Cesar Saint
JF-Expert Member
- Nov 18, 2016
- 424
- 725
Habari Great Thinkers ....
Katika jamii zetu za kiafrika kumekuwa na mambo(desturi) kadha wa kadha ambazo kwa namna moja au nyingine zimekuwa zikitudumaza ama kutuchelewesha kwenye maendeleo katika nyanja ya kifamilia na jamii kwa ujumla .
Leo ningependa kuongelea desturi moja ambayo hurudisha nyuma jitihada za kimaendeleo ya kifamilia hasa upande wa uchumi.
Tuanze na maana ya maneno haya;
* Jamii ni istilahi inayoelezea uwepo wa pamoja wa mwanadamu hivyo basi katika kukua na kuendelea kwa mwanadamu kuna matendo au mitazamo ambayo inampasa kubadilisha au kuachana nayo kutokana na kujifunza zaidi ama kupata taarifa zaidi ya jambo husika.
* Desturi (kutoka Kiarabu) ni jambo la kawaida linalotendwa na jamii fulani mara kwa mara. Neno hilo ni sawa na mazoea, ada au kaida.
Katika mambo(desturi) haya mengi tunayopaswa kuondokana nayo miongoni ni UTARATIBU WA KUGAWA MALI ZA MAREHEMU (MIRATHI).
Kumekuwa na taratibu mbali mbali zinazoongoza swala hili kuanzia katika sheria za nchi,mila na hata kwa upande wa dini . Mwisho wa siku familia hufikia kwenye kugawiana sehemu ndogo ya mali au mirathi katika yale yalioachwa na marehemu .
Wengi wao huonelea njia hii kama mbadala wa kuepusha magomvi katika familia na kutenda hali kwa kila mwenye stahiki na mirathi husika.
Lakini Swali la kujiuliza Je, Tendo hili au desturi Hii ni jambo lenye tija kwa ustawi wa familia husika? Je, Kugawana mali kunachagiza ukuaji wa uchumi wa familia husika?
Kwa mtazamo wangu nafikiri ni ngumu sana au inahitaji mapambano makali kufikia kilele cha mafanikio katika nyaja ya kiuchumi (Utajiri).
Lakini ni njia rahisi endapo familia au ukoo utapitia mchakato wa “Generational building of wealth “ ambapo kila generation itakuwa na jukumu inalotekeleza katika kujenga uchumi wa familia au ukoo.
Kwa mfano ni rahisi sana kwa mjukuu kujenga kama babu alinunua na kuwekeza katika Ardhi au kwa namna nyingine ni rahisi sana kwa mtoto kuanzisha kiwanda na kampuni ya kuchakata mazao ya kilimo kama baba aliwekeza katika kilimo cha biashara.
Katika hatua hizi zote utaona ukuaji wa uchumi kutoka generation moja kwenda nyingine . Hapa ndio inakuja tofauti ya “Being Rich and Being Wealthy” familia iliojenga uchumi wake ni ngumu kuyumba kiuchumi hata pale kiongozi wa familia anapoanguka (Kufariki).
Sasa tukirudi kwenye ile desturi yetu ya kugawana mali za mwendazake inanyong’onyeza hatua za ukuaji wa uchumi wa familia husika na kuwarudisha nyuma zaidi au kupunguza matokeo chanya ambayo wangepata.
Nafikiri ni wakati sasa jamii zetu kuamka na kuanza kutengeneza kampuni ambazo wana familia watakuwa sehemu ya bodi za hizi kampuni na kusimamia biashara au miradi au vyazo vyovyote vile ambavyo mwendazake aliacha kuviendeleza badala ya kuvigawa (kuvitawanya) .
Hili litawaimarisha kiuchumi na kuleta tija zaidi. Umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu na huu ndio umoja thabiti .Kila hatua za maamuzi zina changamoto zake lakini faida uliyopo kwenye uamuzi wa aina hii ni kubwa kuliko kugawana kidogo kidogo katika kile kingi.
Naomba kuwasilisha.