Baadhi ya dalili za Msongo wa mawazo (signs of stress) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baadhi ya dalili za Msongo wa mawazo (signs of stress)

Discussion in 'JF Doctor' started by nkisumuno, Jul 15, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Msongo wa mawazo una madhara makubwa katika kila sekta, mfano daktari mwenye msongo wa mawazo anaweza kumpa dozi isiyostahili mgonjwa na kusababisha madhara zaidi ikiwa ni pamoja na vifo. mwalimu anaweza kufundisha au akawa mkali kwa mwanafunzi kwa vile tu anamsongo wa mawazo, wakati mwingine anaweza kutoa adhabu asiyostahili mwanafunzi Anayefanya viwandani au kushughulika na mashine anaweza kuharibu vifaa au kuweza kupata ajali kwa kujikata na mashine kwa vile tu anamsongo wa mawazo. Hivyo ni vema ofisi ziwe na wanasihi kwa kila sekta ili watu wapate nafasi ya kupata msaada wa kisaikolojia ili kupunguza msongo wa mawazo. Zifuatazo ni baadhi ya dalili za msongo wa mawazo 1.kula sana au kupoteza hamu ya kula 2.kukosa usingizi au kulala usingizi sana 3.kupenda vitu vitamu kama vile pipi, biskuti, soda 4.kunywa pombe sana 5. Kupoteza hamu ya tendo la ndoa au hamu ya tendo la ndoa kuzidi 6. Kupoteza hamu ya kuwasiliana na ndugu au marafi (Kuwachukia) 7. Kujiskia mchovu bila sababu za msingi Hizo ni baadhi tu ya dalili za msongo wa mawazo. Ili kupunguza msongo wa mawazo (stress) fanya yafuatayo 1. Fanya mazoezi ya viungo kama kukimbia, kuendesha baiskeli nk 2. Punguza vyakula vya mafuta, kula mboga na matunda kwa wingi 3. Jithidi kuwa jirani na mtu unayempenda au kundi la watu baadala ya kuwa peke yako 4. kama kuna mnasihi jirani unayemfahamu mwombe ushauri 5. Fanya kitu unachokipenda kama vile kuangalia mpira, tv nk 6. Punguza kufanya kazi, uwe na muda wa kupumzika Nimejaribu kuonyesha kwa ufupi umuhimu wa Unasihi katika jamii ya kitanzania Nawasilisha .
   
Loading...