Baadhi ya google apps ni nzuri sana zaidi ya samsung apps

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Mimi sio mtaalam sana wa mambo ya simu na computer.

Jana katika kupita pita mitandaoni nikaona mjadala wa google apps ambazo unaweza kuziweka kwenye samsung na zikafanya vizuri zaidi.

Kweli nikaweka google massages, google contacts na google phone app kwenye samsung yangu, aisee nimezipenda sana. Ziko vizuri kuliko defaults apps za Samsung.

Nimekuja kugundua pamoja na kuwa huwa nanunua high end devices ila mahitaji au matumizi yangu kwenye hizo devices haizidi 5%. Natama nianze kujifunza ku-utilize haya makitu aisee. Juzi juzi nilipewa zawadi ya laptop hp envy 360, 20GB RAM, 1TB SSD, 4 core na mambo mengi ila nimeishia kuweka picha na few docs imekaa hapo. Natamani hata ningekua napenda movies au games nijaze humo lakini bahati mbaya sipendi.

Naomba kujua apps nyingine zinazotumika kwenye google au pixel phones exclusively ambazo naweza kuziweka kwenye samsung.

Natumia Note 10+.
 
Kwani haiwezekani...??

Sent using Jamii Forums mobile app
Achana na watu wajinga mkuu. Hawajawahi kuona sasa utawaambiaje waamini wakati hivyo ni vitu vinazidi uwezo wao wa kufikiri?

Mwaka 2018 Lenovo walizindua Think Pad yao ina ram ya 128GB.

Hawa wamezoea laptop ya GB 4, sio rahisi kuelewa kua zipo hadi za GB 128.
 
Achana na watu wajinga mkuu. Hawajawahi kuona sasa utawaambiaje waamini wakati hivyo ni vitu vinazidi uwezo wao wa kufikiri?

Mwaka 2018 Lenovo walizindua Think Pad yao ina ram ya 128GB.

Hawa wamezoea laptop ya GB 4, sio rahisi kuelewa kua zipo hadi za GB 128.
512gb,1gb,1.5gb,2gb,3gb,4gb,6gb,8gb,12gb,16gb,32gb

umeona shida ikoo wapi!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapo kisichowezekana ni kipi au kipi ni kigumu kwako? Hujawahi kuona laptop yenye ram ya 20GB ama nini? Au mtu hawezi kupewa zawadi laptop ya gharama hiyo?

Kigumu kwako hapo ni kipi nikusaidie?
Ndio shida ya watu wengi. Kitu asichokijua anaamini hakipo. Mtu computer alizoona ni zile za Gb 4.

Usimlazimishe mtu mkuu, waache na ujinga wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unaweza kuweka vizuri model ya hiyo machine tuicheck google? Maana nyingi hapa naziona zina RAM ya 12GB, 16GB

*Najua RAM Ipo zaidi ya hiyo Ila naongelea hp envy.

Screenshot_20200426-173133.jpg
 
Kwani haiwezekani...??

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana sana tena hata 32gb but ngumu hp kutengeneza laptop halafu aweke gb16 na gb 4 kwanza mashine inaweza hata isdisplay then hasara kupiga combi hiyo.

halafu hakuna ram ya gb 12 pekee kusema aongeze na nane ifike 20 gb. Mfulizo wa ram ni ukiachana na ndogondogo katika DDR 4 unaenda hivi 4g 8gb 16gb 32gb 64gb 128gb nk
Afadhari angesema gb 16 ama 24 au 32 kidogo ingeeleweka
Kumbuka laptop ina slot mbili za ram

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom