Baadhi ya dawa zinaweza kuathiri uwezo wa kumbukumbu wa ubongo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
Ubongo.jpg


Kama tunavyofahamu, uzee, ugonjwa wa mishipa ya damu ya ubongo, na ukosefu wa virutubisho ni chanzo kikuu kinachoathiri uwezo wa kumbukumbu, lakini baadhi ya dawa pia zinaweza kupunguza uwezo wa kukumbuka.

1. Dawa za kutibu ugonjwa wa Parkinson.

Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kutibu ugonjwa wa Paikinson yanaweza kusababisha mgonjwa kushikwa na usingizi na kuathiri uwezo wa kukumbuka.

2. Dawa za kutibu kifafa
Matumizi ya muda mrefu au kupita kiasi ya dawa za kutibu kifafa yanaweza kupunguza akili za wagonjwa.

3. Dawa za usingizi
Dawa nyingi za usingizi zinaweza kufanya mtu alale vizuri na kuepuka mawazo, lakini zinaweza kusababisha watumiaji kutegemea dawa hizo na uwezo wao wa kumbukumbu kupungua.

4. Dawa za kupunguza shinikizo la damu
Matumizi ya muda mrefu ya dawa hizo yanaweza kusababisha hali ya polepole kujibu, kutoweza kuzingatia jambo moja au kushikwa na usingizi.



Ukiwa na Shida yoyote ile unaweza kunitafuta Kwa mawasiliano Kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
 
vipi zile dawa za chenga za mafua mana mkewangu kwa kubugia hiyo midawa hatari sababu mafua kwake hayamuishi hasa asubuhi na aipiti wiki bila kumchaia ndo humeza hizo dawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom