mkandara,

Karibu mzee. Kwanza naomba umuelewe ndugu yangu wa karibu Nungwi, tatizo lake ni kuwa hata hizo data za UDSM kuwa ya 13 Africa anapinga, yaani hajawahi kuiona!!!!!!!!!!! kwanza msaidie akubali ndio tuendelee, maana tutazidi kurudi nyuma.

Pili naomba kabla hujajibu lolote (naelewa sana mtazamo wako) naomba unijibie makala ya Dr Assad Mussa. Kisha ujibu baadhi ya maswali aliyouliza Ogah na mimi ktk huu mjadala.

Sina shaka na uelewa wako nadhani utatupa mwanga zaidi.


Karibu.

FD
 
Jibu langu kwa wote na huyo Mh, Dr Asaad ni moja tuuuu..
Nini maana ya cheti feki?...
Cheti feki ni kile ambacho kimetolewa bila mwanafunzi kupata elimu hiyo. Hapa sioni kabisa uhusiano wa mashtaka yake. Hilo swala la shule hapa sioni linahusika vipi na ufeki!... kwani ukiondoa jina la shule ktk malumbano haya hakuna kitu feki tena.

Nitamalizia kipande hiki kwa maswali pia!
Kuna vyuo kama Devery ambavyo havitambuliwi na board zenu lakini vinatambulika na board nyinginezo. Wasomi wake wengi tu wamepata elimu zao na wanafanya kazi hukuhuku Ulaya. Hakuna mtu wala serikali iliyowakataza kisheria kuendesha shule zao. na wala wahitimu kukatazwa wasitumie wala kutundika vyeti vyao vya Devery.

Je, tumeweza kufanya utafiti wa ndani kufahamu kwa nini chuo hicho hakitambuliki!
Mara nyingi ndugu zangu hizi board ni biashara zaidi ya elimu kwani mauzo ya vitabu na vifaa vya elimu hupewa baadhi ya watu fulani. Waandishi wengi huweka mikataba na hizi board kutumia vitabu vyao kwa hiyo ukikataa kutumia vitabu fulani basi chuo chako kinaondolewa ktk orodha yao, hata kama viitabu unavyotumia wewe ni advanced na viinaeleza vizuri zaidi ktk elimu husika. Uhusiano kati ya chuo na hizi board ni MKATABA sio jinsi shule ilivyo ktk majengo na uwezo wa kutoa elimu. Elimu Ulaya ni biashara na kila mtu anatafuta monopoly kama tulivyokamatwa na microsoft...

Kabla hujatazama nje ni vizuri kutazama ndani mwako!
Hapa nyumbani tuna shule za msingi ambazo hazina majengo (chini ya miti), viti, vitabu wala kalamu lakini bado zinatoa wanafunzi kwenda secondary. Kuna secondary ambazo hazina vifaa vya sayansi hata kile kibatari kilichopewa jina la mtu - Burnsen burner na testtubes lakini wamepokelewa hapo UDSM baada ya matokeo mazuri ya mtihani wa mwisho. Na zaidi mbona wapo walioghushi mitihani lakini bado wamechukuliwa chuo kikuu?
Haya ndiyo maswala ya kuyaangalia mwanzo kabla hujataka kuzungumzia cheti cha mtu mwingine...
Ikiwa Mzumbe imepoteza mwelekeo kuwa na walimu wenye shahada za kuchapia basi inabidi tuziangalie shahada zote za Phd kwa undani zaidi kwani wapo walichukua Phd kwa mazingira ambayo hayaendani kabisa na yetu. Je, hao hawana vyeti feki?.. yawezekana kabisa kuwa Mzumbe wamekwisha ona siku hizi hakuna elimu tena isipokuwa ULAJI. Wameamua kufuata slogan ya chama - Ari, nguvu na kasi mpya.

Somo - Elimu kwa mtandao!
Badala ya kukaa masaa nane kwa siku darasani, elimu kwa njia ya mtandao inakupa nafasi wewe kusoma wakati wengine wamelala. Hatua ya mafanikio yako haisubiri darasa yaani mnakwenda wanafunzi wote kwa pamoja somo hadi somo, semister hadi semister. Elimu kwa mtandao ni juhudi yako, speed yako na kama kweli kichwa kimelala utamaliza mapema. Swala sidhani kama ni muda wa masomo... laaa!
Mbona hapa Ulaya kuna wanafunzi wanaosoma shule toka za msingi hadi kufikia University kwa miaka kumi tu na hata wengine chini ya hapo!.
Wapo watoto kibao hurushwa madarasa kutokana na uwezo wao mkubwa ktk masomo. Je, tuwaite nao kuwa na shahada zao ni feki kwa sababu hawakutumia miaka kumi na minne kumaliza high school? ama swala ni hicho chuo?
Je, elimu ya Phd ni lazima kweli mtu atumie miaka darasani?
Teknologia inazidi kupanda ndugu zangu, zamani nani angekubali kwamba tungeweza kuwasiliana kwa njia ya mtandao na kwa muda mfupi kiasi hiki, tena hata unaweza kumwona mtu live upande wa pili mki - chat!..watoto wadogo wanaichambua PC kwa utundu na hawakwenda darasani. Enzi zetu huwezi hata kufungua computer kama hukwenda shule mwaka mzima kujifunza DOS. Huendi darasa la kwanza bila kupimwa urefu wa mkono wako kushika sikio. Leo hii ni vichekesho na unaweza kusema hivi kweli mwingireza alikuwa na akili kuweka sheria kama hizo! Haya hizo simu siku hizi zinapiga picha, nyingine television na dira ya mji tena basi wavumbuzi wa vitu hivi hawana elimu kubwa sana isipokuwa vijana wadogo wabunifu. Elimu inazidi kukua kila siku na imekuwa rahisi zaidi maanake siku hizi hata fimbo hazitumiki tena.

Mchonga kaondoka na elimu yake akifahamu Pluto ni sayari!...
 
Back
Top Bottom